Siasa ni Hesabu. Anayebisha Amuangalie Lowassa Halafu Awaulize Sitta na Nnape

Lowassa alipokuwa waziri wa ardhi alikuwa anatumia madaraka hayo kuwanyang'anya viwanja wahindi huku akitangaza RTD kuwa kafanya hivyo kwa fiada ya umma lakini baadaye akawa anapokea hela nyingi sana kutoka kwa hao hao aliotanganza kuwanyang'anya viwanja, na baadaye akawarudishia viwanja hivyo kimya kimya. Hicho ndicho kilichokuwa chanzo cha utajiri wa Lowassa. Alipokuwa Waziri Mkuu, alitumia madaraka hayo kulazimisha RichMondulian kupewa tenda ya umeme wa dharura bila kufuata taratibu, jambo ambalo limeiingiza Tanzania katika matatizo makubwa sana ya kisheria kimataifa. Alifanya yote hayo akiwa ni waziri anayewajibika kwa rais. Je mtu huyu akiwa ndiye rais mwenyewe mwenye uamuzi wa mwisho ataacha kufanya lipi kwa manufaa yake binafsi na kulisahau taifa hili? Kikwete mwenyewe ambaye ni nafuu kidogo bado kaliangamiza taifa hile je Lowassa atatuachia nini?

Uongozi wa mwisho unahitaji sana hekima maadili, ambayo nadhani Lowassa hana kabisa. Ni mtaalamu wa kufukuzia mali na kuwashinda wengine kwenye madili ya fedha; akiwa na madaraka atafukuzia sana na kuwazuia watanzania wengine wote wanaoingia katika njia yake ya mali. Inanitisha sana Tanzania tunakoenda!

huu uchapa kazi wa lowassa kama upo kweli bila maadili ya uongozi ni kazi bure kwa taifa..uchapa kazi bila maadili unaweza kufanywa pale kwenye taasisi ndogo ndogo zisizoathiri maisha ya mamilioni ya watu lakini siyo kiti cha Urais. Hata kama atakua mkali kiasi gani na mfuatiliaji na mfokaji huu mfumo uliomnufaisha na atakaoacha imara zaidi utakuja leta vita tanzania ya watoto wetu.
 
uko sawa, ndani ya CCM EL hawezekaniki,,,,yeye hata akiteuliwa tu kugombea urais kupitia CCM huo ni ushindi kwake dhidi ya wabaya wake kama mzee six....hata CHADEMA wangependa sana EL ateuliwe,,,ni rahisi ku - compete na yeye na kumshinda...

Hata hivyo naamini kwa sasa Tanzania inahitaji COMPLETE REFORM

EL siyo mjinga anajua akipita CCM, CDM ni kazi ndogo tu...$ nyingi zitatumika na dola ya CCM itatumika hata ndani ya katiba mpya kama ibadadilishwa na itawekwa b4 2015
 
Umesema vema, ile tu EL kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM 2015 itakuwa ni bonge ya ushindi kwake dhidi ya maadui zake akina Six shida ni kwamba he cannot stand strong with CHADEMA wind....

Kwa sasa wananchi ni kama wanasubiri kuhalalisha utawala wa CHADEMA,,,,naamini inahitajika COMPLETE OVERHAUL of the Political System

kwenye red, CDM sijasikia wakisema hili as a priority than kuitoa tu CCM madarakani na wenyewe kupata dola basi. I doubt their credentials kama wanamageuzi wa kweli au opportunists who only wants state power for themselves
 
Ni kweli kila 1 anajua lowasa ni rais wa ccm na mafisadi lkn si rais wa tz na kamwe hatokuwa. Mwambien hiyo hela asiipoteze bure ili ije imsaidie kutoroka 2015 akipata upenyo.

Kwanza inabidi muda huu tumkomalie Membe bungeni.Hebu tuangalie Extradition treaties ambazo Tanzania imesaini.Hatutaki mhalifu yeyote atoroke bila kurudishwa nchini.Vijana Chadema tutahakikisha tunafanya kazi bega kwa bega kuhakikisha hakuna mwizi yeyote atakayesamehewa.Na napendekeza tuanzishe special Tribunal kwa ajili yao 2015.Najua watalia sana kwamba tunalenga wapinzani kipindi hicho,hili tuliweke wazi kabisa
 
kwenye red, CDM sijasikia wakisema hili as a priority than kuitoa tu CCM madarakani na wenyewe kupata dola basi. I doubt their credentials kama wanamageuzi wa kweli au opportunists who only wants state power for themselves

Usipende kusikia,jenga tabia ya kusoma pia incase hukupata fursa ya kusikia.Soma vizuri ilani 2010-2015 na sera ya Chadema.Ipo hata online
 
nashukuru kaka, ila majukwaani ambapo siasa zetu za kitz ndipo haswa wengi wetu hupata maelezo ya mustakabali wa chama, taifa etc sera, ahadi na mengineyo CDM hawako wawazi kuhusu hii anayosema huyu jamaa yaani a COMPLETE OVERHAUL OF THE CURRENT POLITICAL SYSTEM.
 
umefika wakati kwa kila ajuaye udhaifu wa Lowasa auanike hapa jamvini. kadhalika kila ajuaye mazuri yake ayaweke hapa. tutasoma na kutafakari na kupima wenyewe. maelezo tu yasiwe maoni. yaani yawe facts about Lowasa and not opinions. humu watu wanaleta opinions badala ya facts au wanaleta opinions na kuzijustitfy na weak factss. ninaposema facts ni lazima ziwe porved beyond doubt full with evidence.
 
Huyu jamaa anatumia hell of money na kila mbinu chafu kuununua urais...!! Hv jamani watu hamjiulizi kwanini..????????
Tanzania yetu hizi njaa zitatumaliza jamani, wee uhongwe just laki moja au million afu unayaweka maisha yako na ya vizazi vyako rehani..!! Mbona viongozi watendaji wapo wengi jamani, why should we vote for somebody who is thriving that much just to be a president...!! Siatauza nchi huyu afu wote tuwe wapangaji....!! Why are we nat using common sense au ndo kweli wabongo sikuhizi tumeswitch na kutumia masaburi kufikiri insteady of brain....!!
 
kwa mtazamo rahisi wa kuwa tanzania haiwezekani bila ya ccm watakubaliana haraka na wewe.Lakini je jamii ya binadamu haina na wala haihitaji badiliko.Unaweza kutka kuwaaminisha watu kuwa Lowassa ana hesabu kali za kisiasa lakini kwa hesabu zake anaweza kuzuia mabadiliko wakati ukifika?
Mabadiliko yameikumba kenya,Zambia na karibuni nchi za kiarabuambazo nyingi zilikuwa zinatawaliwa kiimla.Je watanzania leo wanaitazma ccm kama mkombozi wao kwa jinsi walivyokuwa wanaitazama TANU?je ccm ni imara yenyewe kama taasisi?angalia mparaganyiko wa uchaguzi wa jumuia zao.
Kama bado unalala na kuamka ukiamini kama mzee malecele aliwahi kusema kuwa ccm itaendelea kutawala kwa miaka mia moja ijayo keep on dreaming watanzania wameamka
 
na achanje mbuga.

Binafsi namkubali sana. Si kwa lolote bali ni kwa utendaji wake. Yuko vema
utendaji upi?kigezo cha kwanza cha kiongozi bora na uadilifu na uzalendo,ameishawahi kueleza ni kwa jinsi gani amepata ukwasi wake mkubwa wa kutisha?na pili kwa nini atumie pesa nyingi kujitengenezea mazingira ya urais?je ni kigezo cha pesa ambacho we umeona yuko vema?Pole sana kuna kazi kubwa sana ya kuwaelimisha watu kama wewe maana ya uzalendo.
China linapokuja suala la uzalendo hawana masihara wanakuua,hapa nyinyi mtu asipokuwa mzalendo na akitoa rushwa mnamuona shujaa,mnahitaji kuombewa
 
kwenye red, CDM sijasikia wakisema hili as a priority than kuitoa tu CCM madarakani na wenyewe kupata dola basi. I doubt their credentials kama wanamageuzi wa kweli au opportunists who only wants state power for themselves

Hovyoo
 
kama mnataka rais mtendaj na mzalendo ni dr slaa, lakn kama mnamtaka mchapaka kazi ndani ya ccm ni lowassa hakuna mwngne
 
kwa wale wenye kujua mabo ya kisiasa huhitaji kuuliza ya kuwa lowasa ni nani nchi hii kwa upande wangu binafsi naamini kama lowas ndo angekuwa raisi wa nchi hii tungekuwa kama rwanda hata matatizo mengine kama mfumuko wa vitu sokoni usingekuwa kwa kiasi hiki kama ilivyo sasa lowasa ni mtu ambaye siasa inamheshimu na yeye pia naiheshimu pia tofauti na watu kama jk ambaye suala la siasa kwake ni lazima na ndio kaka mkubwa pamoja na mdogo wake nnape wameamua kunyamaza tena hawana tena la kuongea hivyo nami sitashangaa kuona akipitishwa kugombea uraisi na mimi nasema kuwa kama akipitishwa kugombea uraisi mimi kura haina kipingamizi kwani naamini jamaa ni mpiganaji
 
:shut-mouth:
Wadau,

Nianze kwa kuomba radhi kwa wanaJF wenye allergy na EDWARD N. LOWASSA. Najua wapo wadau wengi humu jamvini ambao wakisikia LOWASSA wanakumbuka UFISADI na wakitamka UFISADI wanakumbuka LOWASSA. Watu waliopo kwenye kundi hili, ndiyo ninaowaomba radhi. Wanisamehe sana maana sidhani kama kuna namna unayoweza kuzungumzia siasa za kisasa za Tanzania bila kumgusa LOWASSA.

Katika vipindi vyote au wengine wanavyoita awamu zote za uongozi wa nchi yetu tangu uhuru, hakuna wakati ambapo wananchi tumeshuhudia siasa ikitamalaki kama wakati huu. Mazingira ya sasa nchini kisiasa pengine ni magumu kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Hivi sasa, kila mwanachama w chama fulani na hata raia tu asiye na chama anajisikia kuwa anaweza kuwa rais wa Tanzania. Hali hii ni tofauti na zamani na hii inaweza kuwa imetokana na namna nchi inavyoongozwa kiholela kwa kiwango kisichoweza kutarajiwa. Kwa wanaJF wenye umri wangu, hivi ni wana-ccm gani enzi za Mwl. Nyerere ambao angalau hata walifikiria wakati huo kurithi mikoba ya uongozi kutoka kwa Nyerere? Bila shaka, walikuwa wachache sana na sidhani kama walikuwa wanajionesha waziwazi. Wapo wanaJF wanaoweza kuiongelea hali hii kwa mtazamo hasi kwamba Nyerere alikuwa kiongozi wa kiimra na kwamba hakujenga "mazingira rafiki" ya wanachama kujisikia huru kutangaza nia yao ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha urais. Mtazamo huo unaweza kuwa na ukweli to some extent lakini upande chanya pia unaweza kuwepo kwamba baadhi ya wanachama ulipofika wakati wa uchaguzi walijitazama kwa undani na kujilinganisha na Mwl. Nyerere kiuzalendo, kiuadirifu, kiutendaji, n.k. wakajiona kuwa wanapwaya na hatimaye tamaa za urais zikaishia mioyoni mwao tu pasipo mtu yeyote kujua. Hao nadhani walikuwa wengi. Lakini, kama nilivyoeleza hapo juu, leo hii biashara imepiga u-turn.

Hivi sasa, hata wenzangu na mimi wasio na taranta na rekodi ya uongozi zaidi ya kuwa wamebahatika kupata ubunge na kisha uwaziri, tayari wanajiona wana uwezo wa kukalia kiti kikubwa kabisa cha uongozi wa nchi yetu. Kwamba mimi kama NdasheneMbandu, hatma ya nchi yangu iwe mikononi mwangu kwa sababu tu nimeonja radha ya uongozi baada ya binamu yangu, baba yangu, mjomba wangu n.k. kuniteua kushika wadhifa wa uwaziri!!!

Katika mazingira hayo ya kila mwanachama wa chama cha kisiasa kujisikia na kuhangaikia urais, ndipo mnyukano wa kisiasa ndani na nje ya vyama vya kisiasa unapokuwa mkubwa kwani prospective candidates ni wengi, tofauti na ilivyokuwa zamani. Leo hii kwa mfano, ni mtanzania gani katika nchi hii anayefuatilia msuala ya siasa asiyejua kwamba Mzee Sitta kwa udi na uvumba anataka kuwa rais wa nchi hii? Bila shaka, hakuna. Halikadhalika, nani asiyejua kuwa akina Bernald Membe, Frederick Sumaye na wengine wengi wanautaka urais kwa udi na uvumba? Bila shaka, hakuna. Sasa, katika hali ya kisiasa kama hii, ndipo linapokuja suala la HESABU. Mwanasiasa anayeweza kuruga vigingi na kupenya kwenye kina kirefu cha maji yenye mamba wengi lazima awe mpiga hesabu mzuri. Bila hivyo, hafiki mbali. Mfano mzuri wa mwanasiasa wa aina hiyo ni EDWARD NGOAYI LOWASSA. Jamani tutake tusitake huyu jamaa ni mpiganaji na kama ni hesabu za kisiasa basi hapo ndipo zilipolala na kuamkia.

Mazingira ya kashfa ya RICHMOND iliyomwondoa madarakani Lowassa mpaka leo yamebaki kuwa tatanishi japo yeye binafsi ilifikia hatua aliona liwalo na liwe akaamua kuweka ukweli mezani. Kupitia kinywa chake mwenyewe kwenye kikao rasmi na kizito cha ccm, Lowassa alitamka waziwazi pasipo kupepesa macho huku akimtazama usoni Mwenyekiti wake kwamba ni jambo gani alilofanya kuhusiana na RICHMOND ambalo Mwenyekiti hakulifahamu na hakulitolea maagizo. Hiyo ilikuwa ni hatua na tiba muhimu sana ya Lowassa kisiasa na nadhani aliamua kusema hivyo baada ya uvumilivu kumshinda. Wengi wetu tulihabarishwa pembeni kwamba baada ya maneno hayo ya Lowassa, Mwenyekiti alifunga agenda na kuamuru nyingine ifuate. Suala la RICHMOND limekuwa ni turufu kubwa kwa wanasiasa wengine wenye malengo yanayofanana na Lowassa ya kukalia kile kiti cha enzi.

Wanasiasa kama akina Sitta na wafuasi wao akina Nnape walidhani huo ungekuwa mwisho wa Lowassa. Walijua huo ulikuwa ndiyo msumali wa mwisho kwenye jeneza la Lowassa kisiasa. Lakini wapi, mwenzao aliamua kupiga hesabu za chini chini kwa ku-integrate na ku-differentiate na jitihada hizo hatimaye zimeanza kujibu. Hivi sasa, baada ya chaguzi ndani ya ccm, asilimia kubwa ya "wenye maamuzi kichama" ya nani awe mgombea wa ccm wa urais, ipo upande wa Lowassa. Wapo watakaosema chaguzi ziliendeshwa kwa rushwa lakini ukweli ni kwamba uchaguzi umekwisha na viongozi tayari wamepatikana na hesabu tayari zimejibu. Kilichobaki sasa, tuombe uzima tushuhudie nomination ya candidate wa ccm wa urais wa 2015 kama hamtasikia Dodoma ikirindima na jina Lowassa!

Najua wapo pia watakaosema, ccm ikikosea ikamteua Lowassa itakuwa imejimaliza yenyewe na kwa mara ya kwanza urais utaangukia mikononi mwa vyama vya upinzani. Hao nao wasidhani mambo yatakuwa ni mteremko maana huyu jamaa anayeitwa Lowassa anaona mbele na kupiga hatua kabla wapinzani wake hawajafikiria hata kunyanyua mguu. Kwa maneno mengine, Lowassa ni mzuri sana kwa RISK ANALYSIS. Unachokifikiria wewe leo mwenzio alikifiria juzi na kukitolea uamuzi. Mkono wake mpaka sasa tayari umegusa maeneo yote nyeti na akipita yeye anafunga mlango. Hakuna mwingine anayeweza kupita. Mwenye ufahamu, na ayashike maneno haya.

Hayo ndiyo mahesabu makali ya Lowassa. Wenye uwezo wa kumwelezea Lowassa jinsi alivyo mzuri wa kukokotoa hesabu za kisiasa, ni akina Mzee Sitta na Nnape Nauye ambao walijipambanua kukabiliana nae na sasa bila shaka wanatweta baada ya kuishiwa pumzi huku wakishuhudia mwenzao akichanja mbuga.

Thanks!
Kama issue ya malawi....lakini bado si msafi.
 
Mimi nabisha siasa si hesabu, niliwekewa alama ya vema kama nilivyofundishwa, nilijibu SIASA NI KILIMO.
Sijapoteza hata muda wangu kusoma uliyoyaandika. kichwa cha habari pekee jibu lake ni hilo, HANGAIKENI NALO.
 
Ndugu elewa hesabu za EL sio za kisiasa, ni hesabu anazopiga kuhakikisha hakamatwi, na hiyo ni kanuni ya mwizi yeyote duniani katika medani ya siasa..as they say, the rule number one, don't get caught, kwa hiyo yeye unamuona hesabu zake ni kali kwa kuwa tu hajakamatwa, na hii inatokana mfumo dhaifu uliopo, kwa hiyo hakuna kukata tamaa WaTZ tunahitaji mtu mwenye background nzuri kiuongozi na kimaadili, na SIYO HUYU.
 
Back
Top Bottom