Obhusegwe
JF-Expert Member
- Dec 28, 2008
- 231
- 28
Kama bado upo Dar na nakumbuka tuliwahi kukutana then tunaweza kuwasiliana via email nami nikakuunganisha na mtu wa ndani Zantel akakupa device flani hivi ukaunganisha kwenye Router yako ili kuweza kuunganisha pc zaidi ya 1 (hata 12 inafanya kazi).
Aidha, hapa kwangu nina Wireless na nimejaribu 30m from home bado inakuwa detected. Device ni nzuri na inafanya kazi, wao hawajaitangaza nami walinipa ili niijaribu na kuwapa feedback. Inafanya kazi vizuri sana. Hutakuwa na haja ya kufunga nyaya kibao kwenye cafe yako, sanasana ni kufanya wireless connection ofisini kwako na ndani ya 3hrs service inakuwa ishaanza.
Gharama wameshusha... I have to contact them ili nikwambie bei ikoje kwa 20GB, that's my package na haifiki hata Tshs 450,000/=
Uzuri wa device ile ni kuwa hata hizi modem za VodaCom na SimbaNet inafanya kazi nazo...
Ahsante mkuu
Ahsante sana mkuu,
Nitakutafuta nikikamilisha mipango yote na kuconfirm sehemu nitakapoweka hiyo project. Niko mkoani kwa sasa nadhani by september nitakuwa nimerudi dar permanently.