Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Marehemu Mbaraka Mwinshehe, na Mpiga Ngoma RIP Morris Nyunyusa, hawa walikuwa ndio wawakilishi wakubwa wa taifa letu, kwenye maonyesho mbali mbali ya sanaa ya kimataifa na walilitangaza sana jina la taifa letu huko, hasa mwaka 1970 walipokwenda kutuwakilisha kwenye maonyesho ya Expo Japan.
Nakumbuka wimbo aliotunga waliporudi toka Japan. Kila ninapokwenda Japan tunapoelekea kutua Narita airport huwa nauimba sana wimbo huu kimoyomoyo;
Sasa tunatoa shukurani
Kwa serikali yetu ya Tanzania
Kutupatia nafasi
Ya kwenda mpaka Japan...
Chorus
Maonyesho Japan yalifana sana
Mataifa yote yalifurahi sana
Banda la Tanzania limetia fora, oyeee
Maonyesho Japan yalifana sana
Likembe Mahoka na ngoma za Taifa
Wacheza midimu na wachezea nyoka
Mzee Morris na ngoma zake kumi, oyeee!
Maonyesho Japan yalifana sana
Bwana Mayagila na bendi ya polisi
Wana wa sanaa wa chuo kikuu Dar oyee!
Sayonara Osaka!
Sayonara Tokyo