Swali lisilojibiwa: Ndege ya Qatar iliwezaje kutua KIA?

inasikitisha sana, yaani fuso tatu zinaongozana kuin gia kia ambao ni uwanja wa ndege wa kimataifa
bila chombo chochote cha usalama (ispokuwa askari polisi moja uwanjani) kushtuka!!
this is a huge intelligence failure. kwani hizo fuso zingeweza kuwa zimesheheni mamluki ambao wamepewa jukumu
la kukamata kia.

mola tusaidie
 
Usalama wa taifa lzm unajua,ikulu inajua,hao waliopelekwa mahakamani ni funika kombe mwizi apite
Jamani ingewezekana tungeanza upya tu,tushapotea kama taifa,tena siku nyingi
 
mimi nimechoka ndege ya jeshi la nchi nyingine inatua na kuiba nyara za serikali na kuondoka salama.
 
Kwa kuleta hii kesi mahakamani, serikali imekiri kuwa kuna ndege iliingia nchini aidha kwa kufuata sheria au kinyume cha sheria.

Lakini ingekuwa ni ndege ya kiraia hilo lingekuwa kashfa tosha lakini kuwa ni ndege ya kijeshi ni kashfa mabayo kama waandishi wetu wangekuwa na ujasiri wangetaka maelezo toka JWTZ.. muone watu wanavyoweza kujiuma uma meno!! Hii ni kashfa kubwa kweli ambayo Dr. Hussein Mwinyi anatakiwa aitolee maelezo.

Hajatolea maelezo ya mabomu yaliyoua Watanzania kule Gongo la Mboto na Mbagala, unadhani atasema lolote kuhusu ndege hii ya Kijeshi toka Qatar ambayo inaelekea iliingia nchini bila kufuata taratibu za kufanya hivyo? Tusubiri tuone lakini mimi sina imani kama atasema chochote na kama atasema basi itakuwa ni kujikanyagakanyaga tu kwamba itaundwa tume kuchunguza ndege hii iliingiaje nchini bila kufuata taratibu za kuingia nchini mwetu na blah blah nyingi halafu hoyo ripoti wala tusiisikie imeishia wapi!
 
Polisi na wana usalama, wakiongozwa na kamanda wa operations ambaye mara nyingi amekuwa mkali sana kwa matatizo ya maandsamano na viongozi wa upinzani walikuwa wapi??? Au hili haliwahusu???
 
Mzee Mwanakijiji,
Nimevamia hii mada lakini nimeshindwa kuelewa swali lako haswa kwa sababu sidhani kama cargo plane za mashirika ya ndege zina utaratibu sawa na passenger flights. Nikiwa na maana kwamba ndege za mizogo za mashirika ya ndege ya nje hutua ktk viwanja vya Dar, Kilimanjaro a Mwanza tofauti kabisa na utaratibu uliopo wa ndege za abiria..

Kwa hiyo, zipo ndege za mizigo zinakuja Tanzania lakini hawana au hakuna ndege za abiria za shirika hilo hilo zinakuja kwetu.
 
nchi hii sijui usalama uko wapi,
mara wanyama wanaibiwa , mara mabomu tuliyonunua kwa kodi zetu yanatuua wenyewe,
mara askari kapiga raia risasi, ukirudi nyumbani kuna ulinzi shirikishi majambazi wantuvamia hakuna kulala ,ukipanda magari ya mikoani tunakufa kwa ajali, mchana nzi wa kutosha, usiku mbu kibao. maji ya shida , umeme wa mgao, maisha magumu,
mfumuko wa bei,wachina wanauza mpaka mchicha, ukitaka mkopo lete dhamana,ukitaka kujenga lete 9milion upate kiwanja na mshahara laki3 kwa mwezi.makaburi mengi ni ya wikiwa.
labda uwe fisadi
:fear::attention:

  • Thanks
Reactions: Nzi

My Take:
Ukisoma juu juu unaweza kukosa kitu muhimu zaidi ambacho ni kashfa yenye kuhitaji majibu - Ndege ya jeshi la Qatar iliwezaje kutua nchini? Tatizo siyo wanyama kusafirishwa tu lakini ndege ya taifa jingine imeweza kuingia na kuondoka nchini bila vyombo vyetu vya usalama kuwajibika! Mnakumbuka tuliwahi kununua rada ya kisasa kwa ajili ya "ulinzi wa anga"?

Sasa wamuulize Waziri Mkuu hili swali.. "ndege iliwezaje kuingia na kutoka nchini bila kibali cha jeshi"? mtachoka jibu lake.. "tutaanza mchakato wa kuchunguza..."

Heshima kwako mkuu!!!

Hapo kwenye maandishi mekundu ni kua vyombo vyetu vya usalama kuanzia sungusungu hadi UWT/TISS vina wajibu wa kuwatafuta wale wote wanaomsema vibaya muheshimiwa sana na serikali yake! Wajibu wa kulinda rasilimali la taifa hauko kwenye majukumu yao kwa sasa!!

Hivyo mkuu husishangae kuona yale yaliyotokea KIA!!
 
nchi hii sijui usalama uko wapi,
mara wanyama wanaibiwa , mara mabomu tuliyonunua kwa kodi zetu yanatuua wenyewe,
mara askari kapiga raia risasi, ukirudi nyumbani kuna ulinzi shirikishi majambazi wantuvamia hakuna kulala ,ukipanda magari ya mikoani tunakufa kwa ajali, mchana nzi wa kutosha, usiku mbu kibao. maji ya shida , umeme wa mgao, maisha magumu,
mfumuko wa bei,wachina wanauza mpaka mchicha, ukitaka mkopo lete dhamana,ukitaka kujenga lete 9milion upate kiwanja na mshahara laki3 kwa mwezi.makaburi mengi ni ya wikiwa.
labda uwe fisadi
:fear::attention:

Pole mkuu!
Nakupata sana!!
Maisha ya Bongo sasa ni msongo wa mawazo 24/7!!!
 
Mzee Mwanakijiji,
Nimevamia hii mada lakini nimeshindwa kuelewa swali lako haswa kwa sababu sidhani kama cargo plane za mashirika ya ndege zina utaratibu sawa na passenger flights. Nikiwa na maana kwamba ndege za mizogo za mashirika ya ndege ya nje hutua ktk viwanja vya Dar, Kilimanjaro a Mwanza tofauti kabisa na utaratibu uliopo wa ndege za abiria..

Kwa hiyo, zipo ndege za mizigo zinakuja Tanzania lakini hawana au hakuna ndege za abiria za shirika hilo hilo zinakuja kwetu.

Mkuu, mimi si Mwanakijiji, lakini naomba nimsaidie!!

Hukupaswa kuvamia mada kabla hujaisoma vizuri!!! Ila ukisoma vyema uzi wake, utamuelewa.
Anyway ni kwamba, hapa kinachoengelewa na zaidi ya ndege ya mizigo; inaongelea ndege ya KIJESHI ya Qatar!!! Ndege ambao imepita kwenye anga la TZ, ikatua kwenye uwanja wa TZ na kupaa kutokea uwanja wa TZ kupitia anga la TZ bila vyombo vya usalama kugutukia hiyo tamthilia!!!!!

Hilo ndio linamlomtatiza Mwanakijiji

Asante!!
 
Kwa kuleta hii kesi mahakamani, serikali imekiri kuwa kuna ndege iliingia nchini aidha kwa kufuata sheria au kinyume cha sheria.

Lakini ingekuwa ni ndege ya kiraia hilo lingekuwa kashfa tosha lakini kuwa ni ndege ya kijeshi ni kashfa mabayo kama waandishi wetu wangekuwa na ujasiri wangetaka maelezo toka JWTZ.. muone watu wanavyoweza kujiuma uma meno!! Hii ni kashfa kubwa kweli ambayo Dr. Hussein Mwinyi anatakiwa aitolee maelezo.

Dr. Hussein Mwinyi ?
 
Kama jambo kama hili limefanyika na viongozi wa ngazi zote husika wanakaa kimya na hakuna hatua iliyochukuliwa hadi sasa, basi kuna tatizo. Katika baadhi ya ofisi nyeti za serikali pana watu hawajui mambo wanayofanya. unafika ukitaka msaada na wewe unakuwa mshauri wa jinsi ya kupatiwa msaada. ajira maeneo mengine zimebeba watu wa ajabu sana hata kufafanua hapa haifai .
Issue ya KIA wapo watu wanajoua kilichofanyika ila kwa kuwa watz wana njaa, ulafi, umasikini, na kukosa ustaarabu mambo kama haya wanaona fahari kuyafanya ili kujinusuru na adha ya maisha.Hongera sana MM:attention:
 
Watanzania tutaendelea kufanya vitu visivyoeleweka hadi lini. Waliopelekwa mahakamani ni wale walishiriki njama za kutorosha wanyama nje ya nchi. Wahusika wakuu wa utoroshaji wanyama hawajapelekwa mahakamani. Isije ikawa kama kesi ya Zombe, ambapo yeye alikuwa mshiriki katika mauaji, lakini kwa vile katika kesi yeye ndiye aliyekuwa mshatakiwa mkuu wa mauji alishinda kesi kwa sababu yeye hakuwa aliyefyatua risasi. Vivyo hivyo, waliotorosha wanyama wako wapi? Walioshiriki ni washiriki tu wa kosa lakini si wahusika wakuu.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Japo nimesema kuwa sitaki kuandikia mambo ya uchunguzi tena; hili nalo linanifanya nifikirie maana documents ambazo zimepitishwa kona hizi zinatisha! ooh well.. !!

yaaani swala la kukimbia kuandika habari za kiuchunguzi ni sawa na kuruhusu nchi yetu tuzidi kuibiwa,huna haja ya kukimbia na kuogopa kuandika habari za uchunguzi,kuwa imara na simamia matakwa yako,

kwa ushauri tu unafaa sana kuandika habari za uchunguzi ingawaje kwa bongo watu wapo kivisa sana hususani polisi najuwa ipo siku watakubambikia kesi kama muru pale tu utakapo ingilia maslahi yao,take care

ila kamanda mala nyingi hatishiwi nyau kaza buti twende MMJ
 
yaaani swala la kukimbia kuandika habari za kiuchunguzi ni sawa na kuruhusu nchi yetu tuzidi kuibiwa,huna haja ya kukimbia na kuogopa kuandika habari za uchunguzi,kuwa imara na simamia matakwa yako,

Hapa naona umeamua kunikutakana. Nimesema mahali popote sitaki kuandika kwa sababu kuna mtu namuogopa au kitu? Au sababu zangu hazikueleweka kiasi cha kunitaka nianze kufafanua moja baada ya nyingine. Kwa ufupi nimechoka wengine muendelee hasa unapokutana na madudu kama haya.
 
CCM wanafanya nini hasa hapa, mnazikumbuka ziara za jamaa kule uarabuni? sasa haya ndo matunda yake, yahani mi natamani kulia uwiiii iiiiiiiii hhhaaaaa uuuuuuuuuuuuuuuu iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ccm eeeemnakufa twafwaaaaa jamani Mungu inusuru nchi yetu kutoka kwa CCm tunapoteza kila kitu chetu
 
Back
Top Bottom