FT: Simba 2-0 Yanga | NBC PL | Benjamin Mkapa Stadium | 16.04.2023

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,722
45,128
Mwanamuziki nguli wa Bongofleva, Lady Jay Dee aliwahi kuimba kibao maarufu " Siku hazigandi " alikuwa sahihi. Lile pambano lililokuwa linasubiriwa kwa hamu hatimae ndio linapigwa leo, ama kweli siku hazigandi.

Ndio ni Kariakoo Derby, ni Simba Sc Vs Yanga Sc katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam saa 11:00 jioni.

Mnyama mkubwa mwituni, Simba Sc itakuwa inawaalika wapinzani wao wa jadi Yanga, huku ikijaribu kupunguza pengo la point baina ya timu hizo mbili.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na alama 68 huku Simba ikiwa na alama 60 hivyo kufanya tofauti kuwa alama 8 huku zikisalia mechi 5 kabla ya msimu kuisha.

Simba itashuka dimbani kujaribu kutafuta ushindi wake wa kwanza tangu ilivyofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2019. Ni mechi saba sasa Simba hajamfunga Yanga katika Ligi Kuu ya NBC.

Mechi ya mwisho walipokutana wababe hao, matokeo yalikuwa 1-1 kwa magoli ya Augustine Okrah kwa Simba na Aziz Ki kwa upande wa Yanga.

Simba itashuka dimbani huku ikimtegemea zaidi mshambuliaji wake aliyefomu , Jean Baleke ambaye kwasasa hakamatiki kwa fomu yake huku akina Chama, Ntibazonkiza na Mzamiru wakitegemewa kuleta chachu ya ushindi.

Kwa upande wa Yanga, watamtegemea zaidi Straika wao ambaye fomu yake imekuwa ikipanda na kushuka Fiston Kalala Mayele huku pia Aziz Ki na akina Jesus Moloko wakitegemewa kunogesha zaidi.

Je, Simba atakubali kuendelea kuwa mnyonge kwa Yanga?
Na vipi upande wa pili, ubingwa bila kumfunga mtani unaweza kunoga?

Mwamuzi wa mtanange huo ni mwanamama, Jonesia Rukya akisaidiwa na akina Janeth Balama pamoja na Mohamed Mkono.

Mechi ni saa 11:00 jioni na itakuwa live Azam Sports 1HD

Kwa live updates, utani wa hapa na pale na yote yanayohusu mechi hii basi hapa ndio sehemu sahihi kwako Mwana JF...

Simba.jpg

Kikosi cha Simba
Yanga.jpg

Kikosi cha Yanga
Timu zinaingia uwanjani
Mchezo umeanza
2' Goooooooooooooooooooo
Inonga anafunga goli kwa kichwa baada ya walinzi wa Yanga kuzubaa
5' Mchezo una kasi, Yanga wanajipanga kutafuta goli la kusawazisha
10' Mvua imeanza kunyesha uwanjani
18’ Mchezo umesimama kwa muda Inonga ameumia baada ya kugongana na Musonda
22' Mchezo unaendelea, ufundi umepungua kiasi kutokana na mvua
29’ Shuti la Baleke linagonga nguzo baada ya kupewa pasi nzuri na Chama
29’ Kibu Denis anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo
31’ Yanga wanapata kona ya 3
32’ GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Kibu Denis anafunga goli la pili kwa shuti kali
43' Baleke anakosa nafasi nyingine ya wazi akipokea pasi ya Chama
45' Zinaongezwa dakika 2

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza
45' Mabadiliko kwa Yanga, ametoka Sure Boy ameingia Azizi Ki
Ametoka Yaniki Bangala ameingia Mudathiri Yahya
Ametoka Moloko ameingia Tuisila Kisinda
47' Mayele yupo chini ameumia
56’ Djuma Shaban anapewa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Saido
65’ Mchezo umesimama kwa muda ili kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji kufturu
67’ Mchezo unaendelea
69’ Azizi Ki almanusura afunge, shuti linatoka nje kidogo ya lango
70’ Mabadiliko kwa Yanga, anatoka Musonda anaingia Bernard Morrison
74' Mabadiliko kwa Simba, anatoka Erasto Nyoni anaingia Kapama
82' Simba wanamtoa Baleke anaingia John Bocco
90' Zinaongezwa dakika 5

Full Time
 
#𝐍𝐢𝐒𝐮𝐚𝐥𝐚𝐋𝐚𝐌𝐮𝐝𝐚𝐓𝐮
#𝐊𝐚𝐫𝐢𝐚𝐤𝐨𝐨𝐃𝐞𝐫𝐛𝐲 🤍 𝐯𝐬
#𝐍𝐛𝐜𝐏𝐫𝐞𝐦𝐢𝐞𝐫𝐋𝐞𝐚𝐠𝐮𝐞

𝐇𝐚𝐭𝐢𝐦𝐚𝐞 𝐬𝐢𝐤𝐮 𝐢𝐥𝐢𝐲𝐨𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐢𝐤𝐢𝐬𝐮𝐛𝐢𝐫𝐢𝐰𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐡𝐚𝐦𝐮 𝐢𝐦𝐞𝐟𝐢𝐤𝐚, 𝐧𝐢 𝐬𝐢𝐤𝐮 𝐲𝐚 "𝐓𝐚𝐦𝐚𝐬𝐡𝐚 𝐋𝐚 𝐭𝐚𝐢𝐟𝐚" 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐩𝐨 𝐧𝐢 𝐦𝐩𝐚𝐦𝐛𝐚𝐧𝐨 𝐰𝐚 𝐦𝐚𝐫𝐮𝐝𝐢𝐚𝐧𝐨 𝐤𝐚𝐭𝐢 𝐲𝐚 𝐒𝐢𝐦𝐛𝐚 𝐧𝐚 𝐘𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐦𝐬𝐢𝐦𝐮 𝐰𝐚 𝐋𝐢𝐠𝐢 𝐤𝐮𝐮 𝐲𝐚 𝐍𝐁𝐂 2022/2023..

𝐊𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐦𝐜𝐡𝐞𝐳𝐨 𝐰𝐚 𝐋𝐞𝐨 𝐒𝐢𝐦𝐛𝐚 𝐧𝐢 𝐦𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞𝐣𝐢(𝐇𝐨𝐦𝐞) 𝐧𝐚 𝐘𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐚𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐧𝐢 𝐌𝐠𝐞𝐧𝐢 (𝐀𝐰𝐚𝐲).. 𝐍𝐢 𝐦𝐜𝐡𝐞𝐳𝐨 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐨 𝐘𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐚 𝐏𝐨𝐢𝐧𝐭 68 𝐇𝐮𝐤𝐮 𝐒𝐢𝐦𝐛𝐚 𝐚𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐏𝐨𝐢𝐧𝐭 60 𝐘𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐚𝐧𝐚𝐨𝐧𝐠𝐨𝐳𝐚 𝐥𝐢𝐠𝐢 𝐤𝐰𝐚 𝐭𝐨𝐟𝐚𝐮𝐭𝐢 𝐲𝐚 𝐩𝐨𝐢𝐧𝐭 8 𝐝𝐡𝐢𝐝𝐢 𝐲𝐚 𝐦𝐭𝐚𝐧𝐢 𝐰𝐚𝐤𝐞.. (𝐍𝐢 𝐦𝐞𝐜𝐡𝐢 𝐲𝐚 26 𝐤𝐰𝐚 𝐘𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐧𝐚 𝐒𝐢𝐦𝐛𝐚, 𝐡𝐮𝐤𝐮 𝐥𝐢𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐧𝐢 𝐩𝐚𝐦𝐛𝐚𝐧𝐨 𝐥𝐚 110 𝐭𝐚𝐧𝐠𝐮 𝐋𝐢𝐠𝐢 𝐲𝐚 𝐁𝐚𝐫𝐚 𝐢𝐥𝐢𝐩𝐨𝐚𝐬𝐢𝐬𝐢𝐰𝐚 𝐦𝐰𝐚𝐤𝐚 1965) 𝐌𝐞𝐜𝐡𝐢 𝐡𝐢𝐢 𝐘𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐚𝐧𝐚𝐭𝐚𝐤𝐚 𝐚𝐰𝐞𝐤𝐞 𝐡𝐢𝐬𝐭𝐨𝐫𝐢𝐚 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐦𝐟𝐮𝐧𝐠𝐚 𝐦𝐭𝐚𝐧𝐢 𝐧𝐚 𝐤𝐮𝐛𝐞𝐛𝐚 𝐮𝐛𝐢𝐧𝐠𝐰𝐚 𝐡𝐮𝐤𝐮 𝐒𝐢𝐦𝐛𝐚 𝐚𝐤𝐢𝐭𝐚𝐤𝐚 𝐡𝐞𝐬𝐡𝐢𝐦𝐚

𝐌𝐞𝐜𝐡𝐢 𝐲𝐚 𝐤𝐰𝐚𝐧𝐳𝐚 𝐲𝐚 𝐦𝐬𝐢𝐦𝐮 𝐡𝐮𝐮 𝐛𝐚𝐢𝐧𝐚 𝐲𝐚𝐨 𝐢𝐥𝐢𝐜𝐡𝐞𝐳𝐰𝐚 𝐦𝐧𝐚𝐦𝐨 𝐎𝐤𝐭𝐨𝐛𝐚 23, 2022 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐩𝐨 𝐌𝐚𝐡𝐚𝐬𝐢𝐦𝐮 𝐡𝐚𝐰𝐚 𝐰𝐚𝐥𝐢𝐠𝐚𝐰𝐚𝐧𝐚 𝐚𝐥𝐚𝐦𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐭𝐨𝐤𝐚 1-1...

Timu hizo zinakutana zikiwa zimetoka kupata matokeo chanya kwenye mechi zilizopita za ligi, Yanga ikiifumua Kagera Sugar kwa mabao 5-0, wakati Simba ikishinda 2-0 dhidi ya Ihefu.

𝐏𝐚𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐧𝐚 𝐡𝐚𝐲𝐨 𝐛𝐚𝐝𝐨 𝐢𝐭𝐚𝐛𝐚𝐤𝐢𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐦𝐞𝐜𝐡𝐢 𝐧𝐠𝐮𝐦𝐮 "𝐢𝐬𝐢𝐲𝐨𝐭𝐚𝐛𝐢𝐫𝐢𝐤𝐚" 𝐤𝐰𝐚 𝐩𝐚𝐧𝐝𝐞 𝐳𝐨𝐭𝐞 𝐡𝐚𝐬𝐚 𝐮𝐤𝐢𝐳𝐢𝐧𝐠𝐚𝐭𝐢𝐚 𝐮𝐢𝐦𝐚𝐫𝐚 𝐰𝐚 𝐯𝐢𝐤𝐨𝐬𝐢 𝐯𝐲𝐚𝐨 𝐛𝐢𝐥𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐚𝐡𝐚𝐮 𝐦𝐛𝐢𝐧𝐮 𝐳𝐚 𝐤𝐢𝐮𝐟𝐮𝐧𝐝𝐢 𝐤𝐮𝐭𝐨𝐤𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐚𝐤𝐨𝐜𝐡𝐚 𝐰𝐚𝐨 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐤𝐮𝐣𝐢𝐰𝐞𝐤𝐞𝐚 𝐦𝐚𝐳𝐢𝐧𝐠𝐢𝐫𝐚 𝐦𝐚𝐳𝐮𝐫𝐢 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐭𝐰𝐚𝐚 𝐮𝐛𝐢𝐧𝐠𝐰𝐚 𝐦𝐬𝐢𝐦𝐮 𝐡𝐮𝐮

WAAMUZI

Mechi hiyo ya marudiano ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu wa 2022/2023 inatarajiwa kuchezwa kuanzia Saa 11:00 jioni na Katikati atasimama Mwanamama Jonesia Rukya atasaidiwa na washika vibendera Mohamed Mkono wa Tanga na Janeth Balama wa Iringa, huku Mwamuzi wa akiba akiwa ni Tatu Malogo.

𝐉𝐞, 𝐥𝐞𝐨 𝐧𝐢𝐧𝐢 𝐤𝐢𝐭𝐚𝐭𝐨𝐤𝐞𝐚 𝐛𝐚𝐢𝐧𝐚 𝐲𝐚 𝐦𝐢𝐚𝐦𝐛𝐚 𝐡𝐢𝐢 𝐦𝐢𝐰𝐢𝐥𝐢, 𝐅𝐮𝐚𝐭𝐢𝐥𝐢𝐚 𝐡𝐚𝐩𝐚 𝐦𝐮𝐛𝐚𝐬𝐡𝐚𝐫𝐚 𝐮𝐣𝐮𝐞 𝐤𝐢𝐧𝐚𝐜𝐡𝐨𝐣𝐢𝐫𝐢 𝐤𝐮𝐭𝐨𝐤𝐞𝐚 𝐡𝐚𝐩𝐚 "𝐄𝐬𝐭𝐚𝐝𝐢𝐨 𝐃𝐞 𝐁𝐞𝐧𝐣𝐚𝐦𝐢𝐧 𝐌𝐤𝐚𝐩𝐚"

𝐊𝐰𝐚 𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐯𝐢𝐬𝐢𝐦𝐛𝐮𝐳𝐢 𝐀𝐳𝐚𝐦 𝐒𝐩𝐨𝐫𝐭𝐬 1 𝐇𝐃 𝐰𝐚𝐭𝐚𝐮𝐫𝐮𝐬𝐡𝐚 𝐦𝐩𝐚𝐦𝐛𝐚𝐧𝐨 𝐡𝐮𝐮 𝐥𝐢𝐯𝐞 "𝐤𝐢𝐝𝐞𝐨𝐧𝐢" 𝐧𝐚 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 "𝐬𝐢𝐦𝐮 𝐣𝐚𝐧𝐣𝐚"

𝐍𝐁: 𝐊𝐮𝐛𝐞𝐛𝐚 𝐮𝐛𝐢𝐧𝐠𝐰𝐚 𝐛𝐢𝐥𝐚 𝐤𝐮𝐦𝐟𝐮𝐧𝐠𝐚 𝐦𝐭𝐚𝐧𝐢 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐬𝐞𝐦𝐚𝐠𝐚 𝐡𝐚𝐢𝐧𝐨𝐠𝐢

_______________________________

Simba SC Kocha : Robert Oliviera "Robertinho"
Kocha Msaidizi Juma Mgunda "Guardiola Mnene"

Yanga SC Kocha Mkuu: Nasredeen Nabi "Professor"

Kocha Msaidizi : Cedric Kaze
 
Mwanamuziki nguli wa Bongofleva, Lady Jay Dee aliwahi kuimba kibao maarufu " Siku hazigandi " alikuwa sahihi. Lile pambano lililokuwa linasubiriwa kwa hamu hatimae ndio linapigwa leo, ama kweli siku hazigandi.

Ndio ni Kariakoo Derby, ni Simba Sc Vs Yanga Sc katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam saa 11:00 jioni.

Mnyama mkubwa mwituni, Simba Sc itakuwa inawaalika wapinzani wao wa jadi Yanga, huku ikijaribu kupunguza pengo la point baina ya timu hizo mbili.

Yanga inaongoza kwa tofauti ya alama 8 huku zikisalia mechi 5 kabla ya msimu kuisha.

Simba itashuka dimbani kujaribu kutafuta ushindi wake wa kwanza tangu ilivyofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2019. Ni mechi saba sasa Simba hajamfunga Yanga katika Ligi Kuu ya NBC.

Mechi ya mwisho walipokutana wababe hao, matokeo yalikuwa 1-1 kwa magoli ya Augustine Okrah kwa Simba na Aziz Ki kwa upande wa Yanga.

Simba itashuka dimbani huku ikimtegemea zaidi mshambuliaji wake aliyefomu , Jean Baleke ambaye kwasasa hakamatiki kwa fomu yake huku akina Chama, Ntibazonkiza na Mzamiru wakitegemewa kuleta chachu ya ushindi.

Kwa upande wa Yanga, watamtegemea zaidi Straika wao ambaye fomu yake imekuwa ikipanda na kushuka Fiston Kalala Mayele huku pia Aziz Ki na akina Jesus Moloko wakitegemewa kunogesha zaidi.

Je, Simba atakubali kuendelea kuwa mnyonge kwa Yanga?
Na vipi upande wa pili, ubingwa bila kumfunga mtani unaweza kunoga?

Mwamuzi wa mtanange huo ni mwanamama, Jonesia Rukya akisaidiwa na akina Janeth Balama pamoja na Mohamed Mkono.

Mechi ni saa 11:00 jioni na itakuwa live Azam Sports 1HD

Kwa live updates, utani wa hapa na pale na yote yanayohusu mechi hii basi hapa ndio sehemu sahihi kwako Mwana JF...
Simba ipo kata ya kariakoo yanga ipo kata ya jangwani!
 
No, imetokea wote tumepost muda mmoja kutokana na uzito wa game husika. Mods wataunga utabaki uzi mmoja nao tutatembea nao tu kibingwa
𝐔𝐳𝐢 𝐰𝐨𝐰𝐨𝐭𝐞 𝐮𝐭𝐚𝐤𝐚𝐨𝐩𝐢𝐭𝐢𝐬𝐡𝐰𝐚 𝐬𝐢𝐬𝐢 𝐭𝐮𝐭𝐚𝐭𝐞𝐦𝐛𝐞𝐚 𝐧𝐚𝐨 𝐭𝐮, 𝐡𝐚𝐢𝐧𝐚 𝐦𝐛𝐚𝐲𝐚
 
Back
Top Bottom