Makonda usipitilize unafiki, omboleza kivyako halafu nenda zako

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,172
Nimeikuta hii makala mahali, nikajisemea, wanafiki wote hata geti la mbinguni hawataliona, Makonda akiwemo.

Paulo Makonda akiwa Mkuu wa Mkoa DSM, alimtafuta mwanamke anaitwa Fatma Chikawe, akampa jina la ‘Fatma Lowassa’. Edward Lowassa alikuwa mjumbe wa kamati kuu CHADEMA.

Paulo Makonda akamuita mwanamke huyo katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mbele ya waandishi wa habari, akijitambulisha kama mtoto wa kike aliyetelekezwa na Edward Lowassa.

Edward Lowassa akagoma kupimwa DNA akisema hamtambui mwanamke huyo na anatumika kumchafua kisiasa. Edward Lowassa alisema hayo alipohojiwa na gazeti la NIPASHE 2018.

April 10, 2018, Fatma Chikawe alikuwa kati ya waliojitokeza ofisi ya Mkuu wa Mkoa - DSM kutafuta msaada wa kisheria akidai Edward Lowassa ni baba yake mzazi na hajawahi kumuona tangu kuzaliwa.

April 14, 2018, Paulo Makonda akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema anayo majina zaidi ya 100 ya viongozi wa serikali wakiwepo wastaafu, viongozi wa dini, na wabunge ambao walitajwa.

April 15, 2018, ikaonekana video nyingine katika mitandao ya kijamii, Fatma Chikawe akiomba radhi kwa kumdhalilisha Edward Lowassa akisema tukio hilo limechukuliwa kisiasa na anakosa amani.

Fatma Chikawe katika video hiyo iliyosambaa alinukuliwa alisema aliwahi kukutana na Fred Lowassa (mtoto mkubwa wa Edward Lowassa) na akamuahidi kumsaidia lakini amekuwa kimya.

Mtoto mkubwa wa Edward Lowassa, Fred Lowassa, alishangaa mwanamke huyo aliyejitokeza na kudai kuwa ni binti wa mwanasiasa huyo mkongwe aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

Fred Lowassa akamjibu huyo mwanamke, Fatma Chikawe, “Kwa taarifa tu sisi watu wa Monduli kwetu watoto ni baraka na neema, nimeshangaa ametukosa ukoo mzima kujitambulisha.”.

“Namwambia Paul Makonda, nimetoka naye mbali sana, nasikitika sana anavyotumia nafasi yake vibaya kwa manufaa anayoyajua. Paulo Makonda nimekulea.” Alisema Fred Lowassa

Leo Paulo Makonda nyumbani kwa Edward Lowassa, Masaki, Dar es Salaam, anasema kuna watu walimchafua Edward Lowassa na leo wanampongeza na kumsifia Lowassa. Bashite ni TAPELI wa kisiasa.

🤣🤣🤣🤣
 
Tatizo la Makonda hajui kuutumia ule usemi wa wazungu 'learn to quit while you are still ahead'.

Kwa aliyoyafanya baada ya kuteuliwa kama katibu muenezi yalishasahaulisha watu kuhusu mabaya yake. Sasa yale makofi yamemlevya kiasi cha kutaka makofi zaidi kiasi cha kuanza kuharibu.

Ni swala la muda Makonda atajiangamiza mwenyewe ikiwa tayari alishaanza kuelekea kileleni.

Adui wa Makonda ni Makonda mwenyewe kupitia uraibu wake wa kupenda sifa.
 
Nakumbuka hii movie, Bashite alikua na siasa za kitoto sana

Ila Lowassa siwezi kumlilia , naona ni kati ya mabwanyenye wanufaika na mfumo wa hovyo wa Tz, hakuwa mwana mabadiliko kama wengi wanavyomnadi
mtoto-LOWASSA.jpg
 
Tutofautishe maisha ya mtu akiwa hai na akiwa amekufa. Maana yangu ni nini yapo mambo aliyotenda Marehemu akiwa hai kama yalikuwa ya kipuuzi na watu wakatoka hadharani kuusemea upuuzi huo tusiwajadili kwà mtazamo hasi. Kwà kuwa ilikuwa katika kujenga.

Pia tusipende kumuelezea Marehemu kwà mazuri tu tueleze na mabaya yake ili kupunguza unafiki katika jamii yetu ya kitanzania.
 
sema tu una chuki binafsi labda na makonda, watanzagiza mnapenda sana ku attack watu wa chini makonda alikuwa anatumwa tu kama vile anavyotumwa sasa hivi isitoshe hivi kati ya makonda na aliyemkata lowasa nani kamuumiza zaidi lowasa?

Vipi waliokuwa wanasema kajinyea kipindi cha kampeni na mpaka waliweka picha mitandaoni wote hao haujawaona umemuona makonda tu ?ni kama sasa hivi kila mtu analaumu kila mtu kukosekana kwa umeme lkn mhusika mkuu raisi mwenyewe mnamuacha, hii typical tabia ya tanzagiza …
 
Kauli za wanasiasa sio za kukaa unawazia fikiria ile LIST OF SHAME iliyosomwa pale Mwembe Yanga na CHADEMA uliwahi kuwaza kuwa watakuja kumpa awe mgombea uraisi Lowassa?

" ni haki mbele za mungu kumzomea Lowassa" Godbless Lema. Leo anampongeza
 
Tutofautishe maisha ya mtu akiwa hai na akiwa amekufa.Maana yangu ni nini yapo mambo aliyotenda Marehemu akiwa hai kama yalikuwa ya kipuuzi na watu wakatoka hadharani kuusemea upuuzi huo tusiwajadili kwà mtazamo hasi,Kwà kuwa ilikuwa katika kujenga.Pia tusipende kumuelezea Marehemu kwà mazuri tu tueleze na mabaya yake ili kupunguza unafiki katika jamii yetu ya kitanzania.
Kwahiyo kwako ni sawa Bashite kumsingizia Lowasa mtoto??
 
sema tu una chuki binafsi labda na makonda, watanzagiza mnapenda sana ku attack watu wa chini makonda alikuwa anatumwa tu kama vile anavyotumwa sasa hivi isitoshe hivi kati ya makonda na aliyemkata lowasa nani kamuumiza zaidi lowasa ? vipi waliokuwa wanasema kajinyea kipindi cha kampeni na mpaka waliweka picha mitandaoni wote hao haujawaona umemuona makonda tu ?ni kama sasa hivi kila mtu analaumu kila mtu kukosekana kwa umeme lkn mhusika mkuu raisi mwenyewe mnamuacha, hii typical tabia ya tanzagiza …
Uwepo wa waliosema kajinyea, hakuondoi yaliyofanywa na Makonda. Kila mmoja na mambo yake..!! Hata Nape naye anayo ya kumfanya aonekane mnafiki kwenye huu msiba..!!
 
sema tu una chuki binafsi labda na makonda, watanzagiza mnapenda sana ku attack watu wa chini makonda alikuwa anatumwa tu kama vile anavyotumwa sasa hivi isitoshe hivi kati ya makonda na aliyemkata lowasa nani kamuumiza zaidi lowasa ? vipi waliokuwa wanasema kajinyea kipindi cha kampeni na mpaka waliweka picha mitandaoni wote hao haujawaona umemuona makonda tu ?ni kama sasa hivi kila mtu analaumu kila mtu kukosekana kwa umeme lkn mhusika mkuu raisi mwenyewe mnamuacha, hii typical tabia ya tanzagiza …
Shikamooo,na huo ndio ukweli,watu ni wanafki,wanachuki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom