Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
Huyo slaa angeanza kutaja mafisadi waliyomo ndani ya chama chake! Hii kukimbilia kujitia anajua sana mambo ya CCM ni kutafuta ujiko usio na mshiko!
Slaa ana shughuli nyingi anashughulikia ya CDM na ya CCM next time kama una ombi kama hili mpelekee mapema aorodheshe kwenye list yake.
 
Ikiwa tunangoja ccm watimize ahadi yao ili sisi wananchi tuone nani fisadi, wavukazane ndani ya chama tutoke kwenye kucha ya mafisadi. dk slaa huyo kutochanganya.
Hana uvumilivu, subira hili linatufanya tuanze kuamini uwezo wake wa kuongozataifa kubwa tz likawa salama. kauli ya Msajili wa vyama vya siasa kuhusu dk slaa inaanza kuonekana
hekima ni kitu muhimu, subira ni muhimu pia.
bonge la juha, mijitu mingine bwana
 
Mchakamchaka wa kufa mtu! Yaani walipomaliza usanii wao wa kujivua gamba wakadhani wana ahueni lakini wapi Kamanda Mkuu anaendeleza drill!!! Bravo Chadema, Bravo Dr. Slaa.
 
Ninyi ni walewale mnaonufaika na ufisadi unaoendelea nchini. Kama kweli haunufaiki haingii akilini kuona mtu ambaye kajitoa kuwasaidia watu ili wajue jinsi gani inchi yao inavyo liwa eti ana papara. Huna la maana zaidi ya kujionesha kuwa wewe ni muumini wa ufisadi! Mwisho wenu umewadia....
 
nchi hii inatakiwa majeshi ya YESU yesu yaingilie kati kwakuwa yeye ndiye amirijeshi mkuu wa maamirijeshi wote. akiingilia migogolo yote na ufisadi wote hautakuwapo!

kwenye red panafaa zaidi kanisani ili usiamshe mijadala mingine.
 
Kama Dr. Slaa angekuwa mwehu kama hao CCM si Tz ingekuwa kama Ivory Coast. BTW navutiwa kujua ni kitu gani hasa unatumia (drink/inhale) kiasi cha kuwa bogus namna hii?
Na kama Kikwete si mvumilivu na mwenye hekima basi Tangu aingie madarakani Tanzania isingekuwepo,na dkt Slaa kwa matusi yake angekuwa Segerea.
 
Orodha ya Mwembe Yanga haikuambatana na credible actions. Naomba safari hii Dr. ukimaliza kuwataja uwaeleze waTz nini cha kuwafanya. Kama imechukua muda wa zaidi ya miaka 4 orodho ya awali kutofanyiwa kazi hata nusu, sasa lazima tupande viwango kidogo.

Napendekeza hatua za kisheria, nguvu ya umma (maandamano, migomo nk) viambatane na ushahidi wa watuhumiwa. Ben Ali wa Tunisia ana kesi muda huu, Mubarak nae ana la kujibu. Napendekeza kuwa na proactive- measures from the outset. Name and shame is not good enough now, done them.
 
nchi hii inatakiwa majeshi ya YESU yesu yaingilie kati kwakuwa yeye ndiye amirijeshi mkuu wa maamirijeshi wote. akiingilia migogolo yote na ufisadi wote hautakuwapo!
Mtajitahidi sana kubadilisha mada ila watu wanawashti vilevile.
 
Wote tunaochukia kuibiwa tusaidiane kuwataja mafisadi, isijekuwa chama cha upinzani kikawa kimbilio la wezi wa mali ya umma, anaejua fisadi, hata kama ni chadema, nccr, ccm au cuf na aseme, ila hawa wanaotajwa leo na Slaa, ni wale anaowajua yeye,

tunahitaji sana kuwajua wote
 
Ikiwa tunangoja ccm watimize ahadi yao ili sisi wananchi tuone nani fisadi, wavukazane ndani ya chama tutoke kwenye kucha ya mafisadi. dk slaa huyo kutochanganya.
Hana uvumilivu, subira hili linatufanya tuanze kuamini uwezo wake wa kuongozataifa kubwa tz likawa salama. kauli ya Msajili wa vyama vya siasa kuhusu dk slaa inaanza kuonekana
hekima ni kitu muhimu, subira ni muhimu pia.

Chuma huu haiundwi ikiwa imepoa ndia maana Dr Slaa hana mda wa kuwapa mafisadi wajipange kuhadaha wananchi kwani ktk taifa letu bila elimu ya uraia watu hawatapata fuksa ya kujua uozo wa taifa lao.

So kwa wewe mtoa mada nakufananisha na chupa mpya mvinyo wa zamani.
 
nchi hii inatakiwa majeshi ya YESU yesu yaingilie kati kwakuwa yeye ndiye amirijeshi mkuu wa maamirijeshi wote. akiingilia migogolo yote na ufisadi wote hautakuwapo!

huu ndio uzembe wa hali ya juu!umepewa macho ya kuona,masikio ya kusikia, mikono na miguu ya kuwawajibisha mafisadi halafu unasubiri yesu kwa sababu gani.acheni unafiki kuweni serious!msijidai kila kitu mungu yupo!
 
Dr Slaaa ni nyerere wa pili, ni kiongozi anaeona mbali huwezi kumfananisha na hao walafi wa ccm, tuna imani na dr slaa na tunaamini atatutoa shimoni.
 
Kwa kasi wanayo poromokanayo CCM baada ya miaka miwili ijayo umaarufu wake utakua kama kile chama cha yule MUTA MWEGA kama mnabisha subirini tu mtathibitisha.

Kitaa mambo imewagomea mbayaaaaaaaaaaa.
 
Kwa vile wizi siyo mpaka uwe wa ma-billioni,
Na kwa vile pia FISADI ni NYOKA hata kama anajivua gamba sumu yake bado ipo pale pale,
Dr Slaa usisahau kuongeza kwenye listi ya mafisadi hata wale wa halmashauri ya MUHEZA- TANGA waliotengeneza pikipiki ya Kichina kwa 2,000,000/= wakati bei yake ni laki 8 hadi 9 kununulia mpya !

 
Huyo slaa angeanza kutaja mafisadi waliyomo ndani ya chama chake! Hii kukimbilia kujitia anajua sana mambo ya CCM ni kutafuta ujiko usio na mshiko!

Ni lini CDM walikuwa custodians wa public resources?, ufisadi ni wizi wa mali ya umma, sasa kama CDM waliwahi kuwa waangalizi wa mali ya umma basi nao watajwe tu. CCM sasa hivi wanatumia masheikh wenye njaa kwa kuwapatia rushwa ya kununulia nyama na mchele na kuwataka wahakikishe CDM haikubaliki miongoni mwa waislam kwa kuihusisha na wanachokiita mfumo cristo. Huu ni uchochezi mmbaya sana, na inadhihirisha wazi kuwa CCM haihitaji umoja na utulivu uliopo kama tu vitaanya wao wasichaguliwe.

They divide us insteady of uniting us.
 
Nashukuru Dr. Slaa kwa kuitikia ombi langu kwa kasi ya ajabu maana ni juzi tu nilipendekeza kuwe na jitahada za maksudi kuifanyia update orodha hiyo kila mwaka na kwa mikoa tofauti ili kuwapigisha mchakamchaka mpaka kieleweke.
Hata hivyo pengine Dr. alikuwa na mpango huo tangu awali na hapo ndipo ninapoona umuhimu wa kuiunga mkono CDM kwa kuwa ni makini na wanafanya kweli.

Shime watanzania tuwaunge mkono na miguu wenzetu hawa kwa faida ya nchi yetu.

Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
wanaJF mlioko Tabora tuhabarisheni kinachoendelea katika mkutano wa kimapinduzi ulioko tabora,na "the second list of the shame"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom