Bulicheka na mkewe Lizabeta....(unaishaje huu wimbo wa Wagagagikoko?)
Na ule wa 'Makari hodari....yo yo yo '? unaishaje?
Kuna wanaokumbuka 'Someni Kwa Furaha' kitabu cha kwanza mpaka cha nne. Wagagagigikoko, Lizabeta na Bulicheka? Vitabu vya Alfu Lela U Lela, Abdul etc etc??
Ngoja turekebishe kidogo haka kashairi ka kuukaribisha mwenge.
Twakukaribisha Mwenge
Mgeni wetu uringe
na wenyeji tukuchunge
Huku tukishangiria
Nuru yako yatangaza,
kuwa umetoa giza,
nuru umeieneza,
hapa kwetu Tanzania.
Kwetu ukitoka mwenge,
uelekee mahenge,
kila mwaka tuupange,
kuja kututembelea.
Duh, yaani sijui kwa nini nilkuwa sijaipitia hii thread wandugu.
Nakumbuka Simulizi za Allan Quaterman na Bwana Gudi, na Mashimo ya Mfalme Selemani yaani utafikiri ni kweli kabisa.
Vinara wa Allan Quatrman ni Msolopa Gasi na Shoka la Ajabu liitwalo Inskoskazi, Namkumbuka Faulata, na Bibi Gagula
Jamani wengine tunakumbuka enzi zile tunapo rudi shule pale karume tunarudi na kuuza dawa za mbu jioni na kibatari huku wagambo wakitusumbua aah kweli tumetoka mbali hizi dawa zilikuwa za aina mbili kijani na nyekundu lakini kijani ndio zilikuwa mali yaani zinawaka kuliko hizi nyekundu sijuwi zilikuwa zinatengenezwa wapi hizi
Halafu tuna sema tunenda shule kumbe tunaishia sokoni kariakoo au feri mhh makubwa yamepita.
Stori za Juma Rose and Baraka?
Hizi stori zilikuwa zinanikosha ile mbaya, mwanzoni ngeli ilikuwa haipandi kabisaa, ila nilikuwa nikiona picha za Juma,Rose na baraka stori ilikuwa inapanda kwelikweli.ila stori ya mwisho ktk series za stori Za juma and baraka ilikuwa chapter ya mwisho wakati huo tuko darasa la saba, Juma anaaga anasema byebye, it was too emotional, from that moment i was not a kid again!
Halafu kwa Upande wa vitabu vya Kiswahili, nako ilikuwa burudani tupu.
stori kama KIBANGA AMPIGA MKOLONI, SIZITAKI MBICHI HIZI,SIKU YA GURIO KATERERO,BENDERA YA TANZANIA,ANDUNJE(mtoto mdadisi), NGANENEPA ANG'ATWA NA NYOKA,AHADI KUMI ZA MWANA TANU na nyingine nyingi zote ilikuwa burudani tupu.
Kweli wakati ule mtaala ulikuwa umetulia, kwa sasa hivi sifahamu mitaala ikoje lakini nakiri mtaala katika somo la kiswahili, ulikuwa umetulia.
Nimalizie kwa beti ninazozikumbuka(japo sizikumbuki vizuri sana) kutoka katika shairi la sizitaki mbichi hizi
Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia
hadithi uliyongoja leo ninakuletea
Alitoka siku moja njaa aliposikia
njaa aliposikia sungura nakuambia
Siku hiyo akaenda porini kutembelea
akayaona matunda mtini yameenea
sungura akayapenda mtini akasogea
Mtini akasogea sungura nakuambia
SIZITAKI MBICHI HIZI, sungura akagumia
naona nafanya kazi bila faida kujua
yakamtoka machozi matunda akalilia
Matunda akalilia Sungura nakuambia
Usifanye utani mkuu, kile Kiswahili tulichosoma sie enzi hizo kilikuwa kimetulia sana! Siyo sasa, wanetu hawajui tofauti ya "ndiyo" na "ndio" au "Hapa" na "apa" ama "Hicho" na "hiko". Yaani hapa umenikuna kinoma. Kwanza madarasa yale ya mwanzo kulikuwa na vitabu murua sana, kama kile cha Paulo na Selina (darsa la pili), Kuna hadithi za Kinango na Nzige, Heri Mimi sijasema na kadhalika. Ukija darasa la tatu ndio unakutana na akina Andunje, Nondo Mla watu, Twende Tukawinde, Jogoo Aliyesema (hadithi ya Pazi) na Sadiki na Sikiri.
SHAIRI LA SADIKI NA SIKIRI
Sikiri mimi masikini
Uvivu wangu nyumbani
Ukiwa huu wa njiani
Nakufa hapa kwa nini?
.....................>
Pia kitabu hiki kilikuwa na shairi la kuukaribisha mwenge, kama kuna mtu analikumbuka basi si vibaya akatukumbusha
Ukija Darasa la Nne ndio unakutana na Kibanga Ampiga Mkoloni, Ndoto ya Kimweri (chifu wa Wasambaa), Mkwawa Shujaa, Barua Kwa Mjomba Mndolwa na Siku ya Gulio Katerero (hadithi ya Kiiza).
Shairi la kitabu hiki linaanza hivi:
KAMA MNATAKA MALI
Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
Wakataka na kauli iwafae maishani
Akatamka mgonjwa, ninaumwa kweli kweli
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali
Roho naona yachinjwa, Kifo kimenikabili
Kama mnataka mali, mtayapata shambani
........................................>
Darasa la tano napo kulikuwa na mahanjamu yake. Nakumbuka hadithi kama ile ya 'Safari Yenye Mkosi', Vijana Wapiga Kambi Ngulwi, Ukakamavu, Kapulya Mdadisi, na kadhalika.
SHAIRI LA KITABI HIKI LINAANZA HIVI
Tumeizika elimu, elimu ya kizamani
Elimu ile haramu, maana ya kikoloni
Imetuishia hamu, kuiga ya ugenini
Elimu yetu ya sasa yawafaa wananchi
...................................>
Kitabu cha Kiswahili cha darasa la sita sikikumbuki vizuri, tulikuwa na mwalimu bomu sana ila nitajitahidi kukumbuka, nadhani kulkuwa na mada moja inahusu 'walowezi'.
Kwa upande wa darasa la saba mambo yalikuwa poa sana.
Kulikuwa na mada kama, Chuo Kikuu, Brown Ashika Tama, Jiji la Dar Es Salaam nk.
Kulikuwa na mashairi mawili katika kitabu hiki, moja linaanza hivi:
Ninaye ndege mzuri, mrembo wa Kupendeza
Rangi zake mashuhuri, ni nne nawaeleza
Ndizo rangi za fahari, urembo kuutimiza
Ndege huyu ndege gani, hapa Kwetu Tanzania?
..........................................>
NB:
Mkuu Gamba la Nyoka, enzi za mawaziri Mungai na Kapuya, walivuruga sana wizara hii ya elimu, yaani vila vitabu vimevurugwa sana baada ya kuunganisha baadhi ya masomo, yaani vitabu havina mshawasha kama vile vya mwanzo. nilivipitia kidogo mwaka 2001 kuangali yaliyomo, nilisikitika sana. Wanetu wanakosa mambo mengi sana kutoka katika vitabu vile. Sikatai kuwa walifanya vile ili kwenda na wakati, binafsi sikuona ubaya wa vile vitabu vya mwanzo.
Tuendelee na kumbukumbu hizi!
Mkuu IDIMI nashukuru sana mzee kwa information hizi, kwa kweli nimekumbuka mbali sana na najihisi hata machozi kunidondoka mtu wangu.
Nilikuwa dogo enzi hizo napiga soka balaa, begi kubwa mgongoni ndani madaftari kibao,Kuhusu ile Stori ya Twende Tukawinde ,nimeikumbuka majamaa wameenda kuwinda ngedere ,dingi kabeba gobore, dada yao kawaandalia Mabumunda. katika hiyo stori nakumbuka jamaa alivyokuwa akilalamika kwa machungu jinsi ngedere wanavyomaliza mazao shambani, nanukuu "Ni nani aliyekula Matango yetu?, huyu atakuwa ni Mnyonyaji".
Umenikumbusha tena kuhusu sikiri na Sadiki
Sadiki sasa ashiba
Chakula kingi kwa baba
Nirudi tena kwa baba
Nakufa hapa kwa nini?
Halafu kuhusiana Na Bendera ya Tanzania
kulikuwa na shairi pia, nakumbuka ubeti mmoja
wakoloni walifika,huku na dharau zao
Kudharau Afrika,kutukuza nchi zao
Sasa wanaaibika, hawana tena kikao
..........................,,,,>
Nakumbuka kidoogo kuhusiana na shairi hili
Twakukaribisha Mwenge
Mgeni wetu uringe
na wenyeji tukupambe
Huku tukishangiria!
Idimi unaikumbuka ngonjera ya(mimi nimeikumbuka kwa mbaali,nadhani nitakuwa nimekosea ila najaribu kuvuta feeling)
Dada Asha sikilza
Maneno ya kupendeza
Azimio la Arusha
Lilizaliwa Arusha
Arusha unaitaja
sijui inavyokuja
Azimio la arusha
Azimio kitu gani?