mr. opera
New Member
- Oct 31, 2013
- 3
- 0
Kufuatia serikali kutangaza viwango vipya vya alama za ufaulu kwa shule za sekondari, ni ishara ya serikali kushindwa yafuatayo;
1. Serikali imeshindwa kukabiliana na wimbi la kufeli kwa wanafunzi wa sekondari
2. Serikali imeshindwa kuboresha shule za kata kua katika viwango bora vya utoaji wa elimu,
3. Serikali imeshindwa kusikiliza na kuthamini madai na maslahi ya walimu,
4. Haya ni matokeo ya serikali kutothamini na kupuuza maoni ya wadau mbalimbali kuhusu masuala elimu.
Si sahihi hata kidogo; kama serikali inaona kurahisisha ufaulu ndio njia bora ya kuboresha elimu basi ijue kwamba imepoteza uelekeo, na kwa kufanya hivi tusitegemee kupata taifa bora lenye nguvu na wasomi wa kutusaidia kuondokana na umasikini.
Wito wangu kwa serikali;
*boresheni shule za kata sambamba na kuzipatia mahitaji muhimu,
*wekeni mitaala imara ya elimu,
*Walipeni mishahara mizuri walimu sambamba na kusikilizeni madai ya waalimu
hatua hii ya kubadilisha madaraja ya ufaulu ni ya mwisho kabisa,kwakuwa naamini hata kama utapanga A ni 95 had 100 kama kuna miundombinu mizuri katika elimu wanafunzi watafaulu tu