Uwanja wa Ndege wa KIA Sasa Kusimamiwa na TAA baada ya KADCO Kumaliza Muda wake

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

UWANJA WA NDEGE WA KIA SASA KUSIMAMIWA NA TAA BAADA YA KADCO KUMALIZA MUDA WAKE

Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa leo tarehe 11 Novemba, 2023 ameshuhudia na kusimamia Makabidhiano ya Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) uliokuwa chini ya KADCO ambao sasa utakuwa chini ya TAA.

Akizungumza katika Makabidhiano hayo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile amesema kuwa Makabidhiano ya KIA kutoka KADCO kuja TAA yanafanyika baada ya agizo la Bunge na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuagiza KADCO kukabidhi KIA kije TAA baada ya KADCO kumaliza muda wake.

Makabidhiano kati ya TAA na KADCO yameshuhudiwa na Menejimenti ya KADCO, Menejimenti ya TAA, Watumishi Wizara ya Uchukuzi, Kamati ya Bunge ya PIC na Kamati ya Bunge ya PAC katika ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Airport, Dar es Salaam.
 

Attachments

  • 833A8446(1).JPG
    833A8446(1).JPG
    2.7 MB · Views: 4
  • 833A8489(1).JPG
    2.4 MB · Views: 4
  • DSC00353.jpg
    2.4 MB · Views: 3
  • DSC00436.jpg
    1.7 MB · Views: 4
  • DSC00442.jpg
    1.8 MB · Views: 3
  • DSC00395.jpg
    2 MB · Views: 3
Back
Top Bottom