Simba v/s Azam fc, Yanga v/s Oljoro JKT Live updates

Jana Azam wamezingua sanaaaa. Simba ni timu ya kawaida, Tatizo wachezaji wa AZAM walikua hawachezi mpira wa kazi. walileta Mahaba uwanjani. Kwa mpira ule hata yanga wanaweza wakatufunga Mechi ya jmos. Yule HUMUD alikua anarukaruka tu uwanjani nashangaa kocha alivyomwacha dk 90 zote. Azam tunawapenda but wapunguze Upemba.
Tumia akili angalauu kidogo hivi kati ya Simba na Azam Fc ipi timu ya kawaida sana kuliko nyenzake mfano Azam FC ilicheza na SIMBA B tukawafunga sasa leo kufungwa na timu ya wakubwa mnalilia lia nini kama yanga tuna wafunga goli tano wana singizia mgogoro sasa subiri mzunguko wa piri timu wepo kamili na msifanye mipango kama mlivyofanya raound ya kwanza muone kama hamtachezea mkono mafala nyie..kazi kuia lia tuo simba ya kawaida yakawada wakati inaongoza lingi na ndiyo bingwa mtetezi huku azam akiwa amekula tatu na yanga 6 -1...
 
Didier Kavumbangu ndio anaongoza kwa magoli pale Yanga akifuatiwa na Twite,kiwango cha Twite kweli Rage alistahili kutoa machozi
Ni mchezaji wa kawaida sana, kama ulibahatika kuona kitu alichofanywa na na mshambuliaji wa kagera kisha akaenda kufunga utakubaliana na mimi kuwa wachezaji wa kigeni tuna wakuza kwenye magazetu lakini ni wakawatu..Mchezaji ni okwi na Niyonzima wa msimu uliopita siyo huyu wa msimu huu..
 
Ni mchezaji wa kawaida sana, kama ulibahatika kuona kitu alichofanywa na na mshambuliaji wa kagera kisha akaenda kufunga utakubaliana na mimi kuwa wachezaji wa kigeni tuna wakuza kwenye magazetu lakini ni wakawatu..Mchezaji ni okwi na Niyonzima wa msimu uliopita siyo huyu wa msimu huu..

nakuunga mkono,okwi na niyonzima angalau wanaonekana ni wachezaji wa kimataifa,hawa wengine sunzu na huyu twite mm siwaelewi wanachokifanya uwanjani ni misifa tu waongo tumewajaza,
 
Labda Okwi na Niyonzima wa msimu uliopita but kwa msimu huu Twite ni mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri.Twite anamudu zaidi nafasi ya beki wa kati kuliko kuliko kulia alikokuwa anachezeshwa mwanzo tangu Yondani ameumia ameonyesha uwezo mkubwa na kikubwa zaidi anafunga magoli
 
kama mpira ni mahesabu mkuu mpaka sasa nishaanza kuwa na wasiwasi pindi tunacheza na simba maana wanacheza chini ya kiwango kabisa na sijui kule kagera tulishinda vipi toto walitutoa kamasi baada ya kumueka dida na kuwadharau sasa kwa gemu ya jana ndio gemu iliyo niboa kuliko zote na isitoshe kwa mwendo ule azam tutasubiri sana kutoka..
Mimi sijasema mpira ni mahesabu nilichosema ni kwamba mpira sio hesabu za kujumlisha na kutoa, acheni kulaumu wachezaji, Azam hawana mfungaji kwa sasa zaidi ya Bocco na Kipre Tchetche na Bocco mwenyewe alikuwa mgonjwa; kumbuka msimu uliopita mlikuwa na Mrisho Ngasa, mmemtoa Ngasa hakuna mbadala wake.
 
Mimi sijasema mpira ni mahesabu nilichosema ni kwamba mpira sio hesabu za kujumlisha na kutoa, acheni kulaumu wachezaji, Azam hawana mfungaji kwa sasa zaidi ya Bocco na Kipre Tchetche na Bocco mwenyewe alikuwa mgonjwa; kumbuka msimu uliopita mlikuwa na Mrisho Ngasa, mmemtoa Ngasa hakuna mbadala wake.

na imani hili litawaumiza sana mpka watakapo jua nini maana ya unazi maandazi..
 
Hata mimi nilikuwepo uwanjani jana kushuhudia live simba na azam,nimejuta kupoteza pesa yangu kuingia uwanjani,tulitegemea kuona gemu la ushindani lakini kilichotokea ni bora simba angecheza na polisi moro walau tungeona soka safi,kusema ukweli azam waliuza gemu mana walikuwa wanacheza kama hawataki au kama wameshinda wao vile,mashabiki wengi walianza kuondoka uwanjani mapema sababu mpira ulikuwa haufurahishi kiukweli,subiri yanga na azam ndo utawajua azam ni tawi la simba mana wanageuka wanakuwa mbogo,

Watu kama ni ninyi ndio ambao mtaendelea kudumaza mpira wa nchi kwa kuwa na mawazo yasiyokuwa na tija. Hakuna kuuza wala kununua kwenye mechi hii, na matokeo yalikuwa ni reflection ya hali halisi ya mpira. Azam wakon ktk kipindi cha mpito baada ya kubadilisha kocha wenye falsafa na mifumo tofauti ya ufundishaji. Pia wanakabiliwa na wimbi la majeruhi kwa wachezaji wao tegemeo.

Isitoshe, Simba ktk kiwango chake, ni timu bora na wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu, mfano goli la tatu lililofungwa na Okwi ni la kiwango cha juu, na hakuna aliyelitarajia. Kinachoiponza Azam kwa Simba ni kucheza mchezo unaofanana na wa nafasi, kitu ambacho kwa sasa Simba ni wazuri zaidi baada ya Azam kubadilisha kocha.

Ubora Simba unajidhihirisha kwa njia nyingi tu, ikiwemo rekodi ya kutokufungwa hadi sasa, kufunga magoli mengi, n.k.
Ni vizuri pamoja na ushabiki wetu, kidogo tuwe tunaaangalia mpira kwa macho matatu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom