HOMOSAPIEN
JF-Expert Member
- Mar 31, 2011
- 745
- 271
Kuna Mr mmoja ameamua kubomoa UVCCM kwa mapesa yake kisa anataka kugombea urais 2015 kwa tiketi ya CCM, aelezwe mapema kuwa CDM ni moto wa kuotea mbali,chini ya katiba mpya asitegemee kuiba kura tena kama walivyozoea,kutakuwa na tume huru,sasa hayo mapesa ya ufisadi sijui atawahonga waTZ wote? anajaribu kupanga safu yake kuanzia sasa, na CDM mnatakiwa kuanza kuvunja nguvu zake za kifisadi kuanzia sasa kamwe nchi hii isinunuliwe na mtu kwa manufaa yake na ukoo wake.ishara au somo la kwanza iwe fundisho katika uchaguzi huu mdogo wa madiwani.