Tulipokuwa primary,unakumbuka?

kuna thread nzuri kumbe huku, maana siasa pekee nazo hazi-siasiki, acha tuburudike huku!

mmhh!
 
My eyes are getting wet ninaposoma hii thread!!! So touching... nakumbuka mbali sana!!! Nikiwa Nyamatare huko Musoma... Maisha ya Primary yalikuwa na radha ya tofauti jamani...soooo special!

Nakumbuka kila alipokuwa akiingia darasani mwalimu wa kiswahili watoto wote hata waliokuwa vichakani walirudi darasani wengine kupitia madirishani (Dirisha ambazo zilikuwa zimeuzwa milango tayari!)

Nakumbuka wimbo huu ambao mwalimu wetu alikuwa akiuimba kila anapokaribia mlango wa darasa..

"Tanzania bara ooo ...na visiwani chatumika.
Kiswahili lugha..ya taifa X2
Na mikoani oooo... kimeenea kiswahili.
Kiswahili lugha..ya taifa X2

Wimbo huu ulikuwa ukipigwa pia kipindi kimoja cha RTD kila alhamisi saa nne usiku km kiashirio cha kipindi cha kiswahili.... Hata nikiwa sekondari nilikuwa nakuwa km mgonjwa nikiusikia wimbo huo!

INANIKUMBUSHA MBALI SAAANA JAMANI.... Nazitamani siku hizo!!! Kwetu najua hazitarudi lakini wanetu wangeziona hata kidogo my God!!
 
"Ngozi ya kenge ina madoadoa, inamaaa, inukaaa inamadoadoa"

..Mwanaidi na kikapu cha unga x2,
Ashikashika, aikokoa, aishikashika aikokoa.......!duuuh!

Hakiyanani.....darasa la kwanza hapo......!

Nani anamwogopa simba?......hatumwogopi,akija tutakimbia kimbia tuoneeeee!.....

hapo inakuwa patashika nguo kuchanika......!
 
..Mwanaidi na kikapu cha unga x2,
Ashikashika, aikokoa, aishikashika aikokoa.......!duuuh!

Hakiyanani.....darasa la kwanza hapo......!

Nani anamwoga simba?......hatumwogopi,akija tutakimbia kimbia tuoneeeee!.....

hapo inakuwa patashika nguo kuchanika......!

"Sasa, sasa, saa ya kwenda kwetu, kwaheri mwalimu kwaheriiiii, tutaonana keshoooooo! hapo kinachofata ni mbio
 
Of course hii thread imebeba mambo mengi sana ya shule za msingi za enzi hizo, ni burudani tosha sana.
Long Live JF
 
halooooo umenikusha mbaali sana...... heeeheeeeeee aaaa yaani jamani kweli tunajua tulikotoka
bali hatujui tuendako
 
hizo shule zilitupa uzalendo wa kweli kabisa maana tulikuwa tunajengwa hasa,
hiyo ya wababe wa shule sio mchezo, lazima na wewe uweke matuta kichwani na daftari moja mfuko wa nyuma alafu unatembea unadunda bega moja liko chini kidogo, nakumbuka mjomba wangu alikuwa baharia alkaniletea laba mtoni "spager" ilikuwa ya njano dah ilikuwa ni maisha ya kweli kabisa
 
"Sasa, sasa, saa ya kwenda kwetu, kwaheri mwalimu kwaheriiiii, tutaonana keshoooooo! hapo kinachofata ni mbio
.....he!he!he!heheeeee.....hii nayo La kwanza na la Pili......! daaa zamani hizo....natamani niwe mtoto kweli (JD)!
 
.....he!he!he!heheeeee.....hii nayo La kwanza na la Pili......! daaa zamani hizo....natamani niwe mtoto kweli (JD)!

Huu j, waukumbuka?
"Maua mazuri yapendezaa,ukiyatizamaa, yanameremetaaa.............."
NA
"Hii ndiyo "a" a a a inamkia mfupiii, a a a
 
Huu j, waukumbuka?
"Maua mazuri yapendezaa,ukiyatizamaa, yanameremetaaa.............."
NA
"Hii ndiyo "a" a a a inamkia mfupiii, a a a

...nimo humo as well.......! hapo kny hii ndio a,a,aaaa ina mkia mfupi .aaaa, hii ndiyo e,e,e,e iko kama kata eeeeee......! hapo ni wiki la kwanza tangia upelekwe shule......natamani niwe mtoto!
 
Nakumbuka hadithi za Floods in Ikwiriri Village (std four), Hibiscus flower (nadhani ni std five), The three Brothers( std six - kile kitabu chenye picha ya bendera ya taifa ikiwa mlima kilimanjaro na mkuu Nyirenda)
kila mwisho wa story kulikuwa na maswali ya multiple choice badi dada mmoja darasani mara nyingi alikuwa anashika nambaya mwisho kwenye mitihani ya mihula lakini siku moja peke yake darasani akapata maswali yote ya multiple choice. alipopewa maswali yaleyale maraya pili akakosa yote!

Wakati huo walimu wanashindana kufundisha wanafunzi, wale wa LY wanaendelea na masomo mpaka saa 12 jioni wakati wenzao wa lower classes wamesharudi nyumbani. Na wakati wa likizo ya mwezi wa sita LY hakuna kufunga. walimu wanajitolea kufundisha ili wafaulishe sana bila malipo ndiyo ilikuwa fahari yao.

wakati wa mchakamchaka nakumbuka wakati huo walimu waliokuwa wanatoka JKT (kwa mujibu wa sheria)walikuwa wanakuja na kombati za jeshi. basi walikuwepo walimu wanawake wawili shuleni kwetu wakiwa zamu walikuwa wanavaa kombati basi wakivaa hizo kombati mjua shughuli ipo siku hiyo.
 
Dah mie nakumbuka sana kulikuwa na kipindi cha sanaa, basi tunatoka nje kutengeneza vitu wenyewe kama ni magari ya mabox, vyungu na sometimes ngoma. hii ngoma naukumbuka sana wimbo huu ni vile tu hamtaweza kuipata tune lkn ulikuwa wimbo mzuri ajabu though siipendi CCM. uliimbwa hivi:
CCM oyee, CCM
Baba Nyerere amesema tukae pamoja,
CCM oyee, CCM
mengine yamenitoka.
kwa kweli jinsi tulivyokuwa tunaucheza nikikumbuka moyo waenda mbiooo.
 
Ishu ya kuwahi shule nayo inanikuna barabara, nilikuwa na Bro wangu mie nikiwa sts one yeye alikuwa darasa la nne, alikuwa ananiamsha saa kumi na moja asubuhi, kumi na mbili kasoro tunaondoka tunaelekea shule, tulisoma shule tofauti, sasa pale niliposoma mie kulikuwa kuna jamaa nashindana nae kuwahi shule, jamaa alikuwa kiboko hata niwahi vipi namkuta jamaa keshakoka na moto anaota, hahaha. ikifika moja kamili kengere ya namba inagonga, basi tunagombania namba Moja,. namba Tano na namba ya Mwisho kabisa.hapa sasa ndo maana Lady JD anatamani kuwa mtoto tena.
 
Hahahahahaaaaa, duh wakuu mmenikumbusha mbali sana, tulikuwa tukiwahi namba na endapo una mshkaji wako kachelewa unamuwekea jiwe au dumu la maji kwenye mstari ikiwa ni ishara kuwa kuna mtu, hlf Jumatatu na Alhamis ilikuwa ni ukaguzi, kuna mwalimu alikuwa na ruler ya mbao kwenye ukaguzi yeye alikuwa anapenda kutazama kucha tu, akikukuta na kucha ndefu unakula ruler za vidoleni sita! Hlf uniform ilikuwa ni viatu vyeusi au brown tu! Hahahaaaaa, ikifika wakati wa kuingia darasani baada ya assembly kuna band inapiga kama gwaride la jeshi vile! Hlf watoto wa kihindi na kiarabu ndo walikuwa matajiri zetu mida ya break, anakununulia mihogo ya kukaanga na visheti ili umpe ulinzi kwa wababe wa shule au umpange kwenye timu ya darasa! Duh it was sooo funny, I really miss those great great moments, hlf kuna mwalimu mkuu alinunua gari yake Land rover alikuwa akipaki chini ya mwembe karibu na assembly, hataki mtu aiguse, ukiigusa tu unakwenda kusafisha vyoo ambavyo vilikuwa vichafu balaa, alikuwa akiitwa Mwalimu Sitta, hiyo ilikuwa ni experience ya Lake Primary huko Mwanza! Miaka ya 86- 92!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom