Uchaguzi 2020 Tunduma: Polisi Wawapandisha Kizimbani Wagombea Udiwani wa CHADEMA, Wadaiwa kufanya Wizi kwa kutumia Silaha, mmoja akosa dhamana

Libya

JF-Expert Member
Nov 11, 2016
783
1,918
Mgombea Udiwani wa CHADEMA Kata ya Majengo mjini Tunduma Boniface Mwakabanje ambae alikuwa anashikiliwa kwa ishu ya uraia, leo mchana amefikishwa Mahakamani na kupewa kesi ya 'Armed robbery' shitaka hili halina dhamana so kapelekwa magereza.

Uchaguzi 2020 - Tunduma yazuka vurugu na mabomu ya machozi yapigwa na polisi
1598285493709.png

Mgombea Udiwani wa Chadema Kata ya Majengo mjini Tunduma Boniface Mwakabanje​


====

Kufuatia kuwepo kwa matendo na matukio yanayoashiria kuwepo kwa mipango ya kuhujumu, kuharibu na kuvuruga Uchaguzi Mkuu, mwezi Oktoba, 2020, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinatamka ifuatavyo, kuhusu yanayoendelea kwenye maeneo hayo;

1. Tunduma
Tunaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua hatua za haraka dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa Kanuni na Maadili yq Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, vinavyofanywa na mamlaka za kiserikali ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Wilaya ya Momba, kuratibu mipango ya kuhujumu wagombea ubunge na udiwani wa Chadema wasiweze kurejesha fomu.

Mipango hiyo tayari imeanza kutekelezwa ambapo Mgombea wa Udiwani Kata ya Majengo, Boniphace Mwakanjabe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Tunduma, baada ya kukamatwa jana, leo amefikishwa mahakamani akibambikiwa tuhuma za uvamizi wa kutumia silaha, kwenye kesi Na. 125/2020.

Wagombea wengine wa udiwani; Moses Mshami (Muungano), Florini Mwalongo (Maporomoko), na Hosea Kibwana (Kiloleni) wanatafutwa na polisi kwa ajili ya kuunganishwa kwenye kesi hiyo.

Aidha, kutokana na mipango hiyo yenye lengo la kuharibu uchaguzi, polisi wamemkamata Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Songwe, Stella Fiao ambaye amefunguliwa kesi Na. 126/2020 na kubambikiwa tuhuma za kutokuwa raia wa Tanzania, huku viongozi wengine wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wa Mkoa Ndugu Issakwisa Thobias Lupembe (Mwenyekiti wa Mkoa), Hamza Hussen Mpongolela, Kiswigo Mwakabanje, Eliah Mwabukusi, Mosses Ambilikile Mshani, Frowini Kasiani Mwalongo, na Osiah Anthony Kibwana, wakiendelea kusakwa ili waunganishwe kwenye kesi Na. 125/2020.

2. Masasi-Ndanda
Jeshi la Polisi leo majira ya asubuhi lilimkamata Mgombea wa Ubunge Jimbo la Ndanda, Castor Joseph Mmuni kwa namna ambayo ni kinyume cha utaratibu wa kisheria, kwa tuhuma ambazo hazijajulikana wazi, ambapo awali alivamiwa, kukamatwa kuwekwa kwa nguvu ndani ya gari na kutoweka kabla haijabainika kuwa anashikiliwa Kituo cha Polisi mjini Masasi.

3. Ruangwa;
Hadi sasa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ruangwa ameendelea kumnyima fomu Mgombea Ubunge wa Chadema Edgar Malimus Fakili, huku vitisho dhidi yake na wagombea wengine vikiendelea sambamba na vile wanavyopewa Viongozi wa Chama, wakitishiwa usalama na maisha yao kwa sababu ya Chadema kuweka wagombea ubunge na udiwani katika jimbo analogombea Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa. Watu wasiojulikana wamemfuata Mgombea Udiwani Kata ya Nandagala, Said Mnundumi ambaye ni mtu mwenye ulemavu, wakimtisha kuwa hatakuwa salama iwapo atarejesha fomu zake ili ateuliwe kugombea.

4. Morogoro Kusini (Morogoro DC)
Katika Jimbo la Morogoro Kusini, Morogoro DC, Msimamizi wa Uchaguzi naye ameendelea kumnyima fomu ya kugombea Mgombea wa Chadema John Mwenegoha, kinyume kabisa na taratibu zinazosimamia uchaguzi.

Hitimisho
Matendo na matukio hayo si tu yanahatarisha amani na usalama, bali pia yanahatarisha mstakabali wa uchaguzi wenyewe katika maeneo mahalia na Uchaguzi Mkuu kwa ujumla wake. NEC haipaswi kukaa kimya. Katika mazingira hayo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatakiwa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha wagombea wa Chadema wanapata fomu, wanarejesha fomu na wanateuliwa ili wakashindane kwenye sanduku la kura. Ukimya wa NEC utatafsiriwa kuwa ni kubariki na kuwa sehemu ya uvurugaji na uharibifu wa uchaguzi.

Imetolewa leo Agosti 24, 2020 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
 
Mbona RPC akihojiwa na EATV alisema hawaja mshikilia huyu mtu? Sasa naanza kuamini yale maneno ya kijana wa UVCCM niliyo yasikia leo asubuhi nikiwa wilaya ya Songwe mji wa Mkwajuni akisema wata wapunguza wagombea wa upinzani kwa msaada wa dola na tume maana kwenye sanduku la kura hawata shinda. Hiyo ndiyo Ccm ya mwenyekiti anae changisha hela za kujenga msikiti kanisani.. Shetana hana mti asio tua.
 
#Update_Kutoka_Tunduma

Mgombea Udiwani wa Chadema Kata ya Majengo mjini Tunduma Boniface Mwakabanje ambae alikuwa anashikiliwa kwa ishu ya uraia, leo mchana amefikishwa Mahakamani na kupewa kesi ya 'Armed robbery' shitaka hili halina dhamana so kapelekwa magereza.
Weka source ya information ikiwezekana charge sheet ili tuweze kwenda vizuri
 
Back
Top Bottom