Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

SUSI AND CHUMA
chuma___susi.jpg
 
Son of Alaska, picha safi sana. Nikiziangalia napata picha ya vipi ukoloni unavyorudi TZ kwa kasi. Kuna akina Susi na Chuma wengi tu wamezagaa mawizarani na kwingineko serikalini right now!
 
Mkuu Icadon,

Heshima mbele bro, duh tuendelee kuweka vitu hapa maana so far tunakula elimu safi na ya bure, Ashante sana mkuu,

Mkuu Jasusi,

Please, acha kupoteza muda wako, maana ukiona bin-adam anapigana na picha zisizosema, basi utajua ni kwa nini tuna matatizo kwenye muungano! Sio kwamba hatujamuona na hiyo crying yake for attention, ila tumemdharau,

Najua kuwa unazo picha nyingi za kumbu kumbu, please weka picha hapa achana na kelele za mlango!

Mkuu Invisible,

Ahsante kwa marekebisho naomba uipitie hii topic mara kwa mara kurekebisha picha na maneno yasiyokuwa sawia kuambatana na hizi picha, za viongozi wetu mashuhuri waliotuwekea msingi wa taifa hili, ambalo some of us we are proud citizens wake.

Mkuu Bubu,

Heshima mbele, fimbo ya Mwalimu ilikuwa fupi sio ndefu kama hii ya Malecela,

enzi hizo ilikuwa ni fashion na politically correct kwa kila mwanamapinduzi kiongozi wa Afrika, kushika Fimbo ikiwa ni alama ya kumuiga Nabii Musa na ile Fimbo aliyokuwa akiitumia kuchungia Kondoo, ambayo baadaye Mungu alimuelekeza kuitumia kuwaokoa wana wa Israel kutoka utumwani Misri.

Viongozi wote wa Afrika enzi hizo walikuwa na Fimbo, kuanzia kina Sekou-Toure, Kawawa, Kambona, Mobuttu, Mwalimu, Nasser, Kayibanda, Karekou, Kenyatta, Malecela, Banda, Kaunda (ambaye baadaye alibadili na kuanza kushika kitambaa cheupe), Nkurmah, Tafawa Balewa, Lummumba, Micombero, Nimeiri, Siad Barre, Bongo, Sengor, Ngwabi, hawa wote ni viongozi waliokuwa na hiyo tabia ya kushika Fimbo.

Ahsante Mkuu!

Mkuu Jasusi,

Hakuna wasi wasi mkuu, zipo picha nyingi sana zinakuja hapa, zote zitawekwa hapa, wakuu wengine leteni picha jamani pia natoa hongera za dhati kwa wakuu Kichuguu na hasa mkulu wangu Icadon, mkuu ubarikiwe tu maana naona picha safi sana hizi na ni ukumbosho mzuri sana kwa sisi wananchi,

Unajua inafika mahali as a nation mnakuwa hamuelewi mnakokwenda, kama sasa hivi tulivyo kwenye taifa letu, sio vibaya tukijikumbusha tulikotoka,

hotuba ya juzi ya Rais, binafsi imenihakikishia one thing kwamba sasa hivi we are not effective tena kama tulivyokuwa zamani, kumbuka huko nyuma hotuba zake zote muhimu kwa taifa alikuwa ni lazima alalmikie mtandao huu, kwa maneno ya ujanja ujanja ya ku-generelize ".......mambo yanayofanyika kwenye mitandao...." Hii ni mara ya kwanza ametuacha nje, ina maana hatuwakoseshi usingizi tena sasa hivi, sasa ni vyema kujaribu kutafuta mbinu mpya za kupigana ndani ya forum,

Hatutashindwa, tutashinda tu lakini sometimes ni vyema kukubali ukweli na kujiangalia na kujipanga upya!

FMES,
Kenyatta hakuwa na fimbo peke yake. Alikuwa pia na ule mkia wa ng'ombe uliosukwa kwenye fimbo. Wenyewe wanaita whisk. Ningekuwa na hiyo picha nigeiweka hapa.

Nadhani kiboko zaidi ni pale Nyerere alipokula chati na hasidi wake mkuu Amin

i1372_Amininyerere.jpg
Wakuu zangu Kichuguu na Jasusi ,
Huyu jamaa Le Mutuz enzi hizo alikuwa sawa na Lucifer kabla hajatimuliwa na kulaaniwa kutoka mbinguni, yaani wakati hajawa IBILISI, ndo alikuwa anaweza andika kwa utii. Siku hizi ni aibu tupu..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom