Ujumbe wa Bashe kwa Kikwete uliozua gumzo ni kuhusu Edward Lowassa

Girland

JF-Expert Member
Jan 24, 2016
1,826
2,842
Wakati tunasikitika kumpoteza, Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu, si vibaya tukakumbushana kidogo.

Ikumbukwe, baada ya kukatwa kwa jina la Edward katika kinyang'anyiro cha kumtafuta Mgombea wa CCM mwaka 2015. Mzee Lowassa alitimkia upinzani CHADEMA, ambako alipata nafasi ya kugombea Urais akishindana na Hayati JPM.

KURUDI CCM
Baada ya hapo mwaka 2019, Lowassa alitangaza kurudi CCM na alipongezwa na Rais Mstaafu Kikwete kupitia ukurasa wake wa Twitter (sasa X). Bashe (sasa Waziri wa Kilimo) aliijibu tweet ile akimlaumu JK kuwa ndiye chanzo cha Mzee Lowassa kuhamia Upinzani!

Je Bifu hilo la Lowassa na JK lilisuluhishwa? Karibuni wajuvi nimeweka na ushahidi wa picha ya tweet hizo

IMG_9374.jpeg
 
Nakubaliana na Bashe 100%. Jakaya ni mnafiki sana. Alimuuza sana Lowassa. Niliwahi kukaa na kuzungumza na Lowassa kuhusu hilo na hasa sakata la Richmond. Lowassa aliniambia, "tatizo Rais wetu ni mshamba. Akishakalia hicho kiti anadhani amemaliza yote. Ni muongo na asiyejiamini." Nayaishi maneno haya ya Lowassa Hadi kesho.
 
Back
Top Bottom