Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Kocha wa Yanga Nabi Nasreddine amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya shilingi 500,000 (laki tano) na TPLB kwa kosa la kuwashambulia kwa maneno mwamuzi wa kati na mwamuzi wa akiba kwenye mchezo ambao Yanga walipigwa 2-1 dhidi ya Ihefu FC.
Kamati ya usimamizi wa Ligi Kuu TPLB imeitoza Klabu ya Simba Shilingi 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la baadhi ya wachezaji wake kuingia uwanjani kwa kupitia milango isiyokuwa rasmi kwenye mchezo ambao Simba SC walitoka sare ya moja kwa moja dhidi ya Mbeya City.
Mchezaji Gadiel Michael amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya shilingi 500,000 (laki tano) na TPLB kwa kosa la kulazimisha kuingia uwanjani saa 4: 25 asubuhi kwa kile alichoeleza alitaka kukagua Uwanja kuelekea mchezo wa Mbeya City dhidi Simba SC.