Serikali yatangaza viwango vipya vya alama za ufaulu elimu ya sekondari

Kama usimamizi utakuwa mzuri basi hiyo itakuwa na faida kubwa kwa wanafunzi kwasababu wanafunzi wanatahiniwa kwa masaa 3 tu na hiyo ni 100%. Kwakweli haiwezekani usome kwa miaka 4 au 2 halafu 100% itoke kwa masaa 3.
Hofu yangu ni kwamba usimamizi kama utakuwa sio mzuri basi elimu kwishnei

,,,,ni kweli
 
Jamani jamani watanzania sijui tunaelekea wapi? Viwango vya ufaulu vinashushwa kwa kiwango kikubwa hivyo? Ili iweje? Tena hiyo division 5 ndio inatia aibu zaidi!
 
Habarini wana JF.
Nimejiuliza sana kisha nikakuta jibu nalopata linanichekesha.
Kwahiyo kuanzia sasa ukipata

Physics - 0
Chemistry - 0
Maths -0
.........-0
.........-0




Kiswahili-0
Hapo unaufaulu hafifu sana au division 5.
KWELI KIDUMU CHAMA............................
 
Cha msingi ni kuboresha mfumo wa elimu -- Mitaala bora, vitabu vipatikane wa wingi hasa shule za serikali, maabara, walimu walipeni vizuri ili walio na uwezo waweze kusomea kazi hiyo, wekeni mazingira mazuri ya mwanafunzi kusoma hasa kwenye shule za serikali za kata -- hii ya kupunguza alama za ufaulu ni kuwahadaa watoto wa wazazi wao.
 
Jamani jamani watanzania sijui tunaelekea wapi? Viwango vya ufaulu vinashushwa kwa kiwango kikubwa hivyo? Ili iweje? Tena hiyo division 5 ndio inatia aibu zaidi!


​jamani hamuoni kama inasaidia....miaka minne ni heli upate kitu kuliko kukosaa
 
jamani....hivi mtu akipata division five anapewa cheti.....maana nina rafiki yangu nataka kumshauli ali seat mitihani ya form four....angalau apate hata cheti... Cha form four...

..........DUUH!!! hivi what is it UNASHAULI ALISEAT and UNAMSHAURI .... WHAT IS IT WITH OUR KISWAHILI JAMANI ..............
 
Nimepata update za hayo madaraja ni hvi.....
A 75-100
BPLUS 60-74
B 50-59
C40-49
D30-39
E20-29
F0-19
NA DIVISION ZITAKUWA HIVI...
POINT 7-17 div 1
point 18-24 div 2
point 25-31 div 3
point 32-47 div 4
point 47-48div v

source wizara ya elimu
Duh kwel elimu ya bongo ni noma bora ata ce 2lio soma miaka iyo ila cjui apo
 
Naanza kuelewa kwa nini Nyerere alikuwa hataki hata kidogo kuona Kikwete anakuwa Rais..haya ndo matunda ya ubishi wa watanzania...itawekwe mapka division 7
 
Div 5 a.k.a division mulugo,yangu macho na poleni wadogo zangu kwa huu mkakati wa kuwapanikisha mfeli kwa wale mnaotarajia kuanza mitihani jumatatu,kila la kheri mpambane
 
Hivi mtu aliyepata marks 0 - 19 unamwambiaje kuwa ana ufaulu usioridhisha? Hapo amefaulu nini sasa? Kwenye "0" kuna kufaulu kweli? Kuna maamuzi yanakera na kusikitisha sana! Yaani badala ya kuboresha elimu na mazingira ya upatikanaji wa elimu iliyobora watu (tena wanaojiita wasomi) wanakuja na visuluhisho vya kijinga! Shame!
 
Nikirudi O'level napiga A+ aisee, namshauri apunguze na viwango vya ufaulu kwa VETA. Sababu
A:81-100
B:71-80
C:61-70
D:50-60
F:00-49
 
mie kilichoniacha hoi ni B kuanzia 50. that means mwanafunzi akipata 50 katika masomo saba manaake ana div 1.7!! oow what a joke!!
 
Back
Top Bottom