Spika Sitta amtimua nje Cheyo (UDP) Bungeni kwa kubishana naye!

Bunge ni la CCM; Serikali ni ya CCM; Vyombo vya HABARI vingi vinamilikiwa na wanaCCM na CCM ina vya kwake; Watanzania tulio wengi ni wanaCCM; Watafanya wanavyotaka.

Kwa vyovyote vile watakaangana kwa mafuta yao wenyewe!!
 
Kama kweli Diwani yupo ndani kwa kusema uwongo? Tunaomba DC, RC, IGP na Mawaziri wa Mambo ya Ndani, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Mazingira, Wajiuzuru ikiwa ni sehemu ya collective resposibility katika utendaji wa Serikali.
 
I think there might be a problem, watu wengi Tz wamekasirika tena sana lakini sasa kuna wengine wanaamini kutokupiga kura ndio kuwakomoa hawa wababe mafisadi wa CCM. ninawajua watu wawili ambao wameharibu kadi zao za kura eti kwa sababu wamekasirika na wengine wengi ambao wamesema hawatapoteza muda wao kupanga msitari na kupiga kura.

Tuhimizane jamani tena kwa makundi tukianza na wale walio karibu na sisi, kupiga kura ndio njia pekee itakayotusogeza angalau hatua chache kuelekea kwenye demokrasia ya kweli


Kwanza nikushukuru kwa hii post ( na nimeiquote)

Pili Hoja zangu.
Nimewasoma wote walionitangulia ni wengi sana. Ambao wanaona ni sawa au wanatetea ujinga wa spika ni watatu tu. Kelly01, Dilunga na Magret ambaye ni mgeni kabisa hapa. Nampongeza magret kwa kujiunga namshauri amweleze na ndugu yake ajiunge ili tuwe wengi hapa nadani ya forum.

Katika kusoma, nimefurahishwa na kitu kimoja nacho ni wengi wetu kulitambua tatizo la nchi yetu kuwa ilivyo ni CCM. Miaka arobaini majibu ni ya ovyo ovyo tu. Sielewi kuna kitu gani kinawaaminisha namna hiyo wabunge wa ccm na viongozi wao. Angalia majibu ya Naibu Waziri wa fedha kwa Dk Slaa juu ya meremeta, ukweli yanasikitisha kwa watu wanaopenda nchi yao.

Nashauri tuwe na Kauli mbiu Ifutayo, KATAA CCM, OKOA KIZAZI CHAKO.

Kila mtu apigie chama chochote kingine hata kama kina koti tu limetundikwa lakini siyo ccm, baada ya miaka mitano watashika adabu kabisa. Mimi naipenda CCM lakini mfumo wao wa kuyashughulikia matatizo yetu umenikatisha tamaa kabisa. Wale niliokuwa nawaamini kuwa watatusaidia hawafanyi chochote labda kwa sababu ya Mfumo ulivyo yaani Kamati kuu(CC), Halimashauri kuu (NEC) Kamati ya wabunge ya chama, Kamati ya maadili ya chama nk nk. Sasa hata ukiwa na jipya au dhamira safi utapita vipi vikwazo vyote hivyo?

Kataa ccm, okoa kizazi chako. Wote tuna watoto au tutakuwa na watoto na hivyo wajukuu na hivyo vitukuu na hivyo kizazi chako
 
Sitta anaendesha bunge kwa udikteta na anafanya watu kama watoto.Sijui huyu naye tulitoka naye wapi mpaka akawa spika bora ya msekwa
 
Nilikuwa naenda kulala kitandao nikaona mada hii , bora nichangie kabla sijasahau pengine kesho nikawa na ratiba ngumu kidogo za kufanya kazi

alichojaribu kutetea mh cheyo ni sahihi , tena wengine wale wabunge wanaotoka karibu na north mara walitakiwa ndio wawe wakwanza kutoa kilio chao bungeni , wanancho wa kule walitakiwa wawe wakwanza kutoa kilio chao hata kukifikisha katika vyombo vya kimataifa kwa matatizo yanayotokana na sehemu ile .

Wiki 2 zilizopita tuliona nchini nigeria kampuni ya shell imelipa watu fulani karibu dola mil 15 kwa hasara walizopata watu hao za kimazingira kutokana na utendaji wa kampuni ya shell walifikisha swala mahakamani na wakashinda kesi wakalipwa fidia kubwa sijui nchi yetu inajifunza nini kutokana na kile kinachoendelea

mfano mwingine ni ule wa nile delta huko huko nigeria wale waasi wa eneo lile wanapigania haki zao za kupata maendeleo pamoja na mazingira yanayoharibiwa kutokana na uzalishaji wa mafuta bila wao wazawa wa eneo lile kufaidika na chochote sasa hivi eneo lile ni kuwindana tu .

Juzi hapa tumesikia wapiganaji wa mau mau kenya wakienda kuishitaki serikali ya kikoloni kwa mambo waliyoyafanya miaka karibu 50 iliyopita , subiri tusikie kesi yao itakuwaje hata ikichukuwa miaka 100 wana nafasi kubwa zaidi ya kushinda .

……………………………………..

Kwa serikali ya tanzania na watanzania wanatakiwa wajue kuna mambo karibu 3 ya kuyaweka akilini kutokana na sakata hili sasa hivi .

1 ) mradi wa north mara ambao sumu yake unaingia katika ardhi pamoja na mito ya karibu na eneo hilo hili ni kesi tena kubwa – waziri anayeshugulikia afya na mazingira anatakiwa atoe ufafanuzi wa hili haraka

2 ) kuna viwanda vya bia na viwanda vingine vinavyomwaga maji ziwa viktoria , tunakumbuka maradi wa ziwa viktoria kupeleka maji mikoa jirani kama shinyanga --- yale maji yanayoingiwa ziwani yameathirika kwa kiasi kikubwa , bado watu wetu wananyweshwa na kupelekewa kwa kiasi kikubwa watu wanashangilia mradi wa maji bila kuangalia athari zake za muda mrefu .

Mimi naiona hii kuwa ni fursa kwa wanasheria wetu kuwatetea wazalendo wenzao ambao ni wanyonge kama ambavyo MEWATA wanawahangaikia akina mama wenye ugonjwa wa kansa ya matiti
 
Naomba clip ya hilo tukio kwa mwenye nayo tafadhali.
Sipendi kuamini kinachosemwa hapa. SITA\6\sIX\VI Noooo.
Huyu mzee anaupungufu wa kitu fulani kichwani mwake.May be presha za uchaguzi zinampanda na kumshuka.Wakati Cheyo anachangia labda zilikuwa zimempanada?
 
Poor cheyo, kwa kweli mie niliona kama kamuonea cheyo, aliichukua issue ile kama too personal, nadhani labla anakisirani tu na huyo cheyo, ukweli alichosema cheyo mi sikuona ubaya wake, ni kweli chemicals zingine zinadhuru papo kwa hapo lakini zingine sio, sasa alipotaka kuonyesha kuwa cheyo anajitia mtaalamu kumbe kweli ni mtaalamu, sasa sitta hataki hilo? halafu suala la udikteta wa wapinzani ulikujaje pale? halafu hata namna alivyomfukuza cheyo its as if anafukuza nguruwe alieingia msikitini, to me it wass real bad sikupenda kabisa, yaelekea yeye ndio analeta udikteta kuwa spika si kuwa yuko juu ya kila kitu, anyway C CM wanataka kutawala kila kitu, well we just wait & see what next!
 
Hivyo Ndugu zangu, Tutabaki tunandika kila siku na pia watu walichagua mafiga watu ndio faida yake
 
Huyu Sitta amefanya kinyume na matakwa ya Demokrasia, Hawa ni wababe sana

halafu spika anatetea uvundo tu kwa wanaoijua vizuri issue ya huko north mara, in fact kilichokuwa presented pale na waziri kimepambwa na siasa sana, ili tu kuwafunika funika wabunge na akili zao ndogo, lakini hali halisi ni mbaya kuliko wanavyoizungumzia pale na wataalamu wanalijua hilo. hao wataalamu wenyewe walioandika hiyo report ndo kwanza walienda eneo la tukio last thursday, before that ulikuwa utumbo tu unafanyika huko, halafu ukitaka kujua ile issue ni mbaya angalia Kagasheki alivyoona ile hali akaja juu, we unadhani cheyo alikuwa mjinga kusema yale, serikali ifanye kazi zake sawasawa,. enzi za kutishiana nyau watu wazima zimepitwa na wakati. hebu wajifunze kutawala watu sio udikteta wa kizama wa kumtishia mtoto kiboko, si enzi hizi, CCM waamke otherwise watakosa wateja soon
 
Maneno mengi hayavunji mfupa. Watanzania wamechoka na uongozi wa kiimla wa CCM. Shime wananchi, saidia kuondoa CCM madarakani 2010. Haya yote ni matokeo ya utawala mbovu wa chama cha mapinduzi.
 
Nashauri tuwe na Kauli mbiu Ifutayo, KATAA CCM, OKOA KIZAZI CHAKO.

Kila mtu apigie chama chochote kingine hata kama kina koti tu limetundikwa lakini siyo ccm, baada ya miaka mitano watashika adabu kabisa. Mimi naipenda CCM lakini mfumo wao wa kuyashughulikia matatizo yetu umenikatisha tamaa kabisa. Wale niliokuwa nawaamini kuwa watatusaidia hawafanyi chochote labda kwa sababu ya Mfumo ulivyo yaani Kamati kuu(CC), Halimashauri kuu (NEC) Kamati ya wabunge ya chama, Kamati ya maadili ya chama nk nk. Sasa hata ukiwa na jipya au dhamira safi utapita vipi vikwazo vyote hivyo?

Kataa ccm, okoa kizazi chako. Wote tuna watoto au tutakuwa na watoto na hivyo wajukuu na hivyo vitukuu na hivyo kizazi chako


Hapo umesema KATAA CCM OKOA KIZAZI KIJACHO iwe kauli yetu hakuna namna tutjikomboa hivi mulisikia ile sit down Kutoka kwa spika kwenda kwa Cheyo sikuamini maskio yangu
 
Hivi jamaani nikumbusheni kauli ya SITTA na Kirefu chake kama Spika wa Viwango labda ndio viwango vyake
 
Kwanza nikushukuru kwa hii post ( na nimeiquote)

Pili Hoja zangu.
Nimewasoma wote walionitangulia ni wengi sana. Ambao wanaona ni sawa au wanatetea ujinga wa spika ni watatu tu. Kelly01, Dilunga na Magret ambaye ni mgeni kabisa hapa. Nampongeza magret kwa kujiunga namshauri amweleze na ndugu yake ajiunge ili tuwe wengi hapa nadani ya forum.

Join Date: Thu May 2009
Posts: 15
Thanks: 2
Thanked 3 Times in 3 Posts
Rep Power: 0
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

Credits: 31,690

Wewe je?
 
Sitta amuombe radhi Mzee Cheyo,
Hata kama yuko upinzani si matamshi ya utashi na heshima kumwambia mtu mzima kama Cheyo ''Go Out'' ! ni dharau, ni ufinyu wa fikra mbadala, ni kuwa juu ya ubinadamu wa kuheshimiana na kusikiliza mawazo ya mwingine! Kwa nafasi aliyonayo hakustahili kufanya aliyofanya na najua ANAJUTIA kwa uovyo wa alichokisema.
Hata kama Cheyo alikosea Mzee sitta kwa uelewa wako na kwa kiti cha Spika ambacho najua hakiongei wala hakijui ila ni wewe unayekiratibu na kwa jinsi hiyo unajisemea wewe mwenyewe kuwa amekukosea basi ungemstahi mwenzako kuliko ulivyomdharau.
Wewe ni Mkristo, basi tafuta nafasi humohumo bungeni,muombe radhi Mzee mwenzako, Mwambie na Mama makinda aache jaziba na asikisingizie Kiti cha spika atakiacha hapo bungeni yeye tutakutana huku duniani atakuwa mtupu hana Kiti wala kinga atapambana na hoja Mbadala zitambadilisha.
Nanina wasiwasi kwa speed hiyo basi standard yako imepata mkengeuko wa kifkra na
utashi wa kujua wakati wa kukimbia na wakati wa kutembea,wakati wa kuwa makini na wakati wa kuachia upepo upite, yatafakari hayo.Asante,
Jirudi na Mungu atakuinua tena.
Mithali 24:16; ''Kwa maana mwenye Haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio Haki hukwazwa na Mabaya''
Jone,Ndikupasya Buno Malafyale anganie kangi ambokie.
Ndaga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom