Tatizo la ukosefu wa ajira, makosa ni ya Serikali, Jamii au mtu mwenyewe?

OnTheEarth

Member
Jan 1, 2023
75
63
Katika jamii na taifa kwa ujumla kuna tatizo kubwa la ukosefu wa ajira. Watu wengi: waliohitimu mafunzo na wenye taaluma pamoja na wasio wahitimu pia wasio na mafunzo, hawana kazi za kufanya.

Kwa vyovyote vile, hali hii si nzuri kwa ustawi wa mtu mmoja mmoja, jamii au taifa. Suala la kazi au ajira si tu kwa ajili ya uchumi au fedha, lakini kwa ajili ya afya, uhai, uhusiano na utu.

Ndio kwa maneno mengine, kusema kwamba ukosefu wa ajira au kazi hudhoofisha na pole pole uharibu hali ya utu na mwisho uhai.

Ukosefu wa ajira au kazi si tatizo lililokuja kwa bahati mbaya isipokuwa kwa makosa dhahiri yanayofanywa na taasisi na mamlaka za Ndoa, Jamii, Serikali na Kanisa.

Taasisi ya ndoa; msingi wa familia, ambayo ndio kilele cha jamii ina wajibu wa kipekee na mzito kuhakikisha kwamba, kila uhai unaokuja duniani umewekewa mazingira yote yanayotakiwa kiakili na kimwili kwa ajili ya uhai.

Kwa kuona kwangu mambo pia uelewa wangu wa mambo na elimu ya vitu, matatizo mengi tuliyonayo ikiwa ni pamoja na haya ya ukosefu wa ajira na kazi yana chanzo chao katika ndoa.

Angalia ndoa zetu jinsi zilivyo. Tazama kwa kwa mfano, masuala ya uzazi yalivyo kwenye jamii zetu. Ni nani anajali kuhusu uhai anaouleta duniani? Watu wanazaa hovyohovyo: walio na ndoa wanazaa nje ya ndoa na wasio na ndoa wamezalisha walio na ndoa na pia wasio na ndoa! Ni wanawake wangapi wamezalishwa na wakaachwa? Na je, vipi kuhusu huo uhai? Vipi kuhusu malezi ya hao watoto wanaozaliwa? Na matunzo je?

Suala la ukosefu wa ajira na kazi haliwezi kuangaliwa kwa upande mmoja tu ikiwa tunataka kujua chanzo chake isipokuwa kama kitu kizima. Kama ulivyo ukweli hauwezi kupatikana kwa kuangalia upende mmoja bali kitu kizima.

Kazi kubwa ya Serikali popote ni "Ulinzi". Ulinzi ndio kazi ya Serikali. Sasa swali, Serikali inatekeleza wajibu wake? Inawezekanaje Serikali iruhusu mambo ambayo yakifanyika yanahatarisha uhai?

Ulinzi si tu mambo ya kisiasa na madaraka, lakini mambo yote yahusuyo ustawi wa jamii. Mambo yote yanayotishia kuharibu uhai; kwa namna yanavyofanyika kama yanakwenda kinyume na mpango wa uumbaji, Serikali inawajibu wa kuyaondoa bila kujali ghalama yake.

Kama mtu kwa kujua au kutojua anatishia mpango wa uumbaji, Serikali inatakiwa kuingilia kati. Sasa angalia hali ya uzazi mathalani hapa kwetu Afrika je, hali hiyo haihatarishi uhai?

Ikiwa tunataka kujua tatizo la ukosefu wa ajira na kazi, hakuna mahali pengine popote tunaweza kujua isipokuwa kwenye ndoa. Hapa ndipo chanzo cha matatizo mengi tunayoshuhudia leo.

Wewe mke au wewe mume unawezaje kuleta uhai mpya duniani wakati huo huo hujui huo uhai mpya unaouleta utafanya kazi gani pindi huyo mtoto atakapo anza kujitegemea kimwili na kiakili?

Pengine hili ni jambo kubwa zaidi!

Fikiri kwa mfano, mume na mke wanazaa watoto wakati hawana uwezo wa kuwatunza kimwili ( yaani kuwapatia mahitaji haya: chakula, mavazi, malazi, matibabu, mawasiliano na usafiri) na kiakili ( elimu na mafundisho Mungu).

Kama wazazi hawa wanashindwa kutekeleza wajibu wao wa lazima kwa watoto, inawezekanaje mtoto huyu aliyekosa mahitaji muhimu, akakabilina na mazingira yake?

Au fikiri hivi: ni wanawake wangapi wamezalishwa au wanazalishwa watoto; na watoto hao licha ya kukosa mahitaji muhimu kwa ajili ya maendeleo ya mwili, wanakosa pia malezi ya mzazi mmoja: Je, hawa wanaweza kufikiri vizuri na kuyaona mambo kwa mwanga bora achilia mbali ajira au kazi?

Tatizo la ukosefu wa ajira au kazi halipaswi hata kidogo kuwa jukumu la kisiasa au Serikali. Hili ni wajibu wa kila mtu, kila awae na aitwaye mtu hawezi kukwepa ukweli huu.

Wewe mume, nawe mke unayetaka kufuata wito wa ndoa nawe ambaye tayari uko kwenye ndoa, unaposema unataka kuleta uhai mwingine (kuwa na mtoto) ni, wajibu wako kujua kwa hakika kabisa, kwamba huyu mtoto nitakaye mleta duniani atafanya kazi hii kwa kuwa tayari ipo, na kwa kuwa kila kitu kinachokubalika na kutakiwa kwa ajili yake kipo tayari.

Ukiacha familia, angalia jamii yetu. Wewe hapo ulipo unatoka kwenye familia na uko kwenye jamii, unaona nini kwenye jamii? Je, jamii inatekeleza wajibu wake?

Au labda unaweza kujiuliza hivi: Jamii ni nani?

Kila kitu kilivyo leo; iwe ni chema au kiovu ni kushindwa au kufanya vema kwa mamlaka za Familia, Jamii, Serikali na Kanisa.

Kanisa ndilo linajua wapi mtu anatoka na wapi anaenda. Kwa hiyo mambo yote yahusuyo uhai, ambayo ni pamoja na ajira na kazi ni pia Kanisa. Kwa sababu Kanisa si tu linashugulikia Roho, lakini pia linashugulikia mwili.

Tunajua Roho ni bora na ya thamani zaidi kuliko mwili, lakini pia hatuwezi kupuuza mwili kwa kuwa Mungu aliyeumba Roho ndiye pia aliyeumba na mwili.

Duniani tunamoishi ni makazi pa kila mtu na kila mmoja wetu popote. Maeneo ya kijiografia na kiutawala hayawafungi watu kwenda kuishi mahali popote kwa sababu dunia ndio makazi yetu kwa sasa.

Kwa hiyo kufikiri kwamba tuna eneo kubwa lisilokaliwa na watu na kwa sababu hiyo tunaweza kuleta uhai mwingine pasipo kufuata utaratibu ni, makosa makubwa na uharibifu mbaya.

Mungu hakufanya dunia ili iwe makazi ya watu pekee, bali kwa ajili ya kuendeleza mpango wake wa uumbaji.

Suala la ukosefu wa kazi na ajira ni matokeo ya matumizi mabaya ya akili na mwili. Mwili ni muhimu katika kutekeleza kazi za akili lakini mtu amekuwa akitumia vibaya akili yake.
 
Mada nzuri ,hoja makini. Habari mbaya iliyopo ni kwamba wanajamii forum wanapenda ngono kuliko uhai au afya ama mada kama hizi...
RIP graduetas
 
Kesi ya ajira ni kes ya fursa. fursa haziwrez kuwa nyingi kama population ni kubwa kupita capacity. tukifanikiwa kupanga uzazi waafrika matatizo mengi yatapungua au kwisha kabisa.
 
Tatizo la ajira katengeneza magufuli usipepese macho yeye ndiye aliyeamasisha watanzania wazaliane kama panya yeye atawasomesha bure watz wakaingia mkenge bila kutafakali baada ya kusomeshwa bure je nini kifuatacho? Na kingine kosa kubwa alilofanya kubania ajira kwa miaka kadhaa Kumetengeneza wimbi kubwa La graduate ambalo itachukua mdaha mrefu Kupambana nalo
 
kivip kaka. hoja yako ina ukakasi

..Ccm wanatekeleza vipaumbele vyao na si vipaumbele vya taifa.

..wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere Raisi wa Benki ya Dunia alikuja kutembelea Tanzania.

..serikali ikamtembeza chuo kikuu na kumwambia wanajivunia Kitivo cha SHERIA kuwa muanzilishi wa chuo kikuu hapa Tz.

..Raisi wa Benki ya Dunia anaitwa Robert McNamara alishangaa na kuhoji; kama tunaamini KILIMO ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu kwani hatukuonyesha mfano kwa kitivo cha Kilimo kuwa muanzilishi wa chuo chetu kikuu?

..huo ni mfano mmoja wapo kukazia hoja yangu. Ninayo mifano mingi zaidi.

..Ccm kutekeleza vipaumbele vyao, na si vipaumbele vya taifa, ndio sababu ya kudumaa kwa maendeleo ya Watanzania.
 
Tatizo la ajira katengeneza magufuli usipepese macho yeye ndiye aliyeamasisha watanzania wazaliane kama panya yeye atawasomesha bure watz wakaingia mkenge bila kutafakali baada ya kusomeshwa bure je nini kifuatacho? Na kingine kosa kubwa alilofanya kubania ajira kwa miaka kadhaa Kumetengeneza wimbi kubwa La graduate ambalo itachukua mdaha mrefu Kupambana nalo
wanaosoma kwa magufuli si hata chuo hawajafika? . wewe ni political affiliated
 
Nadhanj ni jamii na serikali yake, japo kila mmoja kwa nafasi yake (wasio na ajira) basi atakua na majibu ni kwanini iko hivyo.

Serikali pia sio wezeshi kabisa kwa vijana, walio kwenye vitengo kama tra, halmashauri, polisi wanawakaba koo sana vijana wanaojiajiri. Kila mtu ni boss kwenye kitengo chake, lakini kumbuka mjasiliamali yeye hana mtumwa wake kila mwenye cheo kwake ni boss wake.
Tra wamkimbize, halmashauri imburute wakija wakaguzi wa nini na nini wamtaftie makosa ili wampige kichache.

Matokeo yake ujanja ujanja mwingi ndo unafanya uishi mtaani, ukitaka kufata haki unaangukia pua.
Graduates wengi wanaingia kitaa kwa kujua kuna haki bin haki, hiki kitu sasa ndo kinaongeza idadi kubwa ya jobless mtaani, kwasababu mitaji walioyotoka nayo chuo kwa kujibana inakata mapema sana.
 
Ukosefu wa ajira unachangiwa na vijana wengi kutotaka kujishughurisha wanatarajia ajira kutoka serikalini kitu ambacho hakiwezekani maana Serikali haiwezii kuajiri watanzania wote kwaiyo kijana anapaswa kuchukua mkopo kutoka halmashauri akajiari hasa kipindi hiki cha uongozi wa Rais Samia Suluhu ameweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri
 
Back
Top Bottom