Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,568
Wananchi wa kata ya Kabwe jimbo la Nkasi Mashariki mkoani Rukwa wameandamana kukataa kuongozwa na upinzani baada ya diwani wa kata hiyo kufariki huku madai yao ni kuongozwa na upinzani kwa miaka 27 bila maendeleo katika eneo hilo.
Kata hiyo ni miongoni mwa kata ambazo tume ya taifa ya uchaguzi NEC imetangaza kurudiwa kwa uchaguzi baada ya diwani wake kufariki na sasa vyama vya siasa vimeanza kampeni kwa ajili ya kumpata diwani mpya atakayeziba nafasi iliyo wazi.
Akizungumza mbele ya wananchi hao mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM taifa @comrade_kawaida amesema ni wakati wa CCM kupewa nafasi katika kata hiyo ili walete maendeleo ambayo kwa muda mrefu yamekosekana katika eneo hilo.
Aidha amewataka vijana na wananchi wote kujitokeza siku ya uchaguzi kutimiza jukumu lao la kikatiba la kuchagua kiongozi atakayefaa katika kuleta maendeleo.