Swali lisilojibiwa: Ndege ya Qatar iliwezaje kutua KIA?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
cheti.jpg

cheti1.jpg


Waliotorosha Twiga kwenda Uarabuni watinga mahakamani


Saturday, 11 June 2011 (Mwananchi)

Daniel Mjema, Moshi


RAIA wawili wa kigeni na Watanzania wanne, wamepandishwa kizimbani wakituhumiwa kwa makosa nane ya uhujumu uchumi kwa kusafirisha wanyama hai wakiwamo Twiga kwenda Doha, Qatar.

Wanyama hao wenye thamani ya dola 113,715 za Marekani, sawa na Sh170.5 milioni, wanadaiwa kusafirishwa kwenda Doha Novemba 26, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).Washtakiwa hao waliofikishwa kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa Kilimanjaro, Simon Kobelo, ni Kamrani Ahamed (29), raia wa Pakistan na Jane Simon Mbogo (33), raia wa Kenya.

Ahamed ambaye ni mshtakiwa wa kwanza, ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Osaka Traders Limited na Jane ambaye ni mshtakiwa wa nne, anafanya kazi Kampuni ya Equity Aviation Services uwanja wa Kia.Washtakiwa wengine ni Hawa Mang’unuka (51), Mfanyabiashara wa Dar es Salaam, Martin Kimati (58), mkaguzi wa Zoo Sanitary na maofisa wawili wanaoshughulikia ulinzi na usalama uwanja wa Kia.

Maofisa hao ni Veronica Beno (51), ambaye ni ofisa mfawidhi wa ulinzi na usalama katika Kampuni ya Kilimanjaro Airport Development Company (Kadco) inayoendesha Kia na mwenzake Locken Kimaro (50).

Miongoni mwa mashtaka yanayowakabili, ni kuongoza uhujumu uchumi, kumiliki isivyo halali nyara za serikali, kufanya biashara ya wanyama isivyo halali na kusafirisha nje ya nchi nyara za serikali kinyume cha sheria.

Mashtaka hayo yalisomwa mahakamani na Wakili wa Serikali Kanda ya Moshi, Veritas Mlay, anayesaidiana na mawakili wenzake, Rajana Zakayo na Mchunguhela Malangwe, wanaotokea Dar es Salaam.

Washtakiwa Martin Kimath, Veronica Beno, Locken Kimaro na Jane Mbogo wameshtakiwa kwa makosa mbadala, yakiwamo uzembe wa kushindwa kuzuia kosa na kushindwa kutoa taarifa ya watu wenye nyara za serikali.

Wanyama wanaodaiwa kusafirishwa kwa magendo ni Twiga wanne wenye thamani ya Sh40 milioni, Choroa sita wenye thamani ya Sh25 milioni na aina mbalimbali za Swala wenye thamani ya Sh65.7 milioni.

Washitakiwa hao wanakabiliwa pia na mashtaka ya kusafirisha aina mbalimbali ya ndege.

Mshtakiwa wa kwanza ndiye anayekabiliwa na mashtaka mengi zaidi ya kuandaa, kusimamia, kuelekeza na kufadhili mpango mzima wa uhalifu wa kusafirisha kwa magendo nyara hizo.

Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka hayo, kuliibuka mabishano makali ya kisheria kuhusu uhalali wa mashtaka dhidi ya washtakiwa na kama chini ya sheria ya uhujumu uchumi walitakiwa kujibu chochote.Wakili anayemtetea mshtakiwa wa kwanza, Median Mwale, anayesaidiana na Andrew Maganga, walitaka mashtaka hayo yafutwe kwa kuwa yamefunguliwa bila kupata kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali, Zakayo alidai kuwa sheria hiyo inataka kuwapo kibali cha DPP katika usikilizaji, lakini kilichofanywa na upande wa mashtaka ni kufungua mashtaka ya awali.Hakimu Kobelo alikubaliana na hoja za upande wa mashtaka na kuamuru washtakiwa kwenda rumande hadi Juni 24, suala la dhamana litakapoamliwa.


SIMULIZI LA TUKIO (RAIA MWEMA MEI 18, 2011)

bul2.gif
Wanyamapori watoroshewa nje
bul2.gif
Wapelekwa Doha usiku wa manane
bul2.gif
Mlango wa dharura KIA watumika kuwapitisha

NOVEMBA 26, 2010, saa saba usiku, wakati idadi kubwa ya Watanzania wakiwa usingizini, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kulikuwa na pilikapilika kubwa ya kupakia mizigo kwenye ndege ya jeshi la anga la Qatar (Qatar Emir Air Force).

Mizigo iliyokuwa inapakiwa usiku huo mkubwa katika ndege hiyo haikuwa ya kawaida. Wahudumu walikuwa wanapakia wanyamapori hai 130 wa aina 14 tofauti na shehena kubwa ya nyamapori iliyokaushwa, mizigo hiyo yote ni inayotambuliwa kuwa kati ya rasilimali muhimu za Taifa.

Kwa mujibu wa wafanyakazi wa uwanja huo na raia wema kadhaa, wanyama hao hai 130 pamoja na shehena ya nyama zilizokaushwa vilikuwa vinatoroshwa kwenda Doha, Qatar.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, mizigo hiyo ilikuwa inaondoka nchini kinyume cha sheria kwa kuwa haikuwa na kibali wala nyaraka sahihi za kiserikali na walioshiriki katika kuratibu na hatimaye kusafirisha mizigo hiyo nao walifanya makosa ya kuhujumu Taifa.

Kati ya wanyamapori hai 130 wakiwa wa aina 14 tofauti, walikuwamo twiga wanne. Twiga hutambuliwa kama alama ya Taifa, sheria za Tanzania zinaharamisha mnyama huyo mpole kuuawa au kusafirishwa kibiashara nje ya nchi.

Shehena ya viroba vya nyamapori zilizokaushwa inaelezwa kuwa ni ya wanyama wengi waliouawa “kijangili” na mtandao wa watu wanaoendesha biashara haramu ya nyamapori.

Ndege hiyo ya Jeshi la Qatar iliwasili KIA Novemba 24, mwanzo ikionekana kama ndege iliyokuwa katika safari za kawaida hadi Novemba 26 usiku wafanyakazi uwanjani hapo waliposhuhudia ikipakia mizigo wakiwamo wanyama hai.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya kuwasili kwa ndege hiyo wafanyakazi wake na marubani walikwenda kupumzika kwa siku mbili katika hoteli ya Naura Springs ya mjini Arusha.

Vinara wa uporaji huo wa wanyama hai wanatajwa kuwa ni raia wawili wa kigeni ambao wameshirikiana na Watanzania wanne ambao walifanikisha kuwatorosha wanyama hao wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 170.

Kati ya vinara hao mmoja ni raia wa Pakistan, Ahmed Kamran, mkazi wa Arusha na mwingine ni mwanamke, raia wa Kenya, Jane Mbogo, mfanyakazi katika kampuni ya Equity Aviation Service inayotoa huduma katika Uwanja wa KIA ambaye anaishi katika nyumba za uwanja huo.

Raia Mwema limefanikiwa kupata majina ya wahusika wengine, lakini haitayataja sasa kwa kuwa haikuweza kuwasiliana nao.

Raia Mwema imefahamishwa pia kwamba washiriki wengine wa mpango huo wa uhujumu ni Watanzania wanne, ambao taarifa zisizotia shaka zilizokusanywa na gazeti hili kwa muda zinaonyesha kuwa ndio waliofanikisha mkakati wa kuwasadia wageni hao kutorosha wanyama hai hao pamoja na shehena ya nyama zilizokaushwa.

Kati yao ni mwanamke mmoja mkazi wa Dar es Salaam ambaye anamiliki kampuni ya kukamata na kumiliki wanyamapori, mtumishi mmoja mwanamke wa idara ya ulinzi ya kampuni ya KADCO inayosimamia shughuli zote za uwanjani KIA, mtumishi wa Serikali katika Idara ya Mifugo KIA na mtumishi mmoja mstaafu wa Idara ya Ushuru wa Forodha.

Wanyama hao walitoroshwaje?

Duru na taarifa zilizokusanywa na Raia Mwema zinaonyesha kuwa kinara wa usafirishaji wa wanyamapori hao ni Kamran ambaye amekuwa akifanya kazi hiyo kwa kutumia leseni ya kuwakamata wanyamapori hai ya kampuni ya mwanamke mmoja wa Dar es Salaam.

Taarifa hizo zinasema wanyamapori waliotoroshwa walikamatwa katika mapori ya akiba na sehemu mbalimbali za mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na kuhifadhiwa katika nyumba anayoishi Mpakistan huyo katika eneo la Baraa, Manispaa ya Arusha.

Taarifa zinaeleza kuwa Mpakistan huyo amekuwa akiwahifadhi wanyama wa aina mbalimbali kwa muda mrefu katika nyumba hiyo ambayo imejengewa ukuta mrefu unaokadiriwa kufikia futi tisa, na kwamba ndani ya nyumba hiyo kuna zizi kubwa la kuhifadhi wanyama na ndege pori.

Ni kutoka ndani ya nyumba hiyo, Novemba 26, mwaka jana, usiku wa saa tatu, malori matatu aina ya Fuso yaliyokuwa yamesheheni wanyamapori hao hai na viroba vya nyamapori zilizokaushwa, yalisafirisha shehena hiyo hadi uwanja wa ndege wa KIA kabla ya kusafirishwa kwenda Doha, Qatar.

Katika uwanja huo, magari hayo yaliyokuwa na wanyama hao yalipitia lango namba 5B ambalo kwa kawaida hutumika kama lango la dharura, hadi ndani ya uwanja ambamo kazi ya kuwapakia ilianza bila vibali kutoka mamlaka za kiserikali zinazohusika.

Kwa utaratibu, wanyama hao walipaswa kupitishwa kupitia lango namba 5A ambako kuna wakaguzi wa Idara za Ushuru wa Forodha, na idara nyingine za kiserikali ambako vibali vyote vingekaguliwa na kupigwa mihuri kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.

Wakati magari hayo yalipowasili, Jane Mbogo, kwa makusudi, hakuwa ameandaa taarifa za mzigo huo (cargo manifest) kwa kuwa kampuni yake hairuhusiwi kisheria kuhudumia ndege inayozidi tani 40, badala yake alitumia vifaa vya kuazima kutoka kampuni ya kuhudumia ndege ya Swissport kufanikisha kazi hiyo.

“Hawa Equity Aviation Serevice kisheria wanaruhusiwa kuhudumia mizigo ya ndege ndogondogo, na kwa kufahamu hilo, mtuhumiwa alifanya mipango ya kuazima vifaa vya kampuni ya Swissport ili kuwapakia wanyama hao lakini pia alikacha makusudi kuanisha aina ya mizigo iliyokuwa inasafirishwa ili kuharibu kumbukumbu,” alieleza mtoa taarifa wetu.

Aidha, taarifa zinaeleza zaidi kuwa yule mtumishi wa Serikali wa Idara ya Mifugo naye akifahamu fika kuwa wanyamapori hao hawakuwa na vibali na walikuwa wanatoroshwa nje ya nchi, hakukagua vibali vinavyotakiwa katika usafirishaji.

“Kwa kawaida mizigo inayosafirishwa kwenda nje ya nchi, hasa wanyama hai, lazima wawe na nyaraka zote sahihi za kiserikali na nyaraka hizo hukaguliwa na mamlaka zote zinazohusika na usalama na mambo mengine muhimu katika uwanja lakini wakati wanyama hao wakipakiwa mambo hayo muhimu hayakuzingatiwa,” alieleza mtoa taarifa wetu aliyeshuhudia tukio hilo.

Taarifa zinasema kuwa wakati watu hao wakifanikisha mpango huo, askari mmoja aliwasili uwanjani hapo na kuhoji akitaka kuona vibali vya kusafirisha wanyama hao, lakini wahusika walimweleza kuwa “mzigo unaosafirishwa ulikuwa wa kiserikali”.

Mtoa taarifa wetu anaeleza zaidi kuwa juhudi za askari huyo kutimiza wajibu wake ziligonga ukuta baada ya kujibiwa kwa ukali na afisa wa mifugo, ambaye ni afisa mwenzake serikalini, aliyekuwa akisimamia zoezi hilo kuwa “asiingilie kazi zisizomhusu”; huku pia akimtukana matusi ya nguoni.

Akimkariri afisa huyo mtoa habari wetu alieleza: “Wewe mpumbavu? Una akili? Unaingilia kazi zisizo zako na hivi nakuambia kuwa nitakufukuzisha kazi. Huu ni ugeni wa Serikali usipende kuhoji kitu kisichokuhusu na kama hunielewi mfuate huyo Mhindi (Kamran) hapo akupatie vibali.”

Taarifa zinasema askari polisi huyo alipomwuliza mtuhumiwa huyo kuhusu vibali vya kusafirisha wanyama alidai kuwa asingeweza kudurufu (kutoa kopi) vibali hivyo kwa kuwa ni usiku wa manane na kuahidi kuwa angempatia asubuhi yake, lakini hata hivyo vibali hivyo havikuwahi kuwasilishwa hadi leo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, askari huyo alikwenda kutoa taarifa kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha KIA, lakini kwa muda huo tayari ndege hiyo ilikuwa imekwishakuondoka na hakukuwa na hatua zilizoweza kuchukuliwa kuzuia mpango huo.

Habari zaidi zinasema ya kuwa baada ya kukamilika kwa kazi ya kuwapakia wanyamapori hao, wahusika waliwapatia wafanyakazi walioshiriki kupakia mzigo kiasi cha shilingi 150,000 za Kitanzania ili wagawane, mgawo huo ukifanyakia uwanjani hapohapo.

Taarfa za karibuni zaidi kuhusu suala hilo zinasema tayari Polisi walikuwa wamefungua jalada la upelelezi wa shauri hilo na kupendekeza watuhumiwa wote waliotajwa wafikishwe mahakamani, lakini katika mazingira yanayotia shaka hadi sasa suala hilo limekaliwa. Miezi mitano baada ya tukio hilo, hakuna hatua zilizochukuliwa.

Kauli za watuhumiwa


Rai Mwema wiki hii ilizungumza na Kamran kwa njia ya simu ikimtaka kuzungumzia suala hilo, lakini alikana kuhusika na akaongeza kuwa hafanyi biashara hiyo.

“Sihusiki na jambo unaloniuliza. Nafikiri umepiga namba isiyo sahihi (wrong number). Si mimi,”alisema na kisha kukata simu yake.

Kwa upande wake, Jane Mbogo alidai kuwa yeye ni mtumishi wa kampuni ya Equity Aviation Services; hivyo masuala yote hayo aulizwe Mkurugenzi wake na akatoa namba ya simu ambayo hata hivyo, ilipopigwa ilionyesha ya kuwa haitumiki.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Swissport, Gaudance Temu, alithibitisha vifaa vya kampuni yake kutumika kupakia mzigo huo na kuongeza kuwa walifanya hivyo baada ya kukodishwa na kampuni ya Equity Aviation Service na walilipwa fedha kiasi cha dola 3,000 za Kimarekani kwa kazi hiyo.

Alisema Temu kuhusu suala hilo: “ Ndiyo, nakumbuka Polisi walikuja kuhoji kuhusu ushiriki wetu katika madai ya kutoroshwa kwa wanyama hao. Lakini tumewaeleza kuwa hatuhusiki, ila vifaa vyetu vilikodishwa na wenzetu wa Equity na walitulipa kwa kazi hiyo. Nafikiri ukienda ofisi yetu ya KIA pale kuna risiti ya malipo hayo kuthibitisha”.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya KADCO ambayo ndiyo inayoendesha Menejimenti ya KIA, Marcus Van De Kreeke, alithibitisha madai ya kutoroshwa kwa wanyamapori hao na kuongeza kuwa hata hivyo menejimenti haihusiki na suala hilo.

“Kazi yetu kama KADCO ni kulinda usalama wa abiria na ndege zinazotumia uwanja huu kwa safari zao, lakini sisi hatuhusiki na usafirishaji wa mizigo inayopita katika uwanja. Hiyo ni kazi ya mamlaka nyingine,” alisema Van De Kreeke.

Aliongeza: “Polisi tayari wameanzisha uchunguzi. Nafikiri tuwaache wafanye kazi yao na tuone uchunguzi wao utaleta majibu gani. Ila kwa upande wetu hatuna tatizo. Tutawapa ushirikiano wa kutosha.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lukas Ng’omboko naye alithibitishia Raia Mwema kuwapo kwa tukio hilo, na kufafanua kuwa upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa unaendeshwa na maafisa wa timu maalumu ya Polisi kutoka Makao Makuu ya jeshi hilo.

“Tukio hilo ni la kweli lakini tafadhali wasiliana na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. Wao ndio waliounda timu maalumu ya askari wa upelelezi na kwa ufahamu wangu walikuwa wameanza kazi ya kuwahoji watuhumiwa,”alisema Kamanda huyo.

Raia Mwema haikufanikiwa kumpata Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba kuelezea hatua walizofikia katika upelelezi wa tukio hilo.

Utorashaji wa raslimali za nchi katika sekta za madini na maliasili umekuwa moja ya matatizo sugu ambayo Tanzania inakabiliana nayo na sababu kubwa inaelezwa kuwa ni kushamiri kwa vitendo vya kifisadi miongoni mwa maafisa wa serikali waliopewa mamlaka ya kusimamia rasilimali hizo kwa niaba ya wananchi.

My Take:
Ukisoma juu juu unaweza kukosa kitu muhimu zaidi ambacho ni kashfa yenye kuhitaji majibu - Ndege ya jeshi la Qatar iliwezaje kutua nchini? Tatizo siyo wanyama kusafirishwa tu lakini ndege ya taifa jingine imeweza kuingia na kuondoka nchini bila vyombo vyetu vya usalama kuwajibika! Mnakumbuka tuliwahi kununua rada ya kisasa kwa ajili ya "ulinzi wa anga"?

Sasa wamuulize Waziri Mkuu hili swali.. "ndege iliwezaje kuingia na kutoka nchini bila kibali cha jeshi"? mtachoka jibu lake.. "tutaanza mchakato wa kuchunguza..."
 

Attachments

  • QATAR-case.zip
    1.6 MB · Views: 381
je nikweli ndege ya jeshi iliagizwa nchini kwa nguvu ipi?mana huwezi tua katika nchi yoyote duniani na kutekeleza uhalifu pasipokuwepo mkono wa mwenye nchi. Je ni kweli wale watuhumiwa ndio hasa waliokula njama za kutorosha nyara izo pasipokuwepo watu wazito {vigogo} nyuma yao? Mi nadhani kuna siri ambayo ipo Nyuma ya hawa wanaotuhumiwa.
 
he he hee "mchakato wa uchunguzi upo mbioni", you read my mind MM. Kuna mawaziri watano walitumwa na JK kwenda kumaliza mgogoro wa kule Babati. MAWAZIRI, siyo maafisa wa wizara, kufika kule wakamuagiza mkuu wa mkoa aunde tume, naye akamuagiza mkuu wa wilaya kufuatilia, mwisho wa yote hamna kilichotatuliwa hadi mauaji yakatokea.
 
We have a long way to go! Mimi ndo maana saa nyingine huwa nafikiria JKT bado tunaihitaji kwa ajili ya kulinda nchi yetu na maadili ya taifa letu.

Itakuwa jambo mhimu sana vijana wote kabla ya kujiunga na vyuo mbalimbali kupitia huko na kuweza kufundishiwa uzalendo, mshikamano na kuwa na uchungu wa dhati.

Watu wengi tena watumishi wa umma, leo hii hawawezi kufanya kazi kwa ajili ya kuendeleza taifa isipokuwa wanashindana kuibia taifa kitu ambacho huwafanya wakose hata ubunifu wa kuongeza ufanisi kwenye kazi zao.
 
hapa ni uhuni tu jamani kweli haingii akili kama ndege ya kijeshi itue KIA , wanyama 140 (aina mbalimbali wachukuliwea bila taarifa zozote kwa nchi huu ni uongo tena naona hao waliokamatwa wanaonewa wa mkamate JK, waziri mhusika wa kipindi kile, polisi pori, {maafisa pori} hata pia mkuu wa usalama wa taifa naye afikishwe mahakamani ndio wanahusika na si hao.
 
Kwa kuleta hii kesi mahakamani, serikali imekiri kuwa kuna ndege iliingia nchini aidha kwa kufuata sheria au kinyume cha sheria.

Lakini ingekuwa ni ndege ya kiraia hilo lingekuwa kashfa tosha lakini kuwa ni ndege ya kijeshi ni kashfa mabayo kama waandishi wetu wangekuwa na ujasiri wangetaka maelezo toka JWTZ.. muone watu wanavyoweza kujiuma uma meno!! Hii ni kashfa kubwa kweli ambayo Dr. Hussein Mwinyi anatakiwa aitolee maelezo.
 
Taifa hili linawayawaya ! Nikiwatizama viongozi wetu napata jibu moja , tunu ya uongozi haipo nasi. Hatuna watu makini wala waadilifu.Tunagenge la watu duni na dhaifu ambao umaskini wa Watu wetu si kipaumbele ila ni faida ya kujipatia kura.Hawana uchungu na raslimali zetu ! Tumekua wajinga , kabisa.
 
My Take:
Ukisoma juu juu unaweza kukosa kitu muhimu zaidi ambacho ni kashfa yenye kuhitaji majibu - Ndege ya jeshi la Qatar iliwezaje kutua nchini? Tatizo siyo wanyama kusafirishwa tu lakini ndege ya taifa jingine imeweza kuingia na kuondoka nchini bila vyombo vyetu vya usalama kuwajibika! Mnakumbuka tuliwahi kununua rada ya kisasa kwa ajili ya "ulinzi wa anga"?

Sasa wamuulize Waziri Mkuu hili swali.. "ndege iliwezaje kuingia na kutoka nchini bila kibali cha jeshi"? mtachoka jibu lake.. "tutaanza mchakato wa kuchunguza..."..............................Kwa kuleta hii kesi mahakaman serikli imekiri kuwa kuna ndege iliingia nchini aidha kwa kufuata sheria au kinyume cha sheria. Lakini ingekuwa ni ndege ya kiraia hilo lingekuwa kashfa tosha lakini kuwa ni ndege ya kijeshi ni kashfa mabayo kama waandishi wetu wangekuwa na ujasiri wangetaka maelezo toka JWTZ.. muone watu wanavyoweza kujiuma uma meno!! Hii ni kashfa kubwa kweli ambayo Dr. Hussein Mwinyi anatakiwa aitolee maelezo.


Couple of things:

1. Haven't really bought this paper for a while. These days, from looking online and borrowing copies, too many vapid columnists who can't write (common to many mainstream papers hapa Bongo, mind you), too much nepotism, too much smug, dully-written humanism , far, far, too Dar centric (I suspect it's stuffed with posho interns who think some of us commenting hapa JF are a bunch of non patriotic nutters na kazi yetu ni kuwapiga wao vita) .

And their editorial staff are exceptionally ill-mannered. I blame it on owners.


2. What was so difficult for the journalist kuwauliza watu wa aviation na kupata ukweli kuhusu the so called DEGE LA JESHI LA QATAR lilioingia Tanzania?

surely its not that difficult kupata :

a) Ndege ilikuwa ina namba zipi?

b) Ilikuwa inaendeshwa na pilot wepi

c) Iliingia na crew wangapi

d) Je hao the so called WANAJESHI WA QATAR walikuwa na vyeo gani

e) Je JWTZ walihusika kutoa vibali

f) Je ndege ilifuata taratibu kuingia katika airspace ya Tanzania?


Kwa haraka haraka utaona kuwa mwandishi wa habari ameamua kuacha either by commission or omission kuweka these vital details na kinachooendelea hapa ni the usual MU ya not only ARAB BASHING bila kuwa na objective journalism

As far as I know inawezekana ndege ilikuwa ni cargo plane ambayo ilikodishwa from Jeshi la Qatar au something like that lakini I wont jump the gun bila kupata FACTS otherwise tutakuwa tunaingia in the same trap ya SUPERMARKET JOURNALISM and mwananchi like many other rags wameprove kuwa na they're all un interesting,un informative, obsessed, irritating or lacking to some degree.

For arguments sake, kwa kukupasha tuu ni kuwa hakuna ndege inayoingia kwenye airpsace ya Tanzania bila kupewa approval na wahusika
 
je nikweli ndege ya jeshi iliagizwa nchini kwa nguvu ipi?mana huwezi tua katika nchi yoyote duniani na kutekeleza uhalifu pasipokuwepo mkono wa mwenye nchi. Je ni kweli wale watuhumiwa ndio hasa waliokula njama za kutorosha nyara izo pasipokuwepo watu wazito {vigogo} nyuma yao? Mi nadhani kuna siri ambayo ipo Nyuma ya hawa wanaotuhumiwa.

No, hapo kwenye red inawezekana, tena sana. Ni hivi karibuni Wamarekani walitua huko Abbotabad Pakistan wakatekeleza "uhalifu" wa kumuua Osama bin Laden bila nchi mwenyeji kuwa na taarifa yoyote. Inawezekana sana.
 
We have a long way to go! Mimi ndo maana saa nyingine huwa nafikiria JKT bado tunaihitaji kwa ajili ya kulinda nchi yetu na maadili ya taifa letu.

Itakuwa jambo mhimu sana vijana wote kabla ya kujiunga na vyuo mbalimbali kupitia huko na kuweza kufundishiwa uzalendo, mshikamano na kuwa na uchungu wa dhati.

Watu wengi tena watumishi wa umma, leo hii hawawezi kufanya kazi kwa ajili ya kuendeleza taifa isipokuwa wanashindana kuibia taifa kitu ambacho huwafanya wakose hata ubunifu wa kuongeza ufanisi kwenye kazi zao.
Kwani Hussein Mwinyi, Pinda, Kikwete na wazee wengine wengi serikalini hawajapita JKT?
 
Kwa kuleta hii kesi mahakaman serikli imekiri kuwa kuna ndege iliingia nchini aidha kwa kufuata sheria au kinyume cha sheria. Lakini ingekuwa ni ndege ya kiraia hilo lingekuwa kashfa tosha lakini kuwa ni ndege ya kijeshi ni kashfa mabayo kama waandishi wetu wangekuwa na ujasiri wangetaka maelezo toka JWTZ.. muone watu wanavyoweza kujiuma uma meno!! Hii ni kashfa kubwa kweli ambayo Dr. Hussein Mwinyi anatakiwa aitolee maelezo.

Hapo kweny red; na ndio maana wamekimbiza vidagaa mahakamani haraka haraka ili kuepusha hoja yoyote endapo itaibuliwa Bungeni au mahali pengine popote - jibu litakuwa rahisi tu "KESI IKO MAHAKAMANI, HAIRUHUSIWI KUJADILIWA" na mkuu atakuwa amepona angalau kwa sasa. Yaani kila kitu ni funika kombe mwanaharamu apite, ndio Tanzania yetu.
 
Mzee mwanakijiji,

Huijui nchi yetu nini? Hao waliokamatwa ni ktk kupoteza ushaidi kwa wakubwa waliohusika, kwani mimi naamini kabisa kuwa ile ni ndege ya jeshi na Viongozi wakuu walijuwa kabusa kuwa kuna ndege ya jeshi ipo nchini na walijuwa nini imefuata ile ndege, na hiyo si biashara ya mtu mmoja kama tunavyofikilia inawahusu watu wakubwa sana hapa nchini

Inasemekana wakati wanaingiza wale wanyama kwa mlango wa nyuma wananchi walitoa taarifa usiku ule lakini hakuna kilichofanyika mpaka ndege inapaaaaaaa na baadae kujifanya kuanza uchunguzi baada ya biashara kufanyika

tunazidi kubadilishana mali zetu kwa vyandaluwa
 
DaahhhLazima kuna watu wa NyandaZa juu ambao wanajua hilihawo wengine hapo airport wameshikishwa tu Au wametimiza amri ya mkuu .. Maana kuna procedure nyingi za kufuataKwenye international flights yeyote ile ....
 
Ile rada tuliuziwa ni bosheni, haifanyi kazi kabisaaaaa

Inawekana ni bosheni lakini kwenye madili ya kishenzi kama haya inaweza kufanyiwa hujuma au ikazimwa kwa muda ili kufanikisha "mradi"; hii ndio Tanzania.

Halafu naanza kupata picha ni kwanini barabara ya Serengeti ilikuwa inapigiwa upatu kiasi hicho na wanasiasa magamba pamoja na wataalamu kuonya juu ya athari nyingi kuhusiana na mradi huo. Kumbe lengo lilikuwa kurahisisha madili ya dizaini hii.

Jamani wanasiasa ioneneeni huruma nchi yetu. Adui nambari wani wa nchi yetu kwa sasa ni wanasiasa magamba.
 
Na hili nalo jipya!!hutasikia waziri maliasiri,ulinzi wala usalama wa taifa kutolea tamko kwa kujidai kesi iko mahamakani,,aibu sana ile rada,_salama wa taifa wamejaa kila kona wanafanya nini sasa au wanamsubiri Mbowe na Slaa wawakamate??aibu sana usalama ulikuwa zamani siku hizi nao wapiga deal tu na hawajui wajibu wao wananunulika tu!!!aibu serikali ya fresh fresh funika lipite style
 
Back
Top Bottom