tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,838
- 18,250
Ndugu watanzania, tuamke kumekucha! Tuamke tupiganie haki yetu ya msingi ya kupewa elimu bora na sio bora elimu. Leo wakati katibu mtendaji wa NECTA anawasilisha matokeo nimemsikiliza kwa makini sana. Amedai eti ufaulu wa mwaka 2023 umepanda kwa 0.87% ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2022.
Baada ya kusikiliza matokeo yaliyowasilishwa, nimeingia kwenye mtandao kujiridhisha kama alichosema katibu kinaakisi kupanda ufaulu au la. Nimegundua serikali imejificha kwenye kichaka cha siasa ndio maana kila siku mambo yanaenda ovyo lakini watanzania hawajali. Wamekaa kimya kama mabubu kana kwamba kila kitu kiko sawa.
Serikali inaficha uovu wake wa kuua elimu ya watanzania kwenye siasa za majitaka. Zamani NECTA walikuwa hawatoi matokeo ya jumla na ya kipuuzi kama haya wanayotoa sasa. Walilazmishwa kubadili mfumo kisiasa ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Kwa mfano, siku za nyuma wanafunzi walikuwa wanachaguliwa kuingia kidato cha kwanza kwa kuangalia jumla ya alama ambazo kila mwanafunzi amepata.
Kipindi hicho nafasi za sekondari zilikuwa chache, hivyo ushindani ulikuwa mkubwa. Pia mitihani ilikuwa migumu sana. Kwa mfano, kwa upande wa shule za msingi kulikuwa na mkusanyiko wa masomo matatu tu yaani Lugha, Hisabati na Maarifa, na kila somo lilichukua jumla ya alama 50. Hivyo, jumla ya alama za juu ilikuwa 150.
Haikuwa ajabu mwanafunzi kupata alama 145 akakosa nafasi ya kwenda sekondari. Siku hizi utakuta mwanafunzi kapata alama 11 lakini anachaguliwa kwenda sekondari kwa kisingizio cha kwamba amepata wastani wa D! Hii ni nchi ya ajabu sana. Ndio maana serikali imefanya kila njia kuongeza mafumbo kwenye elimu ili kuficha udhaifu wa kushuka kwa kiwango cha elimu na ufaulu katika nchi hii.
Nikirejea kwenye hoja yangu ya msingi, ukiangalia matokeo ya shule za serikali (shule za kata) ambazo NECTA inasema ufaulu wake umepanda, ni ubatili mtupu. Nimejaribu kuchukua shule chache kama mfano. Hebu tazama hiki kichekesho, ucheke uongeze siku za kuishi:
Ukihesabu idadi ya wanafunzi walioangukia kwenye ufaulu wa daraja la nne ni zaidi ya 95% ya wanafunzi wote nchi nzima. Kumbe ufauulu ulioongezeka ni wa divisheni foo! Sote tunafahamu kuwa ufaulu wa divisheni foo hauna maana yoyote. Mwanafunzi aliyepata divisheni foo hastahili hata kupewa cheti. Akafanyie nini hicho cheti? Hakina maana yoyote ile.
Hivi serikali sikivu ya CCM mnamdanganya nani na haya matokeo yenu ya mchongo ambayo kila mwaka ufaulu wake unapanda? Haya ndiyo maajabu ya serikali hii ya kusadikika iliyojaa hadaa, usanii na unafiki kila mahali.
Pia soma: Wanne kati ya watano kidato cha pili Temeke wapata daraja la nne na sifuri