Hiyo ni movie inaendelea nimeangalia hizo data sikuamini kama kweli serikali inaweza kuamua kitu cha kuua elimu kiasi hicho!
Naunga mkono hoja. Nimeshindwa kumwelewa Mulugo anapotetea hivyo viwango eti hawajashusha lakini wameondoa tu mlundikano. Kama D ilikuwa inaanzia 35, je kuifanya ianzie 20 siyo kushusha viwango? Kama C ilikuwa inaanzia 50, je kuifanya ianzie 40 siyo kushusha viwango? Kama A ilikuwa inaanzia 81 kuifanya ianzie 75 siyo kushusha viwango? Kwa mujibu wa matokeo ya majaribio ya mfumo huo, kama yangetumika kwa matokeo ya K4 mwaka 2012 ufaulu ungekuwa 93%. Sasa kama bila kufanya mtihani mwingine wizara inaweza kucheza na viwango vya ufaulu na ukapanda toka asilimia 43 hadi 93, je huko siyo kushusha viwango vya ufaulu? Ona jedwali la majaribio
AINA YA WATAHINIWA MWAKA DARAJA ME % KE % WOTE % YA WOTE S 2012 I 6,148 3.01 2859 1.7 9,007 2.42 S 2012 II 17,617 8.63 7940 4.73 25,557 6.87 S 2012 III 35,678 17.48 19920 11.87 55,598 14.95 S 2012 I - III 59,443 29.12 30719 18.3 90,162 24.24 S 2012 IV 132,687 65.01 125782 74.95 258,469 69.5 S 2012 I - IV 192,130 94.13 156501 93.25 348,631 93.74 S 2012 11,962 5.86 11323 6.75 23,285 6.26 Analysis ya Wizara kuhusu matokeo ya majaribio ya mfumo mpya Takwimu katika Jedwali la 3 zimeonesha kuwa kwa kutumia muundo mpya watahiniwa ambao wangefaulu kwa ufaulu
mzuri yaani wale walio kati ya Daraja la I-III ni asilimia 21.22 na wale watakaopata ufaulu hafifu yaani Daraja la IV ni asilimia 70.04. Wanafunzi ambao wangepata ufaulu usioridhisha kabisa ni asilimia 6.26. Kwa mantiki hii mfumo huu uliowazi kwa wote hauna athari ya kuwafanya hata wale ambao hawana uwezo wa kielimu waonekane wana ufaulu mzuri. Hii ina maana bado Taifa linawajibika kuwekeza nguvu zake katika kuimarisha elimu ya sekondari ili idadi kubwa ya wanafunzi iondoke kutoka ufaulu dhaifu na usioridhisha na kuingia kundi la wale wenye ufaulu mzuri na zaidi. Lakini pia ubora wa mfumo ni matokeo ya vitu vingi ikiwemo usimamizi mzuri, umakini na uadilifu ili mfumo uwe na tija