Serikali yatangaza viwango vipya vya alama za ufaulu elimu ya sekondari

Kufuatia serikali kutangaza viwango vipya vya alama za ufaulu kwa shule za sekondari, ni ishara ya serikali kushindwa yafuatayo;

1. Serikali imeshindwa kukabiliana na wimbi la kufeli kwa wanafunzi wa sekondari
2. Serikali imeshindwa kuboresha shule za kata kua katika viwango bora vya utoaji wa elimu,
3. Serikali imeshindwa kusikiliza na kuthamini madai na maslahi ya walimu,
4. Haya ni matokeo ya serikali kutothamini na kupuuza maoni ya wadau mbalimbali kuhusu masuala elimu.

Si sahihi hata kidogo; kama serikali inaona kurahisisha ufaulu ndio njia bora ya kuboresha elimu basi ijue kwamba imepoteza uelekeo, na kwa kufanya hivi tusitegemee kupata taifa bora lenye nguvu na wasomi wa kutusaidia kuondokana na umasikini.
Wito wangu kwa serikali;
*boresheni shule za kata sambamba na kuzipatia mahitaji muhimu,
*wekeni mitaala imara ya elimu,
*Walipeni mishahara mizuri walimu sambamba na kusikilizeni madai ya waalimu

hatua hii ya kubadilisha madaraja ya ufaulu ni ya mwisho kabisa,kwakuwa naamini hata kama utapanga A ni 95 had 100 kama kuna miundombinu mizuri katika elimu wanafunzi watafaulu tu
 
===>Wasomi wa nchi ndio ambao wanatuhujumu sisi watanzania,sijui tunaenda wapi?adui wa matokeo yetu ni hawa hapa:
1---Mishahara,posho na mazingira mazuri ya walimu wetu
2---Madara,maabara na miundombinu mingine kama umeme nk
===>Yakifanyiwa kazi haya hayo madaraja hayana maana hata kidogo
===>Leo nimegundua kwa nini tunaiogopa Jumuiya ya Afrika Mashariki,hapa hakuna ubishi tena uwezo wetu wa kielimu ni mdogo sana,wakenya,warwanda wakija hapa nchini watachukua kila kazi kwa sababu za ajabu kama hizi za kuchakachua elimu.
 
Ndo tatizo letu wabongo badala ya kujadili suala kwa umakini tunaleta siasa na biasnes, hatuwezi kuendelea kama tuna mawazo na akili ya namna hii!

mkuu umelenga kwenye shida. Siasa everywhere! Shuleni si pahala pa siasa tutaharibu kila kitu. Wabunge makini pazeni zenu na wananchi tuache unafiki tuungane kuwatetea watoto wetu wapate elimu bora vinginevyo ni majanga. Hivi,, hawa wa div.5 watapelekwa ualimu siyo?
 
mkuu, fuatilia vizuri. katika alama 40 za CA 15 ni za mtihani wa FM 2 na 15 za fm 3 ambazo hufanyika kikanda. 10 zitzchangiwa na vitu vingine kama project nk.
mzamifu repoti ya maendeleo ya mwanafunzi inajumuisha nini?
 
Last edited by a moderator:
===>Wasomi wa nchi ndio ambao wanatuhujumu sisi watanzania,sijui tunaenda wapi?adui wa matokeo yetu ni hawa hapa:
1---Mishahara,posho na mazingira mazuri ya walimu wetu
2---Madara,maabara na miundombinu mingine kama umeme nk
===>Yakifanyiwa kazi haya hayo madaraja hayana maana hata kidogo
===>Leo nimegundua kwa nini tunaiogopa Jumuiya ya Afrika Mashariki,hapa hakuna ubishi tena uwezo wetu wa kielimu ni mdogo sana,wakenya,warwanda wakija hapa nchini watachukua kila kazi kwa sababu za ajabu kama hizi za kuchakachua elimu.


Kuna shule ya kata inaitwa Mwandeti eti wamefunga shule jana mpaka January 13, 2014.......
 
BRN ni politics at work, tunahangaika na kuwafaulisha kizembe wanafunzi bila kuboresha mitala ya elimu kwanza, mazingira ya kielimu bado mabovu, shule nyingi hazina nyenzo muhim kama maabara etc , shule hazina madawati, watoto wanakaa chini darasani, mazingira ya kazi kwa walimu ni mabovu sana/mishahara,nyumba za kuishi nk. Shule za kata hazina walimu wa kutosha etc, Hakuna mkakati maalum wa kuboresha taaluma ya ualimu nchini....then serikali inatuambia eti BIG RESULT NOW!!! Suala la elimu ni technical issue then serikali inajaribu kua approach kwa politics...majanga..majanga
 
Mimi kwenye madaraja sina la kusema kwa sababu hata mwaka jana nilisoma sana sana sana, nikitegemea nikipata alama 41+ nitakuwa na C, na kwa kweli mtihani ulivyokuwa sikuwa na wasiwasi kabisa na hilo, lkn matokeo yalivyokuja sikuamini kwani nilifeli vibaya (4 ya 33). Wasiwasi wangu ni hapa kwenye CA hasa kwa sisi watahiniwa wa kujitegemea tuliopitia QT, kwani wamesema CA zetu zitatokana na mtihani wa QT. Sasa kwa mfano mimi huo mtihani wa QT niliufanya 2011 hivyo nikafanya mtihani wa form four 2012 nikafeli na mwaka huu na resiti. Swali, je hizo CA zangu za QT watazipataje?? Wana mda kweli NECTA wa kuanza kukagua nilikotoka?? Naumia sana mwaka jana nilitumia nguvu nyingi sana ktk kusoma, na ndicho kilicho kuja kutoka kwenye mtihani lkn sikuambulia kitu. Sijivunii kuwa Mtanzania!, navumilia kuwa Mtanzania!
 
Si Kawambwa tu Mkuu. Serikali yote kuanza Kikwete hawajawahi kufanya lolote la maana zaidi ya madudu katika mawizara mbali mbali waliyopitia hadi katika nafasi zao walizokuwa nazo leo hii. Ni madudu tu, ujanja ujanja na ufisadi wa hali ya juu matokeo yake nchi inakuwa haina maendeleo yoyote yale kila kitu kinadumaa.
Binafsi huu mfumo mpya unaweza kuleta mabadiliko tusiwe tu wa kwanza kulaumu serikali kwa kila kinachobadilika tuupe muda wa kufanyakazi huu mfumo kisha tuone matunda yake .
Watu wengi tunakuwa na tabia ya kuogopa mabadiliko hii tabia inatufanya kubaki nyuma.
nakupa mfano huu kukudhihirishia hilo " kawaida kwako umezoea kitanda kinakuwa pembeni ya ukuta siku ukitoka kazini ukakuta mkeo kakisogeza katikakati ya chumba alafu akaondoka kwenda sokoni ukiingia tu chumbani lazima utashituka na kinachofuatia nikumpigia simu huku ukijiuliza maswali mengi"
Huu ni uwoga mkuu.
 
Hayo ni mawazo yako na upeo wako mdogo wa kufikili kwani grade hizi zinaubaya gani kama kweli unachambua mambo bila ushabiki wa kitoto.
 
kwa style hii hakuna atayefeli maana kila shule zitakua zinapeleka CA maximum wizarani kwan nani atahoji kwa nini zimekua ivyo... mwisho wa cku mtu anapata CA ya 40 alafu final anapata 2/60 anaondoka na c yale safi.... kwa kifupi kutakua hakuna tena watoto wajinga...

Taarifa toka Wizarani inaonesha kuwa walipofanya majaribio ya hiyo grading mpya kwa kutumia matokeo ya mwaka 2013 waliofaulu wanakuwa zaidi ya asilimia 90. Hebu fikiria awali matokeo ya K4 2013 yalikuwa asilimia ya ufaulu ni. 35, wakafanya wanachojua ikaja asilimia 43, sasa kama wangetumia grading hii iliyotangazwa ingekuwa wamefaulu zaidi ya asilimia 90. Hivi kweli hao viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza nchi hii hawawezi kuweka maslahi ya nchi hata chembe. Hawana hata chembe ya aibu kufanya mambo ya OVYO namna hii, Eti CA itachangia 40 wakati hakuna hata walimu katika baadhi ya shule, sasa wanahalalisha mapishi ya hizo CA kwa shuke ambazo hazina walimu katika baadhi ya masomo?

Halafu hilo suala la kutumia CA kwenye private candidates balo sijalielewa kwa sababu watahibiwa binafsi wengi hawaendi shule, wanajisomea tu nyumbani wanafanya mtihani wa Maarifa kisha Mtihani wa K4, sasa wao CA kwa masomo yote zitatoka wapi?

Hii ni zaidi ha BALAA, Ni zaidi ya USANII na ni ZAIDI YA JANGA KWA TAIFA
 
Kaka Lengo la waliopanga haya madaraja ni ili kuwanusuru mawaziri wasiwajibike kwahiyo wamezifuta ziro kwahiyo mtu anaweza kupata F flat na asiwe na Ziro! CCM ni Majanga
 
jamani....hivi mtu akipata division five anapewa cheti.....maana nina rafiki yangu nataka kumshauli ali seat mitihani ya form four....angalau apate hata cheti... Cha form four...
 
na wewe umemaliza form four mwaka 2012? hivi mulugo tumekukosea nini ona mitoto unayotuletea kwenye jamii sasa! division five daah!!
 
mkuu umelenga kwenye shida. Siasa everywhere! Shuleni si pahala pa siasa tutaharibu kila kitu. Wabunge makini pazeni zenu na wananchi tuache unafiki tuungane kuwatetea watoto wetu wapate elimu bora vinginevyo ni majanga. Hivi,, hawa wa div.5 watapelekwa ualimu siyo?
siasa haiepukiki ndo inatawala maisha yetu ya kila siku kuanzia barozi wako haidi raisi wako anatoka na hiyo siasa hivyo hatunabudi kuikubali.
Kutokana na mchanganuo wa madaraja hayo matano na mpangilio wa alama za ufaulu hakuna tatizo uko sawa tu
sema wengi tunakuwa waoga kupokea madiliko.
 
na wewe umemaliza form four mwaka 2012? hivi mulugo tumekukosea nini ona mitoto unayotuletea kwenye jamii sasa! division five daah!!

Mulugo Mulugo, Kikwete Kikwete, mnaandika historia ambayo haitafutika, tena kwa mabaya. Kikwete unamchagua mtu wa elimu ya ku-unga unga aingie kwenye academic excellence arena!
 
Back
Top Bottom