Siasa ni Hesabu. Anayebisha Amuangalie Lowassa Halafu Awaulize Sitta na Nnape

aisee huyu ndio lowasa kama uzi ulivyosema, yaani ana mahesabu makali ya kisiasa, hata hii JF kashaipigia mahesabu kisiasa na ndio maana thread zake haziishi humu ndani.
Acha kutishatisha watu humu. Huyo Lowassa ni wakawaida sana wala hana lolote la maana.
Hawa wapambe wake humu JF wakiongozwa na Pasco ni waganga njaa wanaojipendekeza kwake ili awape ulaji tu.
 
uko sawa, ndani ya CCM EL hawezekaniki,,,,yeye hata akiteuliwa tu kugombea urais kupitia CCM huo ni ushindi kwake dhidi ya wabaya wake kama mzee six....hata CHADEMA wangependa sana EL ateuliwe,,,ni rahisi ku - compete na yeye na kumshinda...

Hata hivyo naamini kwa sasa Tanzania inahitaji COMPLETE REFORM
 
Umesema vema, ile tu EL kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM 2015 itakuwa ni bonge ya ushindi kwake dhidi ya maadui zake akina Six shida ni kwamba he cannot stand strong with CHADEMA wind....

Kwa sasa wananchi ni kama wanasubiri kuhalalisha utawala wa CHADEMA,,,,naamini inahitajika COMPLETE OVERHAUL of the Political System
 
Wadau,

Nianze kwa kuomba radhi kwa wanaJF wenye allergy na EDWARD N. LOWASSA. Najua wapo wadau wengi humu jamvini ambao wakisikia LOWASSA wanakumbuka UFISADI na wakitamka UFISADI wanakumbuka LOWASSA. Watu waliopo kwenye kundi hili, ndiyo ninaowaomba radhi. Wanisamehe sana maana sidhani kama kuna namna unayoweza kuzungumzia siasa za kisasa za Tanzania bila kumgusa LOWASSA.

Katika vipindi vyote au wengine wanavyoita awamu zote za uongozi wa nchi yetu tangu uhuru, hakuna wakati ambapo wananchi tumeshuhudia siasa ikitamalaki kama wakati huu. Mazingira ya sasa nchini kisiasa pengine ni magumu kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Hivi sasa, kila mwanachama w chama fulani na hata raia tu asiye na chama anajisikia kuwa anaweza kuwa rais wa Tanzania. Hali hii ni tofauti na zamani na hii inaweza kuwa imetokana na namna nchi inavyoongozwa kiholela kwa kiwango kisichoweza kutarajiwa. Kwa wanaJF wenye umri wangu, hivi ni wana-ccm gani enzi za Mwl. Nyerere ambao angalau hata walifikiria wakati huo kurithi mikoba ya uongozi kutoka kwa Nyerere? Bila shaka, walikuwa wachache sana na sidhani kama walikuwa wanajionesha waziwazi. Wapo wanaJF wanaoweza kuiongelea hali hii kwa mtazamo hasi kwamba Nyerere alikuwa kiongozi wa kiimra na kwamba hakujenga "mazingira rafiki" ya wanachama kujisikia huru kutangaza nia yao ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha urais. Mtazamo huo unaweza kuwa na ukweli to some extent lakini upande chanya pia unaweza kuwepo kwamba baadhi ya wanachama ulipofika wakati wa uchaguzi walijitazama kwa undani na kujilinganisha na Mwl. Nyerere kiuzalendo, kiuadirifu, kiutendaji, n.k. wakajiona kuwa wanapwaya na hatimaye tamaa za urais zikaishia mioyoni mwao tu pasipo mtu yeyote kujua. Hao nadhani walikuwa wengi. Lakini, kama nilivyoeleza hapo juu, leo hii biashara imepiga u-turn.

Hivi sasa, hata wenzangu na mimi wasio na taranta na rekodi ya uongozi zaidi ya kuwa wamebahatika kupata ubunge na kisha uwaziri, tayari wanajiona wana uwezo wa kukalia kiti kikubwa kabisa cha uongozi wa nchi yetu. Kwamba mimi kama NdasheneMbandu, hatma ya nchi yangu iwe mikononi mwangu kwa sababu tu nimeonja radha ya uongozi baada ya binamu yangu, baba yangu, mjomba wangu n.k. kuniteua kushika wadhifa wa uwaziri!!!

Katika mazingira hayo ya kila mwanachama wa chama cha kisiasa kujisikia na kuhangaikia urais, ndipo mnyukano wa kisiasa ndani na nje ya vyama vya kisiasa unapokuwa mkubwa kwani prospective candidates ni wengi, tofauti na ilivyokuwa zamani. Leo hii kwa mfano, ni mtanzania gani katika nchi hii anayefuatilia msuala ya siasa asiyejua kwamba Mzee Sitta kwa udi na uvumba anataka kuwa rais wa nchi hii? Bila shaka, hakuna. Halikadhalika, nani asiyejua kuwa akina Bernald Membe, Frederick Sumaye na wengine wengi wanautaka urais kwa udi na uvumba? Bila shaka, hakuna. Sasa, katika hali ya kisiasa kama hii, ndipo linapokuja suala la HESABU. Mwanasiasa anayeweza kuruga vigingi na kupenya kwenye kina kirefu cha maji yenye mamba wengi lazima awe mpiga hesabu mzuri. Bila hivyo, hafiki mbali. Mfano mzuri wa mwanasiasa wa aina hiyo ni EDWARD NGOAYI LOWASSA. Jamani tutake tusitake huyu jamaa ni mpiganaji na kama ni hesabu za kisiasa basi hapo ndipo zilipolala na kuamkia.

Mazingira ya kashfa ya RICHMOND iliyomwondoa madarakani Lowassa mpaka leo yamebaki kuwa tatanishi japo yeye binafsi ilifikia hatua aliona liwalo na liwe akaamua kuweka ukweli mezani. Kupitia kinywa chake mwenyewe kwenye kikao rasmi na kizito cha ccm, Lowassa alitamka waziwazi pasipo kupepesa macho huku akimtazama usoni Mwenyekiti wake kwamba ni jambo gani alilofanya kuhusiana na RICHMOND ambalo Mwenyekiti hakulifahamu na hakulitolea maagizo. Hiyo ilikuwa ni hatua na tiba muhimu sana ya Lowassa kisiasa na nadhani aliamua kusema hivyo baada ya uvumilivu kumshinda. Wengi wetu tulihabarishwa pembeni kwamba baada ya maneno hayo ya Lowassa, Mwenyekiti alifunga agenda na kuamuru nyingine ifuate. Suala la RICHMOND limekuwa ni turufu kubwa kwa wanasiasa wengine wenye malengo yanayofanana na Lowassa ya kukalia kile kiti cha enzi.

Wanasiasa kama akina Sitta na wafuasi wao akina Nnape walidhani huo ungekuwa mwisho wa Lowassa. Walijua huo ulikuwa ndiyo msumali wa mwisho kwenye jeneza la Lowassa kisiasa. Lakini wapi, mwenzao aliamua kupiga hesabu za chini chini kwa ku-integrate na ku-differentiate na jitihada hizo hatimaye zimeanza kujibu. Hivi sasa, baada ya chaguzi ndani ya ccm, asilimia kubwa ya "wenye maamuzi kichama" ya nani awe mgombea wa ccm wa urais, ipo upande wa Lowassa. Wapo watakaosema chaguzi ziliendeshwa kwa rushwa lakini ukweli ni kwamba uchaguzi umekwisha na viongozi tayari wamepatikana na hesabu tayari zimejibu. Kilichobaki sasa, tuombe uzima tushuhudie nomination ya candidate wa ccm wa urais wa 2015 kama hamtasikia Dodoma ikirindima na jina Lowassa!

Najua wapo pia watakaosema, ccm ikikosea ikamteua Lowassa itakuwa imejimaliza yenyewe na kwa mara ya kwanza urais utaangukia mikononi mwa vyama vya upinzani. Hao nao wasidhani mambo yatakuwa ni mteremko maana huyu jamaa anayeitwa Lowassa anaona mbele na kupiga hatua kabla wapinzani wake hawajafikiria hata kunyanyua mguu. Kwa maneno mengine, Lowassa ni mzuri sana kwa RISK ANALYSIS. Unachokifikiria wewe leo mwenzio alikifiria juzi na kukitolea uamuzi. Mkono wake mpaka sasa tayari umegusa maeneo yote nyeti na akipita yeye anafunga mlango. Hakuna mwingine anayeweza kupita. Mwenye ufahamu, na ayashike maneno haya.

Hayo ndiyo mahesabu makali ya Lowassa. Wenye uwezo wa kumwelezea Lowassa jinsi alivyo mzuri wa kukokotoa hesabu za kisiasa, ni akina Mzee Sitta na Nnape Nauye ambao walijipambanua kukabiliana nae na sasa bila shaka wanatweta baada ya kuishiwa pumzi huku wakishuhudia mwenzao akichanja mbuga.

Thanks!

Umeanza vizuri kbs, tena kwa kutukumbusha mengi ya historia yetu kwa nyanja zote. Ila hapa mwisho sijakuelewa, unataka kutueleza au kuamini nn kuhusu Lowasa??
Wana JF, mi nadhani kwa thread hii, jamaa anamaanisha kuwa Lowasa ni mtu hatari na hafai kbs kua kiongozi Tanzania. Tuikibali hoja
 
Lowasssa aka mti wenye matunda aka mvi ishara ya hekima aka jembe la tanzania aka mkombozi wa watanzania aka mchapakazi aka next prezdaaaa.
 
Huyu yumo dani ya ccm na hatujamsikia hata siku moja akikemea vioja vinavyofanywa na viongozi katika chama chake. Yumo katika mfumo wa ccm uliooza, hivyo basi naye ameoza. Watanzania tunataka mabadiliko sio kuweka viraka vitokanavyo na nguo iliyochakaa.

Sent from my GT-I9100 using Tapatalk 2
 
lowassa = ufisadi, full stop!

kulingana na jina lako husitaili kujibu usilolijua muulize mr 6 na mawembe wanajua fika richmond ni ya cia na mwenye nyumba huyu bwn kabebeshwa tu mzigo iko siku atasema yote subirini. Hawezi kumwachia mlevi baa na pombe
 
kweli njaa mbaya sana tumeshaanza mambo ya 2005 ya kutuamanisha kuwa wapo watu chaguo la mungu.chonde safari hii msitufikishe huko waachaeni watu wapambanue wenyewe.halafu wekeni hadharani maneno aliyoambiwa na mwl 1995 pale alipojaribu kutia mguu kenye urais
 
Mimi nilikuwa namfagilia Sita lakini tangu aanze kuropoka ovyo na kuwa vuguvugu kwa kusapoti ujinga wa chama na serikali nimetoa kabisa kwenye kundi la viongozi wanaofaa kuchukua nchi yetu..Mpaka sasa CCM sijaona anayefaa kukamatia 2015.
Membe ndio kabisa hafai maana anapenda misifa na ni mnafiki wa hali ya juu. Kwanza hajawahi kufanya chochote ambacho anaweza kujivunia katika uongozi wake, bora hata Lowasa alijenga shule za Kata.
 
Ni kweli aisee watu wanaongelea ufisadi wasio na ushahidi nao, ipo haja ya kutenda haki mara mojamoja. Hizi hukumu za mitaani zinaifanya hii nchi iwe ya kihuni. Ni dhambi kuhukumu bila kufuata misingi ya mifumo stahiki tuliyojiwekea, kama unahisi hakuitendea haki nchi na una ushahidi wa hayo unayoyaongea mahakama ziko wazi kafungue kesi umshitaki ni haki ya kikatiba. Tofauti na hapo ni majungu na fitna na hakika Mungu hapendi. Yapo mazuri aliyofanya na kuzuia yasisemwe ni udikteta. Nawasilisha!
 
Angekuwa na akili kiasi hicho angeshinda ukweni Arumeru Mashariki
-Ajibu tuhuma za ufisadi kwenye list of shame
-Ajibu tuhuma za Richmond
-Ajibu swali la Mwl.Nyerere kwanza,alipata wapi utajiri huo?

Akishajibu yote hayo bado atakuwa hafai as long as yupo ndani ya rogue system ya CCM
 
Ni kweli aisee watu wanaongelea ufisadi wasio na ushahidi nao, ipo haja ya kutenda haki mara mojamoja. Hizi hukumu za mitaani zinaifanya hii nchi iwe ya kihuni. Ni dhambi kuhukumu bila kufuata misingi ya mifumo stahiki tuliyojiwekea, kama unahisi hakuitendea haki nchi na una ushahidi wa hayo unayoyaongea mahakama ziko wazi kafungue kesi umshitaki ni haki ya kikatiba. Tofauti na hapo ni majungu na fitna na hakika Mungu hapendi. Yapo mazuri aliyofanya na kuzuia yasisemwe ni udikteta. Nawasilisha!

Kwa nini yeye asilinde image yake? Je anataka kufanya hivyo baadae?Kwa nini iwe hivyo?
Opportunist!
 
Lowass ndiye Rais wetu ajaye....maeneo yote nyeti yameshamkuibali!

Ni kweli kila 1 anajua lowasa ni rais wa ccm na mafisadi lkn si rais wa tz na kamwe hatokuwa. Mwambien hiyo hela asiipoteze bure ili ije imsaidie kutoroka 2015 akipata upenyo.
 
kulingana na jina lako husitaili kujibu usilolijua muulize mr 6 na mawembe wanajua fika richmond ni ya cia na mwenye nyumba huyu bwn kabebeshwa tu mzigo iko siku atasema yote subirini. Hawezi kumwachia mlevi baa na pombe

Ishakuwa vry late saiv watz hata hatuuitaji huo upuuzi ambao ww eti unauita ukweli. Hatudanganyiki kirahisi kama anaukweli kwa nn asingeusema bungeni badala ya kukimbilia kujiuzulu? Anasubiri ni nini? Na ili amlinde nani? Kwa masilihi ya nani? mtu yeyote akishajiuliza maswali marahisi kama hayo juu ya hyu mwizi hawezi hata kumdhania kwenye nafasi ya urais mamvi. Kitu nnachokifurahia ni kwamba jamaa hawezi kuonga watz wote kama anajidanganya rushwa ndo ushindi.
 
Back
Top Bottom