Spika Sitta amtimua nje Cheyo (UDP) Bungeni kwa kubishana naye!

si unjua viongozi wengi wa ccm vyeti vya kugushi, naona sitta akadhani cheyo nae amegushi

yaani spika inamaanisha hajawi kuona hata kwenye magazeti kwamba kuna madawa ambayo yantupwa kwenye mito na kuleta madhara
hiyo acid ikishaingia kwenye maji(river) makali yake yanabadilika, yeye anasema acid inakuumiza hapo hapo kwani ameambiwa ni ya kumwagiwa dry...

mtu akikumwagia acid moja kwa moja kavu ndio inakuumiza hapohapo lakini ikishaingia kwenye river inakuumiza pole pole ( hii nimejua kwa kusoma magazeti/habari hauitaji kuwa chemist kujua hili, je spika ni mbumbu kiasi hicho au ubabe tuu).


Hivi hata limao si acid wakuu, huyu sita anadhani anaelewa kila kitu ama? hiyo acidi gani ambayo ikimwagwa kwenye mto haiwi diluted? Kuna haja ya kwenda chuo kikuu kusomea hili?
 
Ubabe huu unanikumbusha ile kaulu iliyotolewa siku za nyuma kuwa "Naibu spika asikurupuke kuendesha mjadala fulani wakati spika hayupo" Ukitafakari kwa kina utajua wapi ndiyo pana matatizo
 
hehehehe Mzee Sita kidumu chama cha mapinduzi, mapinduzi oyeeeeeeeeeeee dah hivi spika amesoma kaishia wapi? Tunaomba CV ya Sita tunaweza tukawa tunamwonea bure hapa.
 
Anaposema madhara ni ya mara moja ana maana gani? maana kidogo hiyo kauli mimi sijaielewa vizuri.
 
wababe kwa tz wamezidi ????!!! kwani bila ubabe mambo hayaendi ??? udk mbaya ndo maana hatutapata maendeleo hata kiama kitafika . kuweni waungwana tutfika mbali lakini kibabe ni sawa na hatua moja mbele na tano nyuma sasa je hapa waenda mbele nyuma???!!!
 
Kama hiyo ndiyo 'Speed and Standards' aliyowaahidi watanzania basi Shughuli ipo... Ila watanzania tunaweza kuchemsha dawa ya Sitta na CCM kwa ujumla ili wainywe mwakani,
Tanzania bila ufisadi yawezekana, play your part.
 
Mimi ni mgeni kwenye JF ndo mara yangu ya kwanza kucomment.

Kwa upande wangu Spika hana makosa kama wengi walivyochangia

Jana kile kipindi nilikiona live jioni; Wote wawili yaani Mh. Cheyo na Spika wote wanamakosa. Cheyo alishakalishwa chini na Spika tiyari hiyo ni sheria ya bunge hapaswi kuhoji tena hata iweje lazima uheshimu Kiti jamani lile ni bunge tofauti na kumbi nyingine unaweza kufanya chochote!! Na Spika anamakosa kwani hakuelewa swali akauliza lirudiwe Cheyo akaanza kuelezea kusudi amueleweshe Spika akajitahidi kutokuelewa hata kabla Cheyo hajamaliza akamjibu yeye badala ya Mh. Buliani ambaye ni waziri, ikaonekana Spika alikuwa anamkingia kifua Burian asiulizwe swali. Kwa hiyo wote wawili wanamakosa.
 
Kwa kulinda maslahi ya Barick na unyama wake anaofanya kwenye migodi kwa kutumia watawala waliopo kwenye system.Sitta alitumia counter attack ili amnyamazishe Cheyo.
Hii migogo hasa ya barick inaharibu sana social life za watu waliopo maeno ya migodi, mfano Kahama wananchi hawanufaiki na chochote, barabara mbovu, hali ya uchumi ngumu kwani hakuna mzunguko wa hela, pesa yote inakwenda nje, wanatimua vumbi na kuna wakati mvua ilinyesha maji ya mvua yakuwa mekundu. Binafsi naombea hata bora haya madini yasingekuwepo kabisa
 
Ni mimi tu au kiburi cha wabunge wa CCM kinazidi? Maana kaanza Pinda na kauli zisizo eleweka na sasa ni huyu spika. The only way to bring these people down to earth is through the ballot box. I think loosing their seats next year will humble them.

I think there might be a problem, watu wengi Tz wamekasirika tena sana lakini sasa kuna wengine wanaamini kutokupiga kura ndio kuwakomoa hawa wababe mafisadi wa CCM. ninawajua watu wawili ambao wameharibu kadi zao za kura eti kwa sababu wamekasirika na wengine wengi ambao wamesema hawatapoteza muda wao kupanga msitari na kupiga kura.

Tuhimizane jamani tena kwa makundi tukianza na wale walio karibu na sisi, kupiga kura ndio njia pekee itakayotusogeza angalau hatua chache kuelekea kwenye demokrasia ya kweli
 
Unafikiri kwa nini wengine huwa tunadai rekodi za yaliyotamkwa neno kwa neno?

Watu wanaweza kutumia kurasa mia wanajadili na kulaani utata wa kauli huku hakuna mwenye rekodi ya kilichosemwa. Eti mmoja kamuuliza mwenzake "wewe ni chemistry," Cheyo akajajibu yeye kasomea "Textile Chemistry," Sitta akamwambia umesahau chemistry, nyamaza, Cheyo akaendelea kuuliza, akaambiwa kaa chini, wao wapinzani ni madikteta, "sajenti mtoeni nje"! Mazungumzo ya nusu dakika wakafukuzani bungeni!

Tape no tape. Six alisema hivyo.
 
Ndio maana nasema kuwa Kiburi hiki kitatolewa na Watanzania kuchagua wabunge wengi wa Upinzani
 
Mimi ni mgeni kwenye JF ndo mara yangu ya kwanza kucomment.

Kwa upande wangu Spika hana makosa kama wengi walivyochangia

Jana kile kipindi nilikiona live jioni; Wote wawili yaani Mh. Cheyo na Spika wote wanamakosa.
Ama! sasa Spika ana makosa au hana?
 
Bunge ni la CCM; Serikali ni ya CCM; Vyombo vya HABARI vingi vinamilikiwa na wanaCCM na CCM ina vya kwake; Watanzania tulio wengi ni wanaCCM; Watafanya wanavyotaka.
 
Mimi ni mgeni kwenye JF ndo mara yangu ya kwanza kucomment.

Kwa upande wangu Spika hana makosa kama wengi walivyochangia

Jana kile kipindi nilikiona live jioni; Wote wawili yaani Mh. Cheyo na Spika wote wanamakosa. Cheyo alishakalishwa chini na Spika tiyari hiyo ni sheria ya bunge hapaswi kuhoji tena hata iweje lazima uheshimu Kiti jamani lile ni bunge tofauti na kumbi nyingine unaweza kufanya chochote!! Na Spika anamakosa kwani hakuelewa swali akauliza lirudiwe Cheyo akaanza kuelezea kusudi amueleweshe Spika akajitahidi kutokuelewa hata kabla Cheyo hajamaliza akamjibu yeye badala ya Mh. Buliani ambaye ni waziri, ikaonekana Spika alikuwa anamkingia kifua Burian asiulizwe swali. Kwa hiyo wote wawili wanamakosa.

Dada Margreth unahakika ulielewa ulichosikia na kuona ???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom