Mbunge Saashisha Mafuwe aishukuru Serikali ya CCM kwa kumaliza mgogoro wa muda mrefu KIA

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mbunge wa Jimbo la Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Saashisha Mafuwe amekishukuru Chama Cha Mapinduzi na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia kwa zoezi la kumaliza mgogoro wa Ardhi katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA)

Mhe. Saashisha Mafuwe amesema kuwa ulikuwa ni mgogoro wa muda mrefu ambapo yeye kama Mbunge wa Hai na Mwakilishi wa Wananchi Bungeni amekuwa akilisemea mara kwa mara ili Serikali iwalipe Wananchi fidia ya Ardhi yao ambayo ardhi sasa itakuwa sehemu ya Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA)

Mhe. Saashisha Mafuwe amesema tayari Serikali ya CCM na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa Shilingi Bilioni 11 kwaajili ya kuwalipa Wananchi wanaotakiwa kupisha maeneo ambayo yanatumika kuboresha Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) kama sehemu ya kukuza Utalii nchini.

Aidha, Mhe. Saashisha Mafuwe amepongeza juhudi za kukamilisha Makabidhiano ya Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) uliokuwa unaendeshwa na Kampuni ya Serikali ya KADCO ambapo sasa KIA utakuwa chini ya Mamlaka Viwanja vya Ndege yaani Tanzania Airport Authority (TAA).

Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 14 Februari, 2022 akiwasilisha taarifa ya mgogoro wa Ardhi pale KIA, Saashisha Mafuwe aliitaka Serikali kuingilia kati mgogoro uliopo kati ya Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro na Wananchi wa eneo hilo.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom