Tulipokuwa primary,unakumbuka?

...Halafu kulikuwa na kitabu kimoja cha English darasa la saba sikumbuki tittle yake lakini katika moja ya story zilizomo humo zinahusu Mfalme mmoja na jamaa mmoja anaitwa Abdul... Huyu jamaa kwenye picha zilizochorwa alikuwa anavaa kiatu mbele kimechongoka sana (mkuki moyoni) kwa hiyo alikuwa anampeleka mfalme na msafara wake mahali fulani. Naomba kwa anayekumbuka jina la kitabu na hiyo story ya Abdul na mfalme aendeleze.....Tumetoka mbali sana.....
 
Wakuu ni kweli hivi vitabu vilikuwa na lugha iliyotulia na mwelekeo unaojulikana maana vilikuwa vimejikitia katika dira na itikadi ya nchi, yaani Ujamaa na Kujitegemea. Ila kwa upande mwingine, lazima tukubali kuwa vilikuwa vimejaa sana propaganda za Mwalimu. Pia vina propaganda za kufagilia sana Marafiki zetu Wachina. Mimi niko katika harakati za kuvikusanya hivyo vitabu maana vinasawiri mtazamo wetu ulivyokuwa enzi za zidumu fikra sahisi za Mwenyekiti wa Chama. Cheki dondoo hizi kutoka ktika Tujifunze Lugha Yetu Kitabu cha 8 na cha 9 uone jinsi ujamaa na uzalendo vilivyokuwa vinahubiriwa kama imani:

Naye Baba wa Taifa, pongezi twamtakia,
Kwa wingi wa maarifa, nchi kuipigania
Twapata jambo la sifa, ujumaa kutujia.
Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa
(Ubeti wa 19 wa 'Nchi Yetu Tanzania')

Ujamaa (Ujamaa)
Ulipona (Ulipona)
Kwa sababu (Kwa sababu)
Ya mirija (ya mirija)
Mama (Mwalimu kasema)
kweli (mirija ikatwe)
(Ubeti wa 2 wa 'Wimbo wa Azimio' - huimbwa kwa kupokezana)

Nimempata kwa haki, ndege wangu namtunza,
Abadan hanitoki, sitaki kumpoteza,
Hata nikipewa laki, kwa pesa sitomwuza,
Ndege huyu ndege gani, hapa kwetu Tanzania?
(Ubeti wa 7 wa 'Kitendawili' cha Bendera ya Tanzania)

Kijana we kijana, (kijana wa kijiji)
Kijiji chakungoja.
Hasa wewe kukilinda.
Adui kuwashinda
Kijana we kijana
(Ubeti wa 2 wa shairi katika sura la 'Vijana Watayarishwa')

Nchi ya kwetu naitaja,
Tanzania
Nchi ya shangwe na Umoja,
Hiyo ni nchi yangu,
Hapo pote nipitapo sina pa kukaa,
Baba na mama wakaapo,
Huko kurudi kwamfaa

Mungu wa heri uulinde,
Muungano,
Naye Mwalimu kiongozi,
Pia shujaa Karume
Hapo pote nipitapo sina pa kukaa,
Baba na mama wakaapo,
Huko kurudi kwamfaa
(Ubeti wa 2 na 3 wa shairi katika sura ya 'Muungano')
 
Na hili shairi la 'Ujasiri wa Rais Nyerere' katika Tujifunze Lugha Yetu Kitabu cha 9 ndio funga Kazi kwenye Medani ya Propaganda!

1. Sisi Watanzania hakika yatupasa kuwashukuru mashujaa,
Katika nchi yetu wengi walijaribu na kwa kweli walitufaa,
Heko kwa shujaa wetu mkuu Rais Nyerere mwana wa Afrika,
Yeye hakika mjasiri na mtetezi wetu katika Tanzania.

Kibwagizo
Mengi aliyafanya Tanzania,
Na hata katika nchi za nje,
Uingereza, Amerika, pote katutoa,
Tuondoe utumwani.

2. Yeye mwalimu wetu mwana wa kizalendo apendaye ujamaa.
Kazaliwa Musoma mwaka ishirini na mbili kijiji Butiama,
Alijielimisha sana apate elimu bila ya kuchoka,
Mwaka Arobaini na tano, kapata shahada yake ya ualimu.

3. Kuipata shahada mwaka arobaini na tano, kafufua chama TAA.
Chama hiki cha TAA alikitumia kutuunganisha wote,
Alijitolea kufanya kazi zote bila tofauti,
Kukiongoza chama hiki pamoja na kufundisha mashuleni.

4. Kufuzu kwa mwalimu na kupata shahada hakukumtosheleza,
Arobaini na nane alifuzu mtihani chuo kikuu cha London,
Alijiandikisha tena katika chuo kikuu cha Edinburgh,
Na kupata shahada ya M.A. mwaka hamsini na mbili.

5. Kuwa kwake Ulaya, shujaa mwalimu, hakujirudisha nyuma,
Alikuwa tayari katika kupigana na beberu Mwingereza,
Hakuacha kupigania haki na usawa wa binadamu,
Alisema ukweli wote kwa hayo wanayotenda Wakoloni.

6. Vibaraka wakubwa mwaka hamsini na tano walitumwa UNO,
Nia za vibaraka ni kuitokomeza nchi yetu Tanzania,
Viongozi wetu wa TANU, walizitambua hila zao zote,
Naye shujaa wetu Mwalimu, alifaulu na kuwabwaga wote.

7. Aliporudi UNO, alijiuzulu kazi za kiualimu,
Na akajizamisha kwenye chama TANU bila kujali ijara,
Alionyesha ujasiri kufanya kazi isiyo na kipato,
Hakika hiki ni kitendo kilichokuwa cha kishujaa sana.

8. Shujaa wetu Nyerere alikuwa tayari kumshambulia mkoloni,
Alisema ukweli bila kufichaficha mabaya yao vibaraka,
Hakuwajali vibaraka, mabwana shauri wala Magavana,
Ingawa walimshambulia alikurupuka mikononi mwao.

9. Hamsini na nane, wajumbe wa TANU walikutana Tabora,
Kutaka kususia uchaguzi mkuu kwa sababu ya mseto,
Mwalimu akawaelimisha wajumbe umuhimu wa uchaguzi,
Na TANU ilivigombea na kuvinyakua hivyo viti vyote.

10. Hapo sitini na moja Mwalimu Nyerere akawa Waziri Mkuu
Baada ya siku chache hapo Januari alikiacha cheo chake,
Nia iliyo kubwa sana ni kuimarishwa kwa chama cha TANU
Na pia kutoa uhuru kwa aliye tayari kuiongoza nchi.

11. Ushujaa mwingine ni kuiunganisha Tanganyika na Unguja
Aprili sitini na nne, Marais wawili walikubali muungano,
Nao walishikana vema, bila kujali vitisho vyovyote,
Na Muungano uko imara, heko kwa viongozi wa Tanzania.

12. Hakika ya thabiti Rais Nyerere katika kauli zake,
Mwaka sitini na tano, Umoja wa Afrika ulipitisha Azimio,
Kususiwa kwa Mwingereza kutoa Rhodesea kwa Ian Smith,
Nyerere hakurudi nyuma, kawa mmojawapo kuvunja uhusiano.

13. Mjerumani naye wa huko Magharibi alitishia Tanzania,
Iwapo Tanzania itamkaribisha Mjerumani Mashariki,
Shujaa Mwalimu Nyerere hakugutuliwa na usemi wao,
Kawaambia kuviondoa vitu vyao vya Kijerumani.

14. Lengo lake Mwalimu kwa wana Tanzania ni kujenga Ujamaa,
Mwaka sitini na saba, mwezi Februari, Azimio katangaza,
Kuwaondoa wanyonyaji wa kila aina nchini Tanzania,
Makabaila na Mabepari na hao makupe wasionekane.

15. Nasi Watanzania, tuko nyuma yako ewe Mwalimu Nyerere,
Hatutarudi nyuma utuelimishapo na kutuongoza vema,
Twajua utaleta mengi, yenye manufaa nchini Tanzania,
Hata na Afrika ndima na Ulimwengu wote utaelimishwa.
 
...Halafu kulikuwa na kitabu kimoja cha English darasa la saba sikumbuki tittle yake lakini katika moja ya story zilizomo humo zinahusu Mfalme mmoja na jamaa mmoja anaitwa Abdul... Huyu jamaa kwenye picha zilizochorwa alikuwa anavaa kiatu mbele kimechongoka sana (mkuki moyoni) kwa hiyo alikuwa anampeleka mfalme na msafara wake mahali fulani. Naomba kwa anayekumbuka jina la kitabu na hiyo story ya Abdul na mfalme aendeleze.....Tumetoka mbali sana.....

Tales from the Arabian Nights? Mmh yaani mlikuwa mnasoma Alfu Ulela Ulela shuleni?
 
wakuu mnakumbuka zile nyimbo tulizokuwa tunaimba kwenye mchaka mchaka? it was very patriotic, Nakumbuka nyingi sana kama [Idi Amini akifa mimi siwezi kulia ntamtupa kagera awe chakula cha mamba, , kuna mapambano barani afrika ya kujikomboa na wale mabeberu hoya kaunda,samora,mugabe...nmesahau kidogo hapa, au jua lele litelemke baba nyota nazo zitelemke mama haiya iya iya mama. kma kuna mtu anazifahamu nzima nzima atuwekee hapa tujikumbushe. hvi cjku hizi bado wanakimbiaga mchaka mchaka
 
changarawe nalia kigeu kigeu nasema, shule yangu nnavyoipenda ntakunywa sumu juu yake..siri siwyi naumia naumia. mmalolasa malolasa malosa moyo wangu happy yeye ye malolasa happy yeye malolasa[/COLOR]
 
Hii thread kweli inakumbusha mbali mnakumbuka saa ya kwenda nyumbani!sasa sasa saa ya kwenda kwetu kwaheri mwalimu tutaonana kesho!au This is the time to say goodbye!
baada ya hapo ni nduki!Au ile saa ya kuitwa majina kama ulikuwepo na jana yake basi unasema jana na leo!
 
Tumetoka mbali:

Kazi zetu tayari, twende zetu nyumbani,
Tukifika Nyumbani tunakula Chakula,
Asante Mwalimu, kwaheri mwalimu.
 
...Halafu kulikuwa na kitabu kimoja cha English darasa la saba sikumbuki tittle yake lakini katika moja ya story zilizomo humo zinahusu Mfalme mmoja na jamaa mmoja anaitwa Abdul... Huyu jamaa kwenye picha zilizochorwa alikuwa anavaa kiatu mbele kimechongoka sana (mkuki moyoni) kwa hiyo alikuwa anampeleka mfalme na msafara wake mahali fulani. Naomba kwa anayekumbuka jina la kitabu na hiyo story ya Abdul na mfalme aendeleze.....Tumetoka mbali sana.....

Jamani natafuta hivi vitabu vya abdul, nitavipataje? kuna yeyote mwenye kujua?
 
Mimi naukumbuka kwa mbali sana kile cha Kalume Kenge aliyekataa kwenda shule na ile hadithi ya Paulo usije kucheza na sisi una mikono michafu,,,, Eebwaee kulikuwa kumekucha
Wazee mnanikumbusha mbali sana,,,, naanza kuwa mtoto ghafla
Wacha nikumbuke nitawapa mbili tatu hivi,,,, ha ha ha haaaaa
 
wakuu mnakumbuka zile nyimbo tulizokuwa tunaimba kwenye mchaka mchaka? it was very patriotic, Nakumbuka nyingi sana kama [Idi Amini akifa mimi siwezi kulia ntamtupa kagera awe chakula cha mamba, , kuna mapambano barani afrika ya kujikomboa na wale mabeberu hoya kaunda,samora,mugabe...nmesahau kidogo hapa, au jua lele litelemke baba nyota nazo zitelemke mama haiya iya iya mama. kma kuna mtu anazifahamu nzima nzima atuwekee hapa tujikumbushe. hvi cjku hizi bado wanakimbiaga mchaka mchaka

kuna wimbo huo wa mchakamchaka LY walikuwa wanupenda sana

"twamaliza maliza iyelele mama"
"twamaliza maliza iyeiyee"
"twalipua lipua iyelelemama"
"twalipua lipua iyeiye"
"iye iyeiyee iyeiye,iye iyeiyei".

halafu hapo mtu mmoja anachomekea
"kaburu kamata hiya"
"hiya hiya hiya"
 
kuna wimbo huo wa mchakamchaka LY walikuwa wanupenda sana

"twamaliza maliza iyelele mama"
"twamaliza maliza iyeiyee"
"twalipua lipua iyelelemama"
"twalipua lipua iyeiye"

Nimeukumbuka sana ule wimbo wa Jua lile literemke mama....
Wakati huo ni shule za Msondo tuu (shule za serikali tu) shule za binafsi (fm academia) hasa primary hazikuwepo.
 
Nimeukumbuka sana ule wimbo wa Jua lile literemke mama....
Wakati huo ni shule za Msondo tuu (shule za serikali tu) shule za binafsi (fm academia) hasa primary hazikuwepo.
...Wakati huo mchango shuleni kwa mwaka 20/= lakini daftari likiisha unampelekea mwalimu wa somo anakusainia unaenda kuchukua jipya stoo na mikebe (Mathematical set) ilikuwa tunapewa shuleni....Maisha yalikuwa murwaaaaaaaaaaaaaaa!!!! No ufisadi, No stress za uchavuzi wa mazingira hata kabali street hazikuwa nyingi sana kama sasa...
 
Walimu wetu bado ni hazina kubwa na bado wanaweza kutumika vyema kama wakiangaliwa.Mie mwalimu wangu wa hesabu anawapiga tuisheni ya hesabu wanangu kwa malipo ofcourse na anafurahi sana!!

Kweli walimu wamesahaulika kabisa. Hivi karibuni nilimtembelea mwalimu wangu aliyenifundisha shule ya msingi kaika maongezi akanambia wanafunzi wengi aliowafundisha ni maprofesa sasa ila yeye bado hathaminiki. Inasikitisha sana. Walimu wapewe haki zao kama watumishi wengine.
"Tuwape heshima na unyeyekevu walimu wetu" -Fresh Jumbe
Fikiria dunia bila walimu ingekuwa vipi?
 
Duh, kweli tunatoka mbali.

Nyambala,
Hivi yale mafuta uliyotaja hapo juu "Rays" na "Shanti" bado yapo? Nimecheka sana.
Jamani msisahau kuwa enzi za Waziri mkuu Sokoine watu tulivaa mashati yenye rangi za mawingu! Sijajua yalikuw yanazalishwa wapi, ila nina uhakika ilikuwa ni Tanzania hapa hapa..

Nani alikuwa Kaka Mkuu kama mimi hapa JF? Naoma tubadilishane uzoefu. Mimi nilikuwa kaka mkuu nikiwa darasa la sita.

Idimi mafuta ya "Rays" na "Shanti" moshi bado yanapatikana madukani.
 
Bulicheka na mkewe Lizabeta....(unaishaje huu wimbo wa Wagagagikoko?)

Na ule wa 'Makari hodari....yo yo yo '? unaishaje?
 
Hii thread kweli inakumbusha mbali mnakumbuka saa ya kwenda nyumbani!sasa sasa saa ya kwenda kwetu kwaheri mwalimu tutaonana kesho!au This is the time to say goodbye!
baada ya hapo ni nduki!Au ile saa ya kuitwa majina kama ulikuwepo na jana yake basi unasema jana na leo!

This is hilarious jamani kweli tumetoka mbali...duh
 
Idimi mafuta ya "Rays" na "Shanti" moshi bado yanapatikana madukani.

Sina la kusema kwa hili navunjika mbavu kwa kucheka, kweli watu mna kumbukumbu!!! mi wala sikuwa nakumbuka mambo ya mafuta ya Rays na Shanti ila sasa nimeyakumbuka yenyewe ya rangi ya chenza...kwe.kwe, kweeeee na kwa wale tuliosoma boarding hurudi shule bila shanti au rays matokeo yake darasa zima lanukia Rays na shanti.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom