Simba v/s Azam fc, Yanga v/s Oljoro JKT Live updates

Jamani tumeongoza ligi toka
mechi ya kwanza hadi sasa mechi ya kumi tunaongoza, jueni kwamba
kuongoza ligi sio kazi rahisi hadi uwe unajua, sio kusubiri mabeki
wafunge magoli ya faulo na washambuliaji wafunge magoli ya penati halafu
unataka uongoze ligi, subiri kidogo jamani sasa ni wakati wetu kujidai
hapo juu, huku kwingine mtakuwa mnabadilishana, chezeya mnyama wewe
utalala hoi!!!

Umeona eeh! Yebo yebo ndio amefikia peak hapo asubiri kurudi wa3 na kushuka chini,akikaza sana atabaki hapo 2.
 
Inabidi katiba mpya iwafute maana haiwezekani watu wanapata pt za chee namna hii.
Tatizo la Yanga ni kutaka kubebwa na matokeo ya timu nyingine. Walidhani Azam atashinda ili na wao wasogee. Dua la kuku halimpati mwewe, na ndiyo maana wanalalama matokeo yamepangwa kwani ikiwa matokeo yatabaki hivyo hali yao itabaki ilivyo. Kwa taarifa yenu Simba wameshafanya marekebisho na tokea sasa kila atakayejipendekeza ni kipigo tu.
 
Usitake kuleta uongo, Nuhu Haji ni beki tegemeo wa Azam na kacheza mechi nyingi.

huyu haji alicheza na lyon kala red na kitu kinachokera siku ile wanacheza na yanga wamekipiga kweli ila hapa leo easy goals zote wamechezea kama sio mipango nini simba na wao sijaona kabisa kukaza leo gemu imeuza na uchawi juu ngoja ntakuwekea picha ya uwanjani mkuu Masuke wameniboa balaa
 
Last edited by a moderator:
Matokeo ni vipi arusha?

Watu wa Mara utawajua tu! Yaani wewe matokeo yameshawekwa zaidi ya mara tano hujayaona tu??? Au ndio ulikuwa unamng'oa meno mkeo kwa ngumi (ili aamini kuwa unampenda) wakati watu wanatuma matokeo hapa!
 
hawa Azam hawana tofauti na Kariakoo Lindi au mji mpwapwa...
Kelele nyiiiiiingi lakini uwanjani mavi matupu.
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Pamoja na ukweli kwamba simba imeshinda kwasababu ya mipango ya nje ya uwanja, uhakika nilionao ni kwamba akisha maliza game za TOTO AFRICANS na PRISONS tutakuwa tunawatafuta katika tatu bora kwa mbinde.

Mmmiliki wa Azam amekubali kuinusuru timu yake ya simba isishushwe kileleni kwakuwa Azam bado ana game moja mkononi.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Tatizo la Yanga ni kutaka kubebwa na matokeo ya timu nyingine. Walidhani Azam atashinda ili na wao wasogee. Dua la kuku halimpati mwewe, na ndiyo maana wanalalama matokeo yamepangwa kwani ikiwa matokeo yatabaki hivyo hali yao itabaki ilivyo. Kwa taarifa yenu Simba wameshafanya marekebisho na tokea sasa kila atakayejipendekeza ni kipigo tu.
Anhaa,kumbe mmechezea dar!
 
Umeona eeh! Yebo yebo ndio amefikia peak hapo asubiri kurudi wa3 na kushuka chini,akikaza sana atabaki hapo 2.

nyie nao! Ushind wa mezani tu shida, mngeshinda magoli ya muvu si ndo mngekunya kabisa!!??
 
Pamoja na ukweli kwamba simba imeshinda kwasababu ya mipango ya nje ya uwanja, uhakika nilionao ni kwamba akisha maliza game za TOTO AFRICANS na PRISONS tutakuwa tunawatafuta katika tatu bora kwa mbinde.

Mmmiliki wa Azam amekubali kuinusuru timu yake ya simba isishushwe kileleni kwakuwa Azam bado ana game moja mkononi.

Katika siku zote leo ndiyo nimeona umeingia chaka, nilikuwepo stadium uwezo wa Azam umekomea hapo hawakuwa na jinsi tena.
 
huyu haji alicheza na lyon kala red na kitu kinachokera siku ile wanacheza na yanga wamekipiga kweli ila hapa leo easy goals zote wamechezea kama sio mipango nini simba na wao sijaona kabisa kukaza leo gemu imeuza na uchawi juu ngoja ntakuwekea picha ya uwanjani mkuu Masuke wameniboa balaa
Mkuu mimi mwenyewe nilikuwepo uwanjani, Azam wamezidiwa soka na wala msitake kuleta maneno hapa mara uchawi, mara mechi imeuzwa, hapakuwa na easy goal hata moja, Sunzu kafunga magoli ya kichwa mengi na ndo alichofanya leo, baada ya siku chache utaona clip kwenye you tube jinsi magoli yalivyokuwa ya move, Azam leo hawakucheza vizuri hasa kipindi cha kwanza na dakika 30 za kipindi cha pili, dak 15 za mwisho kipindi cha pili kidogo walijitahidi hasa baada ya kuingia Kipre Balou kidogo aliimarisha kiungo na sisi baada ya Sunzu kutoka mabeki wa Azam wakawa free kupanda, lakini kiukweli tuliwazidi sana Azam.
 
huwa hawachezi hivi mi nakumbia subiri wakutana yanga au timu zingine nadhani utaamini ninachosema na sio kuwa walizidiwa maana mtu hataki kukaba wanatoa pasi za kusakizia ndio maana wakaniboa kinoma na unazi ndio utafanya hii vpl hatutakaa tuichukue..
 
Katika siku zote leo ndiyo nimeona umeingia chaka, nilikuwepo stadium uwezo wa Azam umekomea hapo hawakuwa na jinsi tena.

mkuu mzee wa rula mpaka sasa najiuliza hivi kule kagera tuliwafungaje hawa kagera wababe wa simba na yanga maana kuna vitu vingine inabidi mtu ufikirie sana na hapo subiri siku na yanga ndio utajua azam ina vichembechembe vya simba na yanga..
 
huwa hawachezi hivi mi nakumbia subiri wakutana yanga au timu zingine nadhani utaamini ninachosema na sio kuwa walizidiwa maana mtu hataki kukaba wanatoa pasi za kusakizia ndio maana wakaniboa kinoma na unazi ndio utafanya hii vpl hatutakaa tuichukue..
Mkuu uwezo wa Azam uliishia hapo, unaweza ukasema wanatoa pasi za kusakizia lakini unachotakiwa kujua ni kwamba mpira una njia zake na kama sio hujacheza hata Chandimu huwezi kuziona hizo njia, Simba waliblock njia za pasi za Azam, kumbuka tulikuwa na holding midfielders wawili Mkude na Kiemba, tulikuwa na Kazimoto na Sunzu ambao nao wanakaba na bado Okwi na Ngasa walikuwa wanashuka kusaidia full back wakati Azam wanashambulia, mwaka Azam wasipokuwa makini watafanya vibaya kwa sababu wamewekeza kwa washambuliaji wawili tu Bocco na Kipre Tchetche, Bocco kwa sasa ni mgonjwa hata jana alilazimika kuchezeshwa lakini hakuwa fiti ndo yale yale ya Brazil na Ronaldo mwaka 1998 fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ufaransa, unashangaa kufungwa na Simba lakini hushangai Ruvu Shooting ilivyowatoa jasho.
 
Back
Top Bottom