Sina shaka kwamba ndege hiyo ilifuata taratibu za kuingia nchini, hivyo ilikuwa pale kihalali. Tatizo naloliona ni aliyetoa kibali hicho cha ndege kubwa ya kijeshi kama hiyo kuingia na kutua nchini alizingatia vigezo vipi? kwa kuwa alipaswa kutilia shaka maombi hayo na kuinyima kibali kama kweli anafanya kazi yake kwa kuzingatia sheria, utaratibu na common sense pia.Kwa kuwa mtoa kibali hakutumia common sense ana wajibu wa kutujibu watanzania kwa nini hakutumia common sense, na tuanzie hapo kuwakamata wahusika wote. Pili, wizara yetu ya mambo ya nje isikae kimya kama ilivyokaa kimya kuhusu suala hili, huu ni mgogoro wa kidiplomasia pia, hivyo lazima itoe kauli na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuhitaji twiga hao warudishwe nchini mara moja, na waarabu wote waliokodishwa viunga vya wanyama loliondo mikataba yao isitishwe mara moja na wote wafukuzwe nchini mara moja. Kama hatua zote hizi hazichukuliwi basi kwa kutumia common sense nitakuwa sina budi kuamini kwamba viongozi wajuu wa serikali ni wahusika wakubwa wa wizi huu, na wale ambao wamefikishwa mahakamani ni dagaa tu, kambale wapo nje huru.
Hebu tuache kumung'unya maneno, tatizo la Tanzania ni kuwa watu ambao wamechukua madaraka ya nchi ni wale ambao kama wangekuwa nchi nyingine yoyote duniani wangekuwa sio kada ya viongozi bali ni organized criminals ambao wengi wao wangekuwa jela na wapo kwenye list za watu hatari wa nchi hizo.
We are so unfortunate kwamba watu wa namna hiyo ndio viongozi katika nchi inayoitwa Tanzania. Tanzania tuna majambazi, wahujumu uchumi, wauaji ambao ndio walioshika dola.
I am still optimistic kwamba ipo siku wao au generations zao watalipa haya wanayowafanyia watanzania.