Tulipokuwa primary,unakumbuka?

Nawapongeza wote ambao mmechangia ktk hili la kumbukumbu za Primary...its very interesting...Ushauri wangu MSIWASAHAU WAALIM WETU, WAZEE WETU HAO WALITULEA na hadi sasa wengine wapo hai lkn mishahara yao MIBOVU kupindukia...bado akina MRAMBA walienda kuwakopa...wakati wao wakikaa pale BOT siku moja tu mshahara wa mwalim mwezi mzima...KILA MMOJA AENDE ALIPOSOMA SHULE AKIWA NA CHOCHOTE AMTAFUTE MWALIM WAKE AMBAE ALIMTOA AKIWA HAJUI KUANDIKA WALA KUSOMA...
 
KILA MMOJA AENDE ALIPOSOMA SHULE AKIWA NA CHOCHOTE AMTAFUTE MWALIM WAKE AMBAE ALIMTOA AKIWA HAJUI KUANDIKA WALA KUSOMA...

mimi nilijua kusoma nikiwa shule ya vidudu!
na shule yenyewe is no longer there,
 
Ni wazo zuri kwenda kuwapelekea chochote walimu waliotufundisha, lakini wengi wameshastaafu na hata hatujui waliko, sasa hivi ukienda hapo shuleni unakutana na vibinti vidogovidogo vya Mungai vilivyosoma mwaka mmoja.
 
Data zao zipo ukiwa na Lengo la kuwasaidia utawapata...ukifanya juhudi kumtafuta hata mmoja ambae unaona anafaa kumsaidia. Kimsingi hali zao mbaya.
 
Ni wazo jema kuwakumbuka walimu wetu waliotufikisha hapa mpaka sasa wengine ni waheshimiwa. Inasikitisha kuona kwamba wanalipwa mishara ambayo inatia huruma mpaka leo.
Sema sasa kuna wengine wanapenda kwenda kuona shule walizosoma ila inakuwa ngumu kwenda kuwajulia hali walimu kwa sababu ya ukata na umbali. Unakuta mtu alisoma shule ya msingi "Mkwajuni" kule Tunduru Ruvuma ambako wazazi wake walikuwa anafanya kazi na kwa sasa anaishi Bunazi kule Kagera ambako kaajiriwa kama afisa utumishi. Mshahara wake tu hautoshi kumsafirisha kwenda Tunduru kuiona shule yake aliyosomea, ingawa anatamani sana kufika huko. Kwa hiyo inakuwa vigumu sana.
Ningependa kutoa mfano mmoja mzuri kwa hili. Kocha wa zamani wa Yanga bw Syllersaid Mziray, alikuja siku moja katika sekondari moja mkoani Iringa mwaka 1998, ambako inasemekana alisomea hapo na alifika mpaka bwenini alikokuwa analala. Kabla hajaondoka alitoa mipira ya miguu kadhaa na zawadi nyingine kwa shule yake. Ningependa kumuunga mkono sema sasa uwezo unanikaba sana ila inapendeza sana.

WITO KWA WANA JF
Ni vyema kama tutakuwa tunaitisha "Alumni" kule tulikosoma ili kusaidia shule zetu, kama mmoja alivyotamka hapo juu. Hii itasaidia sana kuziinua shule hizi kitaaluma na kimaendeleo kwa ujumla kwa sababu tutakuwa tunajadili mafanikio na matatizo yanayozikabili shule hizo.
 

Ngoja turekebishe kidogo haka kashairi ka kuukaribisha mwenge.



Twakukaribisha Mwenge
Mgeni wetu uringe
na wenyeji tukuchunge
Huku tukishangiria

Nuru yako yatangaza,
kuwa umetoa giza,
nuru umeieneza,
hapa kwetu Tanzania.

Kwetu ukitoka mwenge,
uelekee mahenge,
kila mwaka tuupange,
kuja kututembelea.

Mkuu IDIMI nashukuru sana mzee kwa information hizi, kwa kweli nimekumbuka mbali sana na najihisi hata machozi kunidondoka mtu wangu.

Nilikuwa dogo enzi hizo napiga soka balaa, begi kubwa mgongoni ndani madaftari kibao,Kuhusu ile Stori ya Twende Tukawinde ,nimeikumbuka majamaa wameenda kuwinda ngedere ,dingi kabeba gobore, dada yao kawaandalia Mabumunda. katika hiyo stori nakumbuka jamaa alivyokuwa akilalamika kwa machungu jinsi ngedere wanavyomaliza mazao shambani, nanukuu "Ni nani aliyekula Matango yetu?, huyu atakuwa ni Mnyonyaji".

Umenikumbusha tena kuhusu sikiri na Sadiki



ngoja niwakumbushe vizuri hapa,


Sikiri mimi masikini,
uvivu wangu nyumbani,
ukiwa huu njiani,
nakufa hapa kwa nini,


Sadiki sasa ashiba
Chakula kingi kwa baba
Nirudi tena kwa baba
Nakufa hapa kwa nini?

Halafu kuhusiana Na Bendera ya Tanzania
kulikuwa na shairi pia, nakumbuka ubeti mmoja

wakoloni walifika,huku na dharau zao
Kudharau Afrika,kutukuza nchi zao
Sasa wanaaibika, hawana tena kikao
..........................,,,,>



Nakumbuka kidoogo kuhusiana na shairi hili

Twakukaribisha Mwenge
Mgeni wetu uringe
na wenyeji tukupambe
Huku tukishangiria!

Idimi unaikumbuka ngonjera ya(mimi nimeikumbuka kwa mbaali,nadhani nitakuwa nimekosea ila najaribu kuvuta feeling)

Dada Asha sikilza
Maneno ya kupendeza
Azimio la Arusha
Lilizaliwa Arusha

Arusha unaitaja
sijui inavyokuja
Azimio la arusha
Azimio kitu gani?
 
Shairi la Mwenge ni hili hapa,

Twakukaribisha mwenge,
mgeni wetu uringe,
na wenyeji tukuchunge,
huku tukishangilia,

nuru yako yatangaza,
kuwa umetoa giza,
nuru umeieneza,
hapa kwetu Tanzania.

kwetu ukitoka mwenge,
uelekee mahenge,
kila mwaka tukupange,
uje kututembelea.

Wakati nasoma enzi hizo nilihakikisha najua shairi kabla mwalimu hajafikia ukurasa huo.

Na lile la bendera ni hili hapa,

Bendera ya Tanzania, ndiyo ya kujivunia,
ilianza kupepea, mwaka sitini na moja,
hapo tunashuhudia, tunavyojitegemea,
hapa kwetu Tanzania, uhuru umechanua.

Bendera yetu mwanana, yajulikana bayana
Duniani twatukuka, katu hatuwi mateka,
Bendera yapeperuka, Uchina na Amerika,
Wala haitatuka, na juani kuchujuka,

Rangi ya chanikiwiti, yaonyesha mbuga zetu,
Ya njano ndiyo madini, yaliyo nchini mwetu,
Bluu huonyesha maji, yaliyo nchini mwetu
Nyeusi ni yetu sisi, Waafrika asilia.
 
.......KILA MMOJA AENDE ALIPOSOMA SHULE AKIWA NA CHOCHOTE AMTAFUTE MWALIM WAKE AMBAE ALIMTOA AKIWA HAJUI KUANDIKA WALA KUSOMA...

Makala ya zamani sikuiona wakati huo.
Mwalimu wangu wa kwanza alikuwa dada yangu baada ya kugoma kusoma kile ki shule cha Vidudu pale Ilala flats miaka hiyo ya 70 katikati. Kisa ni kuwa nilikuwa naona nitachekwa na kaka zangu nikirudi kijijini Sikonge. Mwalimu wangu wa kwanza Primary - Sijui kama yuko hai ila nduguze wanapatina. Huyu mzee alikuwa ni babu tayari wakati naanza shule - Heshima mbele kama bado yuko hai Mwalimu Malembeka aka Makoviki.
Katika walimu waliosaidia sana kukuza elimu kule kwetu Sikonge ni Kauga na Kalangu. Haya majina kweli yamesomesha wengi saana kule kwetu. Wengine kwa mbali ni Yongolo, Saudi (Mmalawi), Mbelwa, Nkulu (alitokea Singida), Lwambano, Nyanza, Loya, Mlimuka, Baruti, Katala, Kadete, Kanumba, Kavalambi etc etc.... Hawa wamebadilisha maisha ya wengi. Kuja kupata walimu kama hao kwa kweli itakuwa miujiza.... Na wote niliowasahau natoa hongera zangu nyingi sana kwao. Hata kama hapa duniani hamkupata malipo, Mungu juu atakulipeni.
Mwisho kwa Mwalimu JK Nyerere. Bila ya huyu, mie nisingelikuwepo hapa (maneno ya marehemu baba yangu).
 
Enzi hizo mtu akifaulu (kuchaguliwa) darasa la saba kwenda form one nyumbani inakuwa bonge la shangwe lakini si siku hizi hamna tena hiyo sherehe maana ni muda wa mzazi kujikuna kumpelekea mamilioni mama Lwakatare (St. Marys) tehe tehe !
Dah mkulu umenikumbusha pa kunikumbusha.....Yaani we acha tu.
Mwenzio nilipewa zawadi ya saa. Nikaambiwa niivae first week ya orientation ya form one, halafu then ikawa nnatakiwa niivae kwa mtoko...Was a long time.....Its so touching.
 
USHINDI WA MAHABA, UMEWAHI KUKISIKIA AU KUSOMA?

Oya washikaji kama kuna mtu anacho kitabu USHINDI WA MAHABA naomba aniazime ili nisome tena. Nilikisoma nikiwa kitu kama darasa la saba au form one hivi na sijawahi kusoma love story nyingine kama ile!!!! And mind u, mi nasoma vitabu ati!
 
Mnakumbuka "KITABU CHEUSI???????",iliaminika kabisa ukiandikwa humo wewe utakuwa na maisha mabaya kweeli baadaye. Kuna mshikaji aliandikwa tukiwa darasa la nne tulikuwa tunaogopa hata kutembea naye maana ilionekana atatuambukiza the expected misfortunes......... Kweli tumetoka mbaaaali
Dah nakumbuka hicho kitabu mkuu...tulikuwa nacho pale skonga....Kuna mshkaji hivi sasa ni mkubwa katika taasisi fulani dar, ilikuwa darasa la tano kama sikosei. Somo la sayansi kilimo, si unajua tena darasa la tano yanaongezeka masomo mawili kama nakumbuka vizuri (Kilimo na Historia), Basi mimi na mshkaji tukawa tunajifanya watoto wa mjini hatutaki kusoma sayansi kilimo tunaingia mtini kipindi chake. Tuna recruit watu wengine kuandaa mechi na shule ya jirani. Basi huo ndio ulikuwa mchezo wetu kwa kipindi kadhaa, kilichoniepusha mimi kuingia kwenye black book ni kuwa madarasa mengine naatendi ila mshkaji wangu yeye akafanya across the board.
Siku za mwizi arubaini....siku hiyo tukakamatwa tukapigishwa magoti katikati ofisi ya walimu tukaanza kusimangwa na walimu wote. Hata huko namuona mwalimu mkuu anaingia na black book mkononi, nilitamani ardhi ipasuke niingie, nikaponea chupuchupu tu kwa sababu mdingi alikuwa katika bodi ya udhamini wa shule (Sijui ndo ufisadi wenyewe huo) anyway..... Mshkaji akaingizwa kwenye black book. Jamaa ilibidi ahame shule sababu ilikuwa noma after that. Hata mechi za madarasa A na B pia ilikuwa hapati namba....Long time!!!!
 
Wakuu, mmenikumbusha mbali sana.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia;
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikia;
Usichoke kujikaza, mazuri kukazania;
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.
 
Stori za Juma Rose and Baraka?
Hizi stori zilikuwa zinanikosha ile mbaya, mwanzoni ngeli ilikuwa haipandi kabisaa, ila nilikuwa nikiona picha za Juma,Rose na baraka stori ilikuwa inapanda kwelikweli.ila stori ya mwisho ktk series za stori Za juma and baraka ilikuwa chapter ya mwisho wakati huo tuko darasa la saba, Juma anaaga anasema byebye, it was too emotional, from that moment i was not a kid again!

Halafu kwa Upande wa vitabu vya Kiswahili, nako ilikuwa burudani tupu.
stori kama KIBANGA AMPIGA MKOLONI, SIZITAKI MBICHI HIZI,SIKU YA GURIO KATERERO,BENDERA YA TANZANIA,ANDUNJE(mtoto mdadisi), NGANENEPA ANG'ATWA NA NYOKA,AHADI KUMI ZA MWANA TANU na nyingine nyingi zote ilikuwa burudani tupu.

Kweli wakati ule mtaala ulikuwa umetulia, kwa sasa hivi sifahamu mitaala ikoje lakini nakiri mtaala katika somo la kiswahili, ulikuwa umetulia.

Nimalizie kwa beti ninazozikumbuka(japo sizikumbuki vizuri sana) kutoka katika shairi la sizitaki mbichi hizi

Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia
hadithi uliyongoja leo ninakuletea
Alitoka siku moja njaa aliposikia
njaa aliposikia sungura nakuambia

Siku hiyo akaenda porini kutembelea
akayaona matunda mtini yameenea
sungura akayapenda mtini akasogea
Mtini akasogea sungura nakuambia

SIZITAKI MBICHI HIZI, sungura akagumia
naona nafanya kazi bila faida kujua
yakamtoka machozi matunda akalilia
Matunda akalilia Sungura nakuambia


Jamani umenikumbusha mbali sana yaani nimesoma mpaka machozi yamenilengalenga....kweli "Old is Gold" I miss those moments..sijui nitawatafutaje marafiki zangu wa primary hata sijui pa kuanzia...
 
Mh imenikumbusha mbali, nakumbuka hadithi ya kwanza ya kitabu cha darasa la kwanza, JUMA NA ROZA

Huyu ni Juma,
Juma ana dada,
Dada yake ni Roza,
Juma anasema,
Tia sukari Roza,
Tia maziwa,
Roza una kiu?
Kunya chai Roza.


Na pia kama sikosei kitabu cha darasa la tatu kilikuwa na hadithi ya Selina na Mariamu walienda msituni, na kuna picha wanaruka kamba, na mwisho kilikuwa kina hitimisha na hadithi ya watu walikuwa wanataka kuchagua kiongozi wao, na kulikuwa kuna picha ya wananchi na mtu mrefu kuliko wote.

OMG, this is superb hata ukiniamsha usingizini nilikuwa naweza ku-narrate hiki kitabu. It was amazing; hivi tulikuwa tunasomaje miaka hiyo? nadhani ilikuwa ni yale mambo ya kukariri sidhani kama wanafanya hivi siku hizi, mhh tumetoka mbali kweli.
 
Primary school kabla ya ukaguzi utasikia kiranja akisema

.......Mikono mbele, juu, kando, chini.

.......Shoto kulia shoto kulia, nyumaaaaaaaaaa geuka

......Mguu pandee, mguu sawa,legeza mwili (ukikosea, AJUWA)

......Walio mbele, nyumaaaaaaaaa geukaaaaaa

......Mstariiiiiiiiiiii nyoosha (hapo kila mwanafunzi anajificha mgongoni kwa mwenzie bila kutokeza kichwa)


Jamani mnanimaliza yaani nacheka mpaka mbavu zinauma kweli ya kale dhahabu, tuanze kutaja shule za msingi tuzlizosoma labda tutakuwa tunajuana humu....
 
Jamani mnanimaliza yaani nacheka mpaka mbavu zinauma kweli ya kale dhahabu, tuanze kutaja shule za msingi tuzlizosoma labda tutakuwa tunajuana humu....
Sana tu na mimi nililifikiria hilp hilo hilo la kutaja shule lakini nikaona kuna unspoken rule ya kutomention identities humu kijiweni. Na mmoja akianza tu mimi nitafuatia. Na ili kuepusha watu kuongopea, watoe na kaishu fulani hivi ambacho kinaambatanisha na kuwa mwenyeji wa mazingira hayo. Ni wazo tu!!
 
Nawapongeza wote ambao mmechangia ktk hili la kumbukumbu za Primary...its very interesting...Ushauri wangu MSIWASAHAU WAALIM WETU, WAZEE WETU HAO WALITULEA na hadi sasa wengine wapo hai lkn mishahara yao MIBOVU kupindukia...bado akina MRAMBA walienda kuwakopa...wakati wao wakikaa pale BOT siku moja tu mshahara wa mwalim mwezi mzima...KILA MMOJA AENDE ALIPOSOMA SHULE AKIWA NA CHOCHOTE AMTAFUTE MWALIM WAKE AMBAE ALIMTOA AKIWA HAJUI KUANDIKA WALA KUSOMA...


Walimu wetu bado ni hazina kubwa na bado wanaweza kutumika vyema kama wakiangaliwa.Mie mwalimu wangu wa hesabu anawapiga tuisheni ya hesabu wanangu kwa malipo ofcourse na anafurahi sana!!
 
Sana tu na mimi nililifikiria hilp hilo hilo la kutaja shule lakini nikaona kuna unspoken rule ya kutomention identities humu kijiweni. Na mmoja akianza tu mimi nitafuatia. Na ili kuepusha watu kuongopea, watoe na kaishu fulani hivi ambacho kinaambatanisha na kuwa mwenyeji wa mazingira hayo. Ni wazo tu!!

Sasa tupo ambao tulikuwa "maripita" ila kwa wale waliofanikiwa kusoma kabarimu-bunda,bulinga-musoma,mabibo-dar,mukigo-manyovu,mukongoro-kigoma na mahembe kigona hebu tupeane nyepesi nyepesi za enzi hizo.

Tukimaliza hapo hebu tutafutane wale tuliosoma shule za mchepuo wa kilimo hasa kwa Mwasamila ili tuone tutakumbuka nini enzi hizo.ni ka hoja tu haka.
 
LY mnalikumbuka pia neno hili.hapo ndio mmeshaingia std seven
...Katibu tarafa LY ndio ilikuwa noma nakumbuka nilipoingia darasa la 7 nilikuwa nafuga nywele ndefu ili uonekane na wewe gangwe mwalimu mmoja kwenye ukaguzi asubuhi alikuja na mkasi akampitia kila mwenye nywele ndefu anachofanya anakuanzishia kunyoa kwa style ya msalaba katikati ya kichwa ili ukirudi kwenu ukamalizie. Si unajua enzi zile ukiwa na nywele ndefu unaweza kutengeneza matuta!!!....LY nayo ilikuwa na raha yake...
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom