Tafsiri na uchambuzi wa matokeo ya udiwani

Mods mnamapenzi sana uzi wangu mmeunganisha na uzi mwingine mnataka wote tusifie Chadema, haya Chadema Oyee wamefanya vizuri.

Kuna haja gani ya kuwa na threads kibao zinazoongelea jambo moja?? twende tutiririke hapa, ccm mmeingiza negative kwenye idadi ya kata mlizokuwa mnaongoza na bado mnajisifia, kweli!??, inaonyesha mlikata tamaa mapema na ndio maana ya vurugu zile, shahada feki zile, vipigo kwa wananchi vile, rushwa ile na ubwabwa ule,!!? you are doomed ccm!
 
kwa maana hii 2015 mkimaintain majimbo mliyonayo na kuongeza japo moja mtakuwa mna chakupongezwa?,hakika matumaini yetu yanazidi kufifia,mtu kama kitila anatoa ***** wa namna hii
 
Namna nyingine ya kuangalia ni kuwa labda ujumbe wa CDM bado haujaeleweka sana, haujakubalika, au haujafikika vizuri kwa wananchi.

Kama watu wangekuwa wanapima hamasa, na mikutano ya watu na jinsi ambavyo CDM jina lake limekuwa saturated kwenye jamii ya Watanzania ni wazi kuwa matokeo haya yalitakiwa yawe CCM viti 5 na CDM viti hivyo vingine. Matokeo haya yanaakisi yale ya Uchaguzi Mkuu ambapo pamoja na mengi sana CDM haikuweza hata kushinda viti 50 vya ubunge licha ya jina lake kutangaa sana mwaka 2010.

Jambo ambalo ni la hatari (kwa chama cha siasa) ni kuangalia "nje" yake kama sababu ya kutofanya vizuri zaidi. Kama CCM ikiwa dhaifu namna hii bado inaweza kushinda, itakuwaje ikija kupata nguvu?

nami naongezea. nilihusika kusimamia uchaguzi wa 2010. Nilichokishuhudia, ni kwamba, vijana wengi hawakuona majina yao. asilimia kubwa ya walioona majina yao, ni wale wakongwe lakini vijana wengi aidha majina yao yalikuwa yamekosewa au yana utata na alikojiandikishia au hawapo kabisa kwenye daftari la mpiga kura.

Uchaguzi huu uliofanyika, ni miaka miwili tangu uchaguzi mkuu uliokuwa na mizengwe mingi. bado majina ya wale ambao hawakupata fursa ya kupiga kura 2012. Lakini pia kuna idadi kubwa ambao hawakujiandikisha kwenye maandalizi ya uchaguzi wa 2010, na wengine wengi ambao wana shauku ya kujiandikisha lakini bado tume ya uchaguzi bado hawajatangaza kutaka kuwatambua vijana hao ambao ndo wanao pamba mikutano ya chadema kwa kiasi kikubwa.

Ninashauri sasa, jitihada zifanywe kuilazimi9sha tume kupitia daftari lake kila mwaka, ili kuwaingiza vijana wapya waliotimiza umri wa kupiga kura, na sio wasubiri hadi uchaguzi mkuu.

Mfumo wa kulipitia daftari kila mwaka, kwanza litasaidia kurekebisha makosa ya majina yaliyokosewa, lakini pia itawahakikishia wapiga kura vituo halisi vinavyowatambua kwa upigaji wa kura.

Juhudi nyingine zifanywe na vyama vya upinzani kwa kuwaelimisha watu umhimu wa kujiandikisha, isije kuwa wanajaza watu lakini hawana shahada.
 
CDM wamepanda kwa 60% .. ?
Hapo kidoooogo hauko sawa, ungeyaacha hayo kwanza.
Labda uangalie Arumeru na Shinyanga kama ni viti mlivyopoteza unnecessarily na nawapa pongezi sana kwa kunyakua Mlangila .
Rombo na mvomero ..... yeeah but no.

Arumeru hatujapoteza!Hii kata ilikuwepo Arumeru Magharibi eneo ambalo CDM haikuwahi kuwa na nguvu huko nyuma.Eneo hili bado watu si waelewa sana hivyo ni rahisi bado kurubuniwa na tshrt,kofia na kanga tofauti na watu wa Arumeru mashariki kwa Nassari.
Huko Shinyanga bado sioni kama Chadema imepoteza
 
Hadi dakika hii matokeo yanaonyesha kwamba katika Kata 29, CHADEMA wameshinda katika kata 5 and TLP (1) na CCM kushinda katika kata zilizobaki.

Kwa muono wa karibu unaweza ukadhani kwamba CHADEMA wamepoteza sana katika uchaguzi huu. Hata hivyo ukiyachunguza matokeo haya kwa ukaribu utaona kwamba CHADEMA wamepata mafanikio makubwa na CCM wametelemka.

Tukumbuke kwamba CHADEMA walikuwa na kata mbili za kuzilinda katika uchaguzi huu ambazo ni Rombo na Mvomero. Kata hizi wamefanikiwa kuzilinda na kuongeza zingine tatu, ambazo ni Mlangila (Ludewa), Ipole na Daraja Mbili (zote hizi zilikuwa za CCM). Kwa hiyo wamelinda kata zao na kuzipokonya zingine tatu kutoka mikononi mwa CCM.

Na yote hii ni ndani ya miezi 24 tu tangu uchaguzi mkuu ufanyike. Kwa hiyo kimehesabu CCM wameshuka kwa 11.1% na CHADEMA wamepanda kwa 60%! So, CDM keep up the momentum!

Kitila,
kuna ulazima sana wa CDM kubadili mfumo wake wa siasa za level ya udiwani na hata serikali za mitaa la sivyo mtarudia makosa yale yale yanayovigharimu vyama vingi vya upinzani.
Lazima muanze leo kuimarisha ofisi zenu za mikoa na wilaya ili siasa ziwe karibu na wananchi kimazingira,aina ya maisha ya eneo husika na milio za siasa za eneo husika.Hakika mashambulizi yawe karibu na walengwa toka wilayani kwenda katani ni karibu kulinganisha na convoy inayotoka makao makuu na kujaza umati wa watu na siku wakiondoka wanaondoka na umati wao.Haitasaidia chochote zaidi ya baadae kuonekana kama ni sehemu ya posho kwa viongozi wa makao.
Fatilia kwa makini hotuba zilizotolewa na makamanda mbali mbali toka makao makuu walikuwa wana-address mambo ya kitaifa na wala sio yanayowagusa wakazi wa eneo huska mna over estimate mambo.Vijijini issue ya kupatikana kwa chumvi ni deal kwani ndo matatizo yao ya kila siku watu wanakula chakula bila chumvi,CCM daima huu ndo mtaji wao.
Kijijini hawana haja na KAGODA au MEREMETA,KUTEKWA KWA ULIMBOKA, MABILIONI YA USWIS,hizi ni siasa za level ya vyuo vikuu kama umealikwa katika mihadhara ya vyuo au kitaifa pale ndo mahali pake.
Mimi nimeishi vijijini na hata chaguzi nyingi zinanikuta huko,CDM inakosa BEAT ya vijijini na hata mwendelezo wake ni mdogo sana.
Shusheni mikakati ya chama kwa ngazi ya chini simikeni uongozi na uwezesheni kufanya kazi kueneza sera za chama kwani ni rahisi vijijini kumuamini mtu wanaeishi nae kuliko yule wa kuja na kuondoka,mara nyingi wanaambiwa hawa wataleta fujo na wananchi wanaamini kirahisi.

Badilisheni mfumo haraka sana na muufanyie kazi kabla ya chaguzi za serikali za mitaa.
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi, hii ni hatua moja kuu muhimu sana kisiasa!
 
Ndugu zangu sisi ambao tuko field kupambana na CCM tunajua sababu nyingi ambazo CCM inazitumia kushinda, kwanza wanatumia vyombo vya dola kama tume ya uchaguzi, kuna sababu gani tume kukataa kuandisha wapiga kura wapya kwa zaidi ya miaka minne sasa, new voters wengi ambao wanashabikia na wamehamasishwa na kupewa matumaini na CHADEMA hawaandikishwi! Mimi nilisimamia kituo chenye wapiga kura 380 lakini walio piga kura ni watu 88 tu, na kati hao niliipatia kura 56 CHADEMA na CCM 26 unaweza ukaona hii idadi ndogo ya watu wanao piga kura, lakini kulikuwa na malalamiko mengi ya watu waliopoteza vitambulisho walikuja wakifikiri wanaweza kuruhusiwa kupiga kura! Hiyo ni Sababu ya msingi sana, lakini vijana wengi ambao ndio wanaotaka mabadiliko hawajaandikishwa! Sababu nyingine CCM wanatumia rushwa kwa kiwango cha juu sana na kwenye jamii zenye elimu ndogo ya uraia CCM wanafanikiwa kushinda chaguzi kwa rushwa! Sijafurahishwa na matokeo haya ingewaje CHADEMA hatujapoteza kiti hata kimoja lakini margin yetu ilipaswa kuongezeka kwahiyo tujifunze na tuendelee kujiimarisha!
 
Kitila,
kuna ulazima sana wa CDM kubadili mfumo wake wa siasa za level ya udiwani na hata serikali za mitaa la sivyo mtarudia makosa yale yale yanayovigharimu vyama vingi vya upinzani.
Lazima muanze leo kuimarisha ofisi zenu za mikoa na wilaya ili siasa ziwe karibu na wananchi kimazingira,aina ya maisha ya eneo husika na milio za siasa za eneo husika.Hakika mashambulizi yawe karibu na walengwa toka wilayani kwenda katani ni karibu kulinganisha na convoy inayotoka makao makuu na kujaza umati wa watu na siku wakiondoka wanaondoka na umati wao.Haitasaidia chochote zaidi ya baadae kuonekana kama ni sehemu ya posho kwa viongozi wa makao.
Fatilia kwa makini hotuba zilizotolewa na makamanda mbali mbali toka makao makuu walikuwa wana-address mambo ya kitaifa na wala sio yanayowagusa wakazi wa eneo huska mna over estimate mambo.Vijijini issue ya kupatikana kwa chumvi ni deal kwani ndo matatizo yao ya kila siku watu wanakula chakula bila chumvi,CCM daima huu ndo mtaji wao.
Kijijini hawana haja na KAGODA au MEREMETA,KUTEKWA KWA ULIMBOKA, MABILIONI YA USWIS,hizi ni siasa za level ya vyuo vikuu kama umealikwa katika mihadhara ya vyuo au kitaifa pale ndo mahali pake.
Mimi nimeishi vijijini na hata chaguzi nyingi zinanikuta huko,CDM inakosa BEAT ya vijijini na hata mwendelezo wake ni mdogo sana.
Shusheni mikakati ya chama kwa ngazi ya chini simikeni uongozi na uwezesheni kufanya kazi kueneza sera za chama kwani ni rahisi vijijini kumuamini mtu wanaeishi nae kuliko yule wa kuja na kuondoka,mara nyingi wanaambiwa hawa wataleta fujo na wananchi wanaamini kirahisi.

Badilisheni mfumo haraka sana na muufanyie kazi kabla ya chaguzi za serikali za mitaa.

Ushauri mzuri sana, bila shaka utawafikia walengwa!
 
Nakipenda CHADEMA lakini binafsi sikuridhishwa sana na matokeo haya. Nimesikikitishwa sana kushindwa kupata ushindi katika baadhi ya kata kama:

1. Mpwapwa
2. Msalato
3. Mwawaza
4. Lwenzela
5. Kata iliyopo Arumeru Mashariki.

Hata hivyo, nyongeza ya kata 3 si haba. Kimtokacho mtu kimemtoka.

Ninaomba Sekeritariati ya CHADEMA ifanye uchambuzi yakinifu na iwajuze wanachama ni wapi kuna matatizo. Matatizo mengi yako katika Halmashauri zetu, hivyo CHADEMA hakina budi kujipanga kuchukua Halmashauri nyingi ifikapo 2015, hata zaidi ya kufikiria kuchukua serikali kuu. Inabidi kuanzia sasa, waanze kujitokeza wanachama wazuri wa kugombea udiwani, wakiwemo wasomi, ambao watasimamia halmashauri zetu vizuri, hasa kwa kuziba mianya ya upotevu wa fedha nyingi katika halmashauri za wilaya, miji na majiji.

HONGERENI WASHINDI. CHAPENI KAZI.
 
Kitila,
kuna ulazima sana wa CDM kubadili mfumo wake wa siasa za level ya udiwani na hata serikali za mitaa la sivyo mtarudia makosa yale yale yanayovigharimu vyama vingi vya upinzani.
Lazima muanze leo kuimarisha ofisi zenu za mikoa na wilaya ili siasa ziwe karibu na wananchi kimazingira,aina ya maisha ya eneo husika na milio za siasa za eneo husika.Hakika mashambulizi yawe karibu na walengwa toka wilayani kwenda katani ni karibu kulinganisha na convoy inayotoka makao makuu na kujaza umati wa watu na siku wakiondoka wanaondoka na umati wao.Haitasaidia chochote zaidi ya baadae kuonekana kama ni sehemu ya posho kwa viongozi wa makao.
Fatilia kwa makini hotuba zilizotolewa na makamanda mbali mbali toka makao makuu walikuwa wana-address mambo ya kitaifa na wala sio yanayowagusa wakazi wa eneo huska mna over estimate mambo.Vijijini issue ya kupatikana kwa chumvi ni deal kwani ndo matatizo yao ya kila siku watu wanakula chakula bila chumvi,CCM daima huu ndo mtaji wao.
Kijijini hawana haja na KAGODA au MEREMETA,KUTEKWA KWA ULIMBOKA, MABILIONI YA USWIS,hizi ni siasa za level ya vyuo vikuu kama umealikwa katika mihadhara ya vyuo au kitaifa pale ndo mahali pake.
Mimi nimeishi vijijini na hata chaguzi nyingi zinanikuta huko,CDM inakosa BEAT ya vijijini na hata mwendelezo wake ni mdogo sana.
Shusheni mikakati ya chama kwa ngazi ya chini simikeni uongozi na uwezesheni kufanya kazi kueneza sera za chama kwani ni rahisi vijijini kumuamini mtu wanaeishi nae kuliko yule wa kuja na kuondoka,mara nyingi wanaambiwa hawa wataleta fujo na wananchi wanaamini kirahisi.

Badilisheni mfumo haraka sana na muufanyie kazi kabla ya chaguzi za serikali za mitaa.
Ni kweli mkuu CDM bdo hawajaweza kuimarisha uongoz katika ngaz za chini huwa najiuliza kuna ugumu gani wa kuwa na redio na televishen ya CDM.Mabaraza ya CDM bdo sana hasa BAWACHA IMEKUFA ASILIMIA KUBWA YA WALIOICHAGUA CCM JANA NI AKINA MAMA NI LAZIMA KUWE NA UWAJIBIKAJ NDAN YA CHAMA HAIWEZEKAN WA2 WANAANGALIANA SURA WANACHEKEANA HUKU CHAMA KIKIKOSA HAMASA
 
Kuna factor nyingine muhimu pia ya kuzingatia. Wote waliopiga kura ni wale walioandikishwa yapata miaka mitatu iliyopita na tangu hapo orodha ya wapigakura haijawa updated. Kuna jeshi kubwa sana la vijana wa CDM ambao hawajaandikishwa kuwa wapigakura. I can assure you, 2014 will make the difference after the voters register is updated. CCM wanalijua sana hili.
 
Namna nyingine ya kuangalia ni kuwa labda ujumbe wa CDM bado haujaeleweka sana, haujakubalika, au haujafikika vizuri kwa wananchi.

Kama watu wangekuwa wanapima hamasa, na mikutano ya watu na jinsi ambavyo CDM jina lake limekuwa saturated kwenye jamii ya Watanzania ni wazi kuwa matokeo haya yalitakiwa yawe CCM viti 5 na CDM viti hivyo vingine. Matokeo haya yanaakisi yale ya Uchaguzi Mkuu ambapo pamoja na mengi sana CDM haikuweza hata kushinda viti 50 vya ubunge licha ya jina lake kutangaa sana mwaka 2010.

Jambo ambalo ni la hatari (kwa chama cha siasa) ni kuangalia "nje" yake kama sababu ya kutofanya vizuri zaidi. Kama CCM ikiwa dhaifu namna hii bado inaweza kushinda, itakuwaje ikija kupata nguvu?

Mkuu Mzee Mwanakijiji umeleta uchambuzi mzuri usio na biasness, hata kama kuna wanajamii forum wengine wanaokulaumu kwamba wewe ni CCM. tutakuwa hatukisaidii CDM kama tukiamua kukisifia tu hata pale ambapo kuna mapungufu ambayo yanabidi kufanyiwa kazi ili kiweze kuchukua uongozi wa nchi mwaka 2015.
 
Tume ya uchaguzi ilitakiwa kuandikisha watu ambao wanastaili kupiga kura ambao wametimiza mda wao mwaka huu ni wengi sana na waliopoteza shahada ni wengi ili hawakufanya na hawa wengi wao ni wapenda mabadiliko,so kwa upande wa chadema mi naona wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa yaani kulinda kata zao mbili na kuongeza kata 3,chamsingi ni kujitahidi kuangalia aina na uwezo wa wagombea wetu wa chadema wakati umefika tusimamishe vijana wenye elimu kama kati hata vyuo vikuu tuachane na darasa la saba na kidato cha nne(4),kwa jamii imebadilika sana ili ni swala la kudhingatia ukiangalia mtaani kuna vijana wengi wa vyuo vikuu ha diploma wapo na wanaweza tuwape nafasi ili kubadili na kuleta ushindani wa kutosha katika chaguzi zetu.
 
Hadi dakika hii matokeo yanaonyesha kwamba katika Kata 29, CHADEMA wameshinda katika kata 5 and TLP (1) na CCM kushinda katika kata zilizobaki.

Kwa muono wa karibu unaweza ukadhani kwamba CHADEMA wamepoteza sana katika uchaguzi huu. Hata hivyo ukiyachunguza matokeo haya kwa ukaribu utaona kwamba CHADEMA wamepata mafanikio makubwa na CCM wametelemka.

Tukumbuke kwamba CHADEMA walikuwa na kata mbili za kuzilinda katika uchaguzi huu ambazo ni Rombo na Mvomero. Kata hizi wamefanikiwa kuzilinda na kuongeza zingine tatu, ambazo ni Mlangila (Ludewa), Ipole na Daraja Mbili (zote hizi zilikuwa za CCM). Kwa hiyo wamelinda kata zao na kuzipokonya zingine tatu kutoka mikononi mwa CCM.

Na yote hii ni ndani ya miezi 24 tu tangu uchaguzi mkuu ufanyike. Kwa hiyo kimehesabu CCM wameshuka kwa 11.1% na CHADEMA wamepanda kwa 60%! So, CDM keep up the momentum!

Dr. Kitila, mbali na kukubaliana nawe kuwa CHADEMA kimeongeza idadi ya madiwani, bado ningetegemea uuseme na ukweli huu kuwa ushindi huu umekuwa chini ya mategemeo ya wengi, nikiwemo mimi. Inawezekana sekretariati ya CHADEMA haikuupa uzito unaostahili uchaguzi huu. Wakae chini wafanye tathmini ya kina na wajitahidi kurekebisha madhaifu yaliyosababisha kutoshinda vema mapema. Mimi ninathamini kuongoza halmashauri nyingi kuliko kuanza malumbano ya nani atakuwa rais mwaka 2015.
 
Namna nyingine ya kuangalia ni kuwa labda ujumbe wa CDM bado haujaeleweka sana, haujakubalika, au haujafikika vizuri kwa wananchi.

Kama watu wangekuwa wanapima hamasa, na mikutano ya watu na jinsi ambavyo CDM jina lake limekuwa saturated kwenye jamii ya Watanzania ni wazi kuwa matokeo haya yalitakiwa yawe CCM viti 5 na CDM viti hivyo vingine. Matokeo haya yanaakisi yale ya Uchaguzi Mkuu ambapo pamoja na mengi sana CDM haikuweza hata kushinda viti 50 vya ubunge licha ya jina lake kutangaa sana mwaka 2010.

Jambo ambalo ni la hatari (kwa chama cha siasa) ni kuangalia "nje" yake kama sababu ya kutofanya vizuri zaidi. Kama CCM ikiwa dhaifu namna hii bado inaweza kushinda, itakuwaje ikija kupata nguvu?

Kwenye medani ya siasa kama hata umepoteza kitongoji kimoja na mpinzani wako kanyakua kitongoji hicho basi yule aliyejiongezea kitongoji ndiye kashinda!

CHADEMA wameweza tetea viti vyao 2 vya udiwani na kujiongezea vingine 3 huu ni ushindi mkubwa mno kwa CHADEMA na madai kuwa walipaswa kuchukua viti vyote 27 vya CCM vilivyokuwa vinagombaniwa ni madai sio tu ya ajabu bali hayapo kwenye siasa za ushindani!

Kwa matokeo haya nyie wapenzi wa CHADEMA ingieni mitaani kushangilia ushindi wenu!CHADEMA wameongeza madiwani na CCM wamepoteza madiwani na itabaki hivyo kwenye kumbukumbu za vitabu vya Tume ya Uchaguzi(NEC)!

Ujumbe wa CHADEMA umeeleweka na wamewapa kata 3 zaidi!Ujumbe wao usiingeeleweka wangepoteza kata zao 2 walizoweza zitetea!
 
Kuna sehemu mbili za matokeo haya kwa mtazamo wangu.
1. CDM kuweza kuchukua kiti katika mkoa mtiifu wa Morogoro ni dalili njema
2. Matarajio ya ushindi hayakidhi kabisa jitihada za CDM kujieneza.

Kwa jinsi CCM ilivypopoteza umaarufu matokeo hayakupaswa kuwa kama inavyoonekana. Kupoteza asilimia 11 kwa CCM ni mafanikio kwasababu walitarajia kupoteza more than 50%.
Chadema kuongeza 60% ni suala la hesabu ambazo nadhani zina utata.

Ratio ya viti ni 5:27,tukifanya nadharia tu katika viti 270 huenda chadema wangepata 40 sijui kama 60% itapatikana.
Endapo CDM ingeshinda kwa asilimia 100, je hiyo ingeongeza viti hadi kufikia 10?

Nguvu inayotumika CDM na matokeo haviwiani kabisa. Kwa ''mvumo'' uliopo CDM hawapaswi kuona haya ni mafanikio.

Tatizo
Mikutano imetoa tija hasa huko vijijini? Tulionya na kusema hakuna sababu uongozi wa Dar uende kuimarisha chama kwa msaada wa viongozi wa mkoa. Viongozi wa mkoa na wilaya wanapaswa kuimarisha chama kwa msaada wa viongozi wa kitaifa.

Tumeuliza, hivi CDM walitafuta tatizo la upigaji kura mdogo baada ya chaguzi za Mbeya, Tarime na kwingineko?
CDM inaonekana kuridhika na jibu la tume ya uchaguzi kuwa hawajui sababu na sasa inawagharimu.

Daftari la wpiga kura:
Je CDM walishafanyia kazi au wanasubiri tume ya uchaguzi ambayo ni tawi la chama tawala lifanye kazi hiyo?

Udhaifu:
Licha ya matatizo hayo makubwa bado CDM wamejikita katika kutafuta wagombea wa Urais. Leo hii kama uchaguzi ungekuwa kitaifa hii ndiyo reflection halisi. Je, CDM wanatumaini la kupata ushindi wa kuchukua dola!

Ushauri
CDM waimarishe matawi hasa vijijini. Kazi hiyo ifanywe na wakuu wa mikoa na wilaya kichama. Anayeshindwa awajibike kabla ya kuangamiza chama zaidi.

CDM wajikite kutafuta vyanzo vya uandikishaji mdogo, kujitokeza kudogo katika kura, uharamia n.k
Watumie mikutano kuimarisha chama na si kukusanya watu.

Viongozi waelekeze nguvu zao kukabiliana na changamoto na waache kuanza tamaa za kuwagawa wanachama.
Dola haichukuliwi na mtu moja au umaarufu wa mtu mmoja.

CDM itafute mbinu za kuandikisha wapiga kura wao na kuwafuatilia wakati wa chaguzi.
CDM ijitahtmini upya na kujiuliza kama nguvu yake inakubalika na kama ni hivyo tatizo ni nini.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom