Ubora wa vyuo vikuu duniani: Oxford chaongoza duniani, Cape Town chaongoza bara la Afrika

Bora hata UDOM cha majuzi tu hakina hata historia,ila wama UDSM wamekuwa wakitamba sana kwamba ni chuo bora Africa Mashariki na kati,nashangaa hata hakikuzungumziwa.Tatizo ma prof badala ya kujikita na utafiti wanafanya siasa.
Usimwamshe aliyelala........
 
_91344199_9ba38105-603d-4b23-a9e8-852c43503e00.jpg


Chuo kikuu cha Oxford kimeibuka kidedea katika orodha ya vyuo vikuu bora duniani ya Times Higher Education. Hi ni mara ya kwanza kwa chuo kikuu cha Uingereza.

Oxford imeisukuma katika nafasi ya pili, California Institute of Technology, ambayo imekuwa ikiongoza orodha hiyo kwa miaka mitano iliopita .

Katika orodha ya vyuo vikuu bora barani Afrika, chuo kikuu cha Cape Town kimeibuka wa kwanza kutoka Afrika kusini kwenye orodha hiyo ya Times Higher Education.

Inadhihirisha umahiri wa taifa hilo, ambalo vyuo vyake vikuu 6 vipo katika nafasi za vyuo vikuu 15 bora kikwemo chuo cha Witwatersrand katika nafasi ya pili, Stellenbosch nafasi ya tatu, tChuo kikuu cha KwaZulu-Natal katika nafasi 5 na chuo kikuu cha Pretoria katika nafasi ya sita.

Makerere kilichopo Uganda ndiyo chuo kikuu nje ya Afrika kusini kufanikiwa kuwa atika nafasi ya nne.

Vyengine ni chuo kikuu cha Ghana katika nafasi ya 7, na chuo kikuu cha Nairobi katika nafasi ya 8.

Orodha ya Times Higher Education duniani inapima vitu kama mafunzo, utafiti, na mtazamao wa kimaaifa - kwa mfano, idadi ya wanafunzi wanaotoka nje na wafanyakazi.

Nico Cloete, mkurugenzi wa taasisi ya Higher Education Trust na mratibu wa utafiti wa elimu ya juu na Advocacy Network in Africa, anasema taasisi hizo nne katika orodha ya Afrika - Cape Town, Makerere, Nairobi na Ghana - "zimeidhinisha mipango ya kuwa vyuo vikuu vinavyoongoza kwa utafiti" nchini mwao na vimeshuhudia "ongezeko kubwa kwa wanaofuzu kwa ushahada ya uzamifu na kuunda taasisi za utafiti katika miaka mitano iliopita".


Chanzo: BBC Swahili

Vyuo 30 bora Afrika.

Rank
1 University of Cape Town - South Africa
2 University of the Witwatersrand - South Africa
3 Makerere University - Uganda
4 Stellenbosch University - South Africa
5 University of KwaZulu-Natal - South Africa
6 University of Port Harcourt - Nigeria
7 University of the Western Cape - South Africa
8 University of Nairobi - Kenya
9 University of Johannesburg - South Africa
10 University of Marrakech Cadi Ayyad - Morocco
11 University of Pretoria - South Africa
12 University of Ghana - Ghana
13 University of South Africa - South Africa
14 Suez Canal University - Egypt
15 University of Hassan II Casablanca - Morocco
16 Addis Ababa University - Ethiopia
17 Rhodes University - South Africa
18 University of the Free State - South Africa
19 North-West University - South Africa
20 University of Tunis - Tunisia
21 Ecole Nationale d’Ingénieurs de Sfax - Tunisia
22 Université Mohammed V – Agdal - Morocco
23 American University in Cairo - Egypt
24 Nelson Mandela Metropolitan University - South Africa
25 South Valley University - Egypt
26 Alexandria University - Egypt
27 Assiut University - Egypt
28 University of Sfax - Tunisia
29 University of Yaounde I - Cameroon
30 Minia University - Egypt
Ungeweka chuo cha 31,32,33 vingekuwa UDSM,UDOM na SUA bila shaka.
 
Chuo kama Makerere kimeshika nafasi ya 4 kwa sababu kimewekeza katika tafiti. Kuna tafiti za kilimo, afya na kiteknolojia na mchango wake ni mkubwa katika maendeleo ya nchi.

Na hii ndo kazi ya vyuo vikuu duniani, kufanya utafiti.

Mfano hapa chini angalia baadhi ya tafiti zinazofanywa na Makerere.
Research Projects
 
Tafuteni kimataifa link zote mnazojua nyie mkikuta The Open University of Tanzania ipo chini ya University of Masifa na Vipanga wa Kukariri na kumeza madesa(udsm) nitakuja kufuta kauli hapa

-Chuo wanafunzi wapo bash kila siku
-chuo wanafunzi(kiume) wanaingia class kaweka dawa nywele na kiduku kama cha SHEAMUS
-chuo wanafunzi kazi yao ni "ukitoboa coet ww kichwa" hata grade za concrete hawajui zinatumikaje(vipanga hao wa form 6) hawa tulikua nao field.
 
Ungekuwa una elimunzuri ungefahamu kuwa orodha ya vyou vikuu bora duniani hutolewa na taasisi nyingi tu sio hao 'times' peke yao. Kabla hujafikia conclusion ungetafuta orodha ya taasisi nyingine pia na pengine ungetambua vigezo vyao ni vipi. Usiwe kama wengine wanasema eti wahitimu hawajui kiingereza. Kuna wataalamu huko Japan hata maneno kumi ya kiingereza hana lakini hatari hao, usipime.Kufikiri na kufanya 'analysis' kuna hitaji weledi na sio papara kama hivi. Harvard, Stanford na Yale nivya ngapi katika hiyo list yenu?

Usiwe na shaka kuhusu elimu yangu. Ni nzuri sana. Nafahamu kwamba rating ya Times Higher Education inaheshimika sana. Nafahamu pia ziko rating agencies nyingine, na kwamba utafiti mwingi wa hizo ratings unafanyika kwenye internet. Najua chuo kimoja kilichopanda chati hatua nyingi sana kwa kuweka sawa website yao pekee.

Unaweza kucheki mwenyewe na kuona kwamba vyuo ulivyotaja vya Harvard, Stanford na Yale huwa siku zote viko nafsi za juu kwenye ratings za Times Higher Education.

Ukificha ugonjwa kifo kitakusema. Usitetee udhaifu uliojitokeza UDSM. Ni wa kutibu, na sio kuufunika kwa maneno.
 
  • Thanks
Reactions: Izc
UDSM imezorota siku za karibuni. Kiashiria kimoja ni website yao. Zamani ilikuwa imekaa vizuri, lakin sasa inatisha. Pull-down menu zake hazikupeleki popote penye habari za maana. Haikuwa hivyo miaka michache iliyopita.

Kama Makerere inaweza kwanini sisi tushindwe kufanya vizuri?

Ukiacha shule chache za binafsi, elimu imedorora sana Tanzania kwa ujumla. Maana inabidi kujenga toka kwenye msingi na sio kuanzia chuo kikuu. Hatua moja kubwa ya kwanza ni kurudisha HADHI ya waalimu katika jamii. Mwalimu anapashwa kuwa na hadhi sawa na daktari. That is the case in China. We can start by doubling or trebling the salaries of teachers. Inabidi tuanze sasa kutenga asilimia 27 - 30 ya bajeti iwe ya elimu. Na tufanye hivyo kweli, sio kudanganya hadharani kisha fedha hazitolewi. If you think education is expensive, try ignorance.
una mawazo jenzi mkuu. kwangu shida aliyeshikilia kijiti maskini. ni kama hajui hata
 
UDSM imezorota siku za karibuni. Kiashiria kimoja ni website yao. Zamani ilikuwa imekaa vizuri, lakin sasa inatisha. Pull-down menu zake hazikupeleki popote penye habari za maana. Haikuwa hivyo miaka michache iliyopita.

Kama Makerere inaweza kwanini sisi tushindwe kufanya vizuri?

Ukiacha shule chache za binafsi, elimu imedorora sana Tanzania kwa ujumla. Maana inabidi kujenga toka kwenye msingi na sio kuanzia chuo kikuu. Hatua moja kubwa ya kwanza ni kurudisha HADHI ya waalimu katika jamii. Mwalimu anapashwa kuwa na hadhi sawa na daktari. That is the case in China. We can start by doubling or trebling the salaries of teachers. Inabidi tuanze sasa kutenga asilimia 27 - 30 ya bajeti iwe ya elimu. Na tufanye hivyo kweli, sio kudanganya hadharani kisha fedha hazitolewi. If you think education is expensive, try ignorance.
una mawazo jenzi mkuu. kwangu shida ni aliyeshikilia kijiti maskini. ana hata chembe ya uabunifu wa hivo?
 
Ungekuwa una elimunzuri ungefahamu kuwa orodha ya vyou vikuu bora duniani hutolewa na taasisi nyingi tu sio hao 'times' peke yao. Kabla hujafikia conclusion ungetafuta orodha ya taasisi nyingine pia na pengine ungetambua vigezo vyao ni vipi. Usiwe kama wengine wanasema eti wahitimu hawajui kiingereza. Kuna wataalamu huko Japan hata maneno kumi ya kiingereza hana lakini hatari hao, usipime.Kufikiri na kufanya 'analysis' kuna hitaji weledi na sio papara kama hivi. Harvard, Stanford na Yale nivya ngapi katika hiyo list yenu?
Tanzania tunaanza kufundishwa kiingereza darasa la tatu. Sekondari hadi chuo kikuu masomo yanafundishwa kwa kiingereza. Hivyo si sahihi kulinganisha wasomi wa Japan na Tanzania kuhusu kujua kiingereza. Kutojua kiingereza kwa mtaalam aliyesomea TZ ni tatizo. Atajieleza kwa lugha gani? Au Kiswa-english!!
Hoja zako nyingine nakubaliana nazo. Nakutakia siku njema.
 
  • Thanks
Reactions: Izc
Ungeweka chuo cha 31,32,33 vingekuwa UDSM,UDOM na SUA bila shaka.
Kuna watu wanashangaa wakidhani hii ni mara ya kwanza kwa UDSM kutokuwapo kwenye orodha ya Times Higher Education! In short ni kwamba, hii si mara ya kwanza bali haijawahi kuwapo... labda miaka hiyoo!

Aidha, hata kama wataweka hadi 40 Bora, bado hakuna chuo cha Tanzania ambacho kitakuwapo kwenye hiyo orodha! The problem ni kwamba watu zamani walikuwa wanamezeshwa ranking za www.4icu.org. Ukiangalia hiyo ranking, UDSM na SUA utazikuta kwenye nafasi mzuri! Hata hivyo, tofauti na Times Higher Education, ranking ya 4icu haiangalii academic performance bali web popularity.

Mbali na Times Higher Education, wengine wanao-rank by academic performance ni URAP (University Ranking by Academic Performance)! Hapa napo, hata ukichukua vyuo 40 bora Afrika, hutaikuta SUA wala UDSM! Kwa mfano, ranking ya karibuni kabisa UDSM ipo nafasi ya 47, Sokoine nafasi ya 60. Hakuna chuo kingine cha Tanzania zaidi ya hivyo viwili! Chuo cha Makerere kipo nafasi ya 10 na Nairobi nafasi ya 20.
 
  • Thanks
Reactions: Izc
UDSM wameshupalia kuongeza degree programmes kwa UG bila hata kuzingatia rasilimali walizo nazo na miundombinu. mwisho wa siku ni kama shule ya kata tu... una rundo la wanafunzi unategemea hao wa hadhiri wafanye utafiti saa ngapi...... alafu kuna hatari kubwa zaidi wale wazee waliopo wakiondoka wote.maana wengi wa vijana wanao ajiriwa siku hizi ni majanga. wavivu na hawana moyo wa kufundisha kabisa
 
Back
Top Bottom