Picha ya Ali Msham na Iddi Faiz Mafungo ndani ya kumbukuzi ya nyumba ya Baba wa Taifa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,924
30,272
PICHA YA ALI MSHAM NA IDDI FAIZ MAFUNGO NDANI YA NYUMBA YA KUMBUKIZI YA BABA WA TAIFA

Jana nimeeleza kazi ya Jaffar Mponda katika kutayarisha kipindi cha Nyerere Day.

Jaffar Mponda alikuwa keshamaliza kazi kubwa katika kupita kote alikopita Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika zaidi ya miaka 70 sasa akinihoji huku tumezungukwa na watu mitaani ambao walikuwa kama wasikilkizaji ndani ya studio iliyokuwa nje.

Tulianza na nyumba Abdul Sykes aliyoishi Mwalimu Mtaa wa Stanley na Sikukuu kisha tukaja Mtaa wa Kipata na Sikukuu ilipokuwa nyumba ya Clement Mtamila Mwenyekiti wa TANU, tukaenda nyumbani kwa Bi. Mruguru bint Mussa, Ukumbi wa Arnautoglu nyumba ya Bi. Mwamtoro bint Chuma.

Jaffar alikuwa heshi kunihurumia na kunipa pole kwa jua kali lililokuwa linawaka nami sikuchoka kumkumbusha kila mahali tuliposimama mimi nikimweleza kuwa hali hiyo anayoiona leo haikuwapo hata katika fikra za sisi tuliolelewa mitaa hiyo.

Hakuna aliyepata kuwaza hata kwa mbali sana kuwa Gerezani kutajengwa majumba ya gorofa mazuri ya kuishi watu na mahoteli ya kupendeza yenye lifti na viyoyozi na ndani kutakuwa na migahawa kama ile iliyokuwapo Uzunguni sehemu za Acacia Avenue sasa Samora Avenue.

Tulipomaliza mahojinao yetu nje ya nyumba ya Bi. Mwamtoro bint Chuma nyumba ambayo iko nyuma ya Ofisi Ndogo ya CCM tukaelekea Magomeni Mtaa wa Ifunda kwenye nyumba aliyojenga Mwalimu mwaka wa 1958 na akaishi pale kwa kipindi kifupi akahamia Sea View nyumba ya serikali.

Mwalimu alikuwa sasa anangojea kuongoza serikali ya madaraka mwaka wa 1960 kisha uhuru kamili na kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika.

Hivi sasa nyumba hii ya Magomeni imegeuzwa kuwa kumbukizi ya Mwalimu Nyerere.

Historia yake imehifadhiwa katika nyumba hii pakiwa na picha zake na vitu alivyotumia wakati akiishi hapo.

Tulipokelewa vyema sana na wafanyakazi wote wa nyumba hiyo wakubwa kwa wadogo khasa kwa kuwa Jaffar na amesaidia sana kupitia AZAM TV kuitangaza nyumba hii ya Baba wa Taifa kwa umma.

''Mzee Mohamed nakuomba tufunge kipindi hiki kwa wewe kueleza machache katika katika picha hizi za Baba wa Taifa ziliopo hapa,'' Jaffar aliniambia.

Wakuu wa nyumba hii walikuwa wametuzunguka kusikiliza nikamsikia mmoja anasema nyuma ya mgongo wangu kuwa mimi ninajua mengi sana katika historia ya Mwalimu Nyerere.

Nilicheka kimoyomoyo.
Najua kwa nini alisema hivyo.

Sababu ni kuwa walipokuwa wanatafuta picha za Mwalimu Nyerere niliwapatia picha nyingi na baadhi zipo hapo wamezitundika ukutani kwa kila ajae pale kuziona.

Niliwapatia picha nyingi kutoka Maktaba ya Picha ya Ukoo wa Sykes.

''Naomba nizieleze picha tatu na sabubu ni kuwa mimi ndiyo nilihusika kuziweka hadharani kwa watu wote kuziona na kuzifahamu.''

Hapa nilisimama na kuomba radhi nisieleweke kuwa najipigia zumari langu mwenyewe.

''Picha hizi wamenipa watu mimi nimezifikisha hapa nyumbani kwa Baba wa Taifa ili ziwakumbushe wataokuja hapa historia ya Mwalimu Nyerere na historia ya wale ambao walikuwa na yeye katika siku zile ngumu za kupigania uhuru lakini kwa bahati mbaya wamesahaulika.''

Jicho langu likaenda kwenye picha Ali Msham akiwa na Mwalimu Nyerere, John Rupia, Zuberi Mtemvu na vijana wa Bantu Group, picha iliyopigwa nyumbani kwa Ali Msham Magomeni, Mtaa wa Jaribu mwaka wa 1955.

Nikamweleza Ali Msham alikuwa nani kwa TANU, Mwalimu Nyerere na Mama Maria.

Picha hii wamenipa watoto wa Ali Msham na ni kati ya picha 11 walizoniokabidhi nizitumie nipendavyo kwa manufaa ya umma.

Nikaisogelea picha nyingine ya mwaka huo huo 1955 safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO picha iliyopigwa uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.

Wamesimama watu wengi kwenye picha hii pembeni ya Mwalimu alikuwa Iddi Faiz Mafungo na nikamweleza nani alikuwa Iddi Faiz Mafungo.

''Huyu alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na Mweka Hazina wa TANU kadi yake ya TANU ni No. 24 na No. 25 ni ya ndigi yake Iddi Tosiri na yeye ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya Mwalimu Nyerere UNO.

Iddi Faiz na Iddi Tosiri ndiyo walimtambilisha Nyerere kwa Sheikh Mohamed Ramiyya Bagamoyo''

Picha hii niliipata kwa Jim Bailey, Mzungu kutoka Afrika ya Kusini aliyekuwa mmiliki wa gazeti la Drum.

Kuna baadhi ya wafanyakazi wa Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere ndiyo kwa mara ya kwanza wanaisikia historia ya Iddi Faiz Mafungo.

Nikahitimisha kwa kueleza picha maarufu ya Mwalimu Nyerere akiwa na Baraza la Wazee wa TANU.

Kidole changu kikaenda kwa Said Chamwenyewe nikawaeleza wasikilizaji wangu kuwa Mzee Said Chamwenyewe ndiye aliyeipatia wanachama wake wa kwanza TANU kutoka Rufiji.

Nikamaliza kwa kueleza kuwa picha hiyo nilipewa na Msakala Tambaza, mjukuu wa Mzee Mohamed Tambaza.

Historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Kambarage Nyerere inapendeza pale inapoelezwa na historiza za wazalendo wengine waliopigania uhuru na Mwalimu bega kwa bega.

PICHA

Ali Msham waliosimama wapili.

Hapo ni nyumbani kwake Magomeni yupo na Bantu Group.

Waliokaa kulia Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia.

Kuliani kwa Nyerere kavaa kanzu koti na tarbush ni Iddi Faiz Mafungo.

Baraza la Wazee wa TANU.

Jaffar Mponda akiwa na watendaji wa Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere.

1665632297260.png
1665632328924.png
1665632375478.png
1665632418461.png
 
Ahsante sana Mzee wangu kwa muendelezo huu wa historia iliyotukuka ya nchi yetu, shukran laka.
 
Tulipomaliza mahojinao yetu nje ya nyumba ya Bi. Mwamtoro bint Chuma nyumba ambayo iko nyuma ya Ofisi Ndogo ya CCM tukaelekea Magomeni Mtaa wa Ifunda kwenye nyumba aliyojenga Mwalimu mwaka wa 1958 na akaishi pale kwa kipindi kifupi akahamia Sea View nyumba ya serikali.

View attachment 2385422View attachment 2385425View attachment 2385428View attachment 2385431
TANU ilikuwa inamlipa mshahara Nyerere?

Najaribu kuwaza aliwezaje kujenga hiyo nyumba wakati alishaacha kazi yake ya kufundisha Pugu.
 
TANU ilikuwa inamlipa mshahara Nyerere?

Najaribu kuwaza aliwezaje kujenga hiyo nyumba wakati alishaacha kazi yake ya kufundisha Pugu.
Gagnija,
Ilikarabatiwa nyumba ya Mwalimu Nyerere palifanyika uzinduzi na mimi nilikuwapo.

Madaraka Nyerere alizungumza kuhusu nyumba ile.

Madaraka Nyerere alieza ujenzi wa nyumba ile kuwa kiwanja alinunua Mwalimu kwa fedha zake mwenyewe na nyumba ile ikajengwa kwa msaada wa marafiki zake wakiwemo akina Sykes na Mzee Rupia.

Mwalimu akilipwa mshahara na TANU na kwa hakika Mwalimu alikuwa maslahi bora akiwa mwajiriwa wa TANU kupita yake aliyokuwa analipwa katika kazi ya ualimu.
 
Back
Top Bottom