Mdani
Member
- Sep 17, 2011
- 28
- 44
Wadau wa JF, kabla ya yote nikili jf kuwa chuo kwangu kwani napata madini mengi kupitia komenti za wanajf.
Leo nimeonelea nije na mada chokozi; ni kwa nini mtandao wa fiber internet na air fiber umekuwa mgumu kusambazwa mikoani na maeneo ya vijijini.
Kampuni nyingi zinajielekeza kutoa huduma maeneo ya mjini tu (city center na 5G zone).
-Kwa nini hali iko hivyo?
-Changamoto ni zepi haya makampuni yanakabiliwa nazo kusambaza fiber?
-Je mtoa huduma mkuu ni mmoja kiasi kwamba kila 2nd ISP lazima achukue kwenye miundombinu hiyo hiyo?
-Je mkongo wa taifa uliosambazwa wakati wa Rais J.K Kikwete nchi nzima hauhusiani na hii intaneti ya fiber?
-Je utaalamu wa usambazaji wa fiber upoje? Kuna kitu cha kuzingatiwa kwa ma-isp?
-Je mimi kama mjasiriamali mdogo nawezaje kuwa ISP hata eneo dogo hapa wilayani?
-Je upande wa sera za nchi umekaeje mpaka hatupati ma-isp wadogo wadogo?
Kama mdau wa JF una utaalamu gani au mawazo gani kuhusu hizo hoja hapo juu?
Ila binafsi naweza kukiri kwamba hata viongozi wetu wa kisiasa hawana utashi kushinikiza digital life katika maisha yetu ya kila siku. Wenyewe macho yao yako kwenye maji, barabara na umeme.
Wenzetu wakenya wako mbali sana kwenye masuala ya intaneti na teknolojia ya habari. Makala nyingi nikitafuta mtandaoni ni za wakenya, Malaysia, Indonesia, Pakistan na nchi za hivyo.
Ila sio kwa Tanzania hawapo, wapo ila ni kama waganga wa kienyeji kujificha na ujuzi.
Nashukuru JF nimeweza kupata wataalam hapa na pale wa kibongo wanaoyajua na kuyaishi maisha ya dijitali; internet, electronics, connectivity na mambo kama hayo
Ahsanteni, karibuni kwa ujuzi
Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app