Serikali yakanusha 'kujiuzulu' kwa Magufuli

Nilishalisema hili na narudia tena. Nitamwamini Magufuri siku akitekeleza azma yake ya bomoa bomoa. Mbali na hivyo atabaki kama msanii kwa namna alivyo bosi wake.
Hii si mara ya kwanza kuweka X kwenye majumba. Lakini hakuna linalofanyika. Sasa kama kweli anakusudia kufanya kazi basi avunje tuone. Naona ni usanii mwingine wa aina yake uko kazini!!!! Na mavuno yake ndio haya ya kudhalilishwa na bosi wake.
Sasa yeye avunje ili uone boss wake atachukua hatua gani. Waache usanii kwenye kazi za umma. Muda na resources walizotumia kuweka hizo X na wasibomoe nyumba itakuwa vichekesho vingine vya mwaka!!!!
 
Pinda ni Waziri Mkuu na Bosi wa Magufuri mnapaswa kujua hilo, mnatetea upuuzi bila kujua lolote; Magufuri hawezi kujiuzulu kwasababu Bosi wake kamzua hasifanye ujinga wa kuonea Watanzania bila kufuata utaratibu, kaambiwa mara kadhaa ila anataka sifa kwasababu anajua wengi ni wapuuzi na hawachambui mambo kiupana, kama wanamtete humu akajifanya kuendelea, njia pekee ilikuwa ni kumfokea ikiwezekana kumfukuza kazi, Pinda alimkemea kistaarabu sana, kama mimi angekiona cha moto.

Hawezi kujiuzulu ingawa anapenda sifa hizo kwasababu kuu moja, hana pa kwenda, wezi wenzake wa CCM wanamjua fika, wanajua jinsi anavyoiba na wanajua weakness zake zote wanajua alivyoiba awamu ya tatu (3), wanajua alivyoiba na kufanya biashara za samaki na kujifanya kutangaza kuwakamata wachache walioshindana dau, wanajua jinsi ya kumvua nguo na kumuanika uchi dk.1/60; hawezi kama kuna mtu anajidanganya hivyo aendelee kujidanganya na kujipa moyo days are counting.

Pili hamna chama kilicho makini kinaweza kumkubali mtu kama Magafuri, labda kama kinataka kufa mara moja, huo ndio ukweli na utaendelea kubaki na kusimama daima.

Kama hujui kufa chungulia kifo, Magufuri ni bomu kuliko Mrema - TLP, Bomu kuliko Maalim - CUF, wanacho mpendea CCM ni kufanya any risk task without analysis issue za Magufuri zikiibuka ni Jela Direct, kwasababu zilifanywa na Bulldozer yaani bila kutumia akili, ndio maana Mzee Kikwete alimsamehe issue ya kuuza nyumba maana Jela nje nje wala huangaiki kutafuta evidence zipo openly; ndio maana wanamwita Bulldozer yaani mashine inayotumian nguvu nyingi kuliko akili.

Hii hadhiti ya kilevi kuwa anatekeleza sheria ni utoto wa watu wasiojua maana ya sheria
 
Pinda ni Waziri Mkuu na Bosi wa Magufuri mnapaswa kujua hilo, mnatetea upuuzi bila kujua lolote; Magufuri hawezi kujiuzulu kwasababu Bosi wake kamzua hasifanye ujinga wa kuonea Watanzania bila kufuata utaratibu, kaambiwa mara kadhaa ila anataka sifa kwasababu anajua wengi ni wapuuzi na hawachambui mambo kiupana, .......

Hii hadhiti ya kilevi kuwa anatekeleza sheria ni utoto wa watu wasiojua maana ya sheria
Muungwana Arafat hapa umenena. Sijui kwa nini watu wanampapatikia huyu bwana wakati miaka yote aliyokuwa waziri hakuna jambo lolote analoweza akaonyesha kuwa amelifanya ambalo ni zuri kwa Taifa.

Badala ya akina Pinda kumsubiri Magufuli atangaze kujiuzulu, ingekuwa vema wakamfukuza kazi kwa kutoa maamuzi yasiyozingatia madhara kwa mashirika ya umma na kwa wananchi kwa ujumla.
 

Mhhh jamani tujitahidi kuandika kiswahili fasaha, hatusemi "Unamulaumu" bali unamlaumu. Pia hatusemi "Kujihuzuru" bali Kujiudhuru.

Aliyeuziwa cheni katoa noti bandia na aliyeuza cheni kauza cheni ya bandia, hii ni ngoma droo!
 
Alikuwa anapima upepo tu,Hakuna wazir wa Ccm mwenye uzalendo wa kweli,Magufuli anataka sifa tu.HANA LOLOTE

Anataka sifa? Kwa kujiuzulu? Sifa anayotaka DR Magufri ni kufanya kazi, full stop. Sasa kazi amesimamishwa na mkubwa wake sasa atake sifa gani tena ktk hali hiyo? Unajua hata sisi tunatoa mawazo yetu kama Pinda, au?
 
Aliyeuziwa cheni katoa noti bandia na aliyeuza cheni kauza cheni ya bandia, hii ni ngoma droo!
Inanikumbushia stori moja kuhusiana na mtalii wa kitaliano ambayue baada ya kusindikizwa airport na changu,wakati wa kuagana,Mtaliani akamwambia yule changudoa "Dollaro fekino" na yule changudoa alipogunduwa kaachiwa dola feki na Mtaliani,akamwambia mtaliani "Gonorreano gerentino" hah ha ha!Yani ngoma droo kwasababu amemguarantee kuwa atakuwa na yeye kamwambukizia gonorrea!
 
hizo ni longo longo tu kwanini asiongee mwenyewe Dr magufuli?????????? mmesha mchkachua ninyi na mme mdhalilisha sana hatuja ipenda hiyooooooo >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>.
 
Muungwana Arafat hapa umenena. Sijui kwa nini watu wanampapatikia huyu bwana wakati miaka yote aliyokuwa waziri hakuna jambo lolote analoweza akaonyesha kuwa amelifanya ambalo ni zuri kwa Taifa.

Badala ya akina Pinda kumsubiri Magufuli atangaze kujiuzulu, ingekuwa vema wakamfukuza kazi kwa kutoa maamuzi yasiyozingatia madhara kwa mashirika ya umma na kwa wananchi kwa ujumla.

Siasa za Tanzania ni kama kichwa cha mwenda wazimu, kuna wakati ukisikiliza watu na kusoma michango ya Watanzania unaweza kulia, maana watu walio wengi hajui lolote, kabla Mwl hajafariki ili kuwa nafuu, alijua raia wake hawajui lolote wanahitaji kufanyiwa kila kitu ili wasipotee, hivyo Mzee Nyerere alikuwa kidete katika kusaidia kung'amua nani hafai na nani anafaa.

Toka alivyo fariki Mwl ni hatari sana; Kama alivyo Magufuri ndivyo alivyo kuwa Kikwete 2005; Kikwete alikuwa bomu tulijaribu kukataa lakini wajinga na wapumbavu walikuwa wengi kuliko werevu, hivyo alishinda tena kwa kishindo kikubwa sana, ulikuwa ukijaribu kuuliza kafanya nini na robustness yake kama kawaida wapumbavu utumia nguvu kuliko hoja walitushinda kwa nguvu, mimi ndio maana huwa simlaumu Kikwete hata siku moja naamini katika kumpa muda amalize ungwe yake maana alijulikana hatoweza hata kabla, sasa kama tulimchagua, ina maana tulikubalia na udhaifu wake tusilalamike, tumpe muda. Leo hii kuna watu wanajitokeza adharani kutetea upuuzi wa huyu Bwana kuwa anatete sheria sijui sheria ya nchni gani hiyo, watu hawajui hata sheria swala la sheria ni la kitaalam siyo siasa.

Mjue kuwa maumivu tunayo yapata kutokana na watawala ni Ujinga wetu kutokuwa makini katika kuchambua wagombea, tukiendelea hivi tutaendela kuumia hadi kiama maana pia ni Upuuzi kupiga kura kumchagua Mtu hasiyefaa wewe mwenyewe alafu tena uende barabarani kupinga wakati hukutumia vyema kura yako.

Huu ni wakati wa kutafakari sana, na kuchambua watu kwa umakini siyo Ukabila, Udini wala Ukanda pia tuwahukumu watu kwa haki tuweke mizani mezani siyo ushabiki wa Mpira bila kujua nyuma ya biashara ya mpira kuna nini?
 
- Damage is done, ni ujumbe mzito tu kwa Magufuli kwamba asifikirie 2015 atakuwa peke yake kwenye ulingo wa kaya ha! ha! fumbo mfumbie mjinga!, tulisang'amua siku nyingi sana!

FMeS!
 
Hana lolote huyu alikua ana beep tuu ,aone kombora lake lina nguvu gani, alijua hata akiandika hiyo barua kwa kipindi hiki haiwezekani kukubalika .
Kimaadili ya uongozi sijui imekaaje, ila Pinda alipo ongea sikuona kibaya zaidi alichokisema,zaidi niliona kama ali msifu Maghufuli kama Mchapa kazi na hana mchezo, ila yeye alijaribu kupunguza nguvu ka kuwapa wananchi elimu zaidi ya kile kinacho taka fanywa na serikali.
 
Huu ni wakati wa kutafakari sana, na kuchambua watu kwa umakini siyo Ukabila, Udini wala Ukanda pia tuwahukumu watu kwa haki tuweke mizani mezani siyo ushabiki wa Mpira bila kujua nyuma ya biashara ya mpira kuna nini?

Hivi vya ukabila, udini na ukanda naona ndio vitu vya kuangalia sana maana kuna wajinga wengi ambao huko ndiko walikoegemea. Ukingalia maamuzi ya Kikwete anayoyatangaza mengi ni ya kujitafutia umaarufu tu.

Kwa hiyo hawa wote wenye maamuzi ya kisifa-sifa kama Magufuli hawafai kabisa kukaribishwa kugombea uraisi na ndio watu ambao Nyerere alikuwa hawataki.
 
:smash::embarassed2::hatari::ballchain::washing::focus: sineme ya pono :juggle::juggle::crutch::tongue::embarassed2: :focus::hatari::hatari:
 
<p>
<font size="3"><font color="navy"><b>Hivi vya ukabila, udini na ukanda naona ndio vitu vya kuangalia sana maana kuna wajinga wengi ambao huko ndiko walikoegemea. Ukingalia maamuzi ya Kikwete anayoyatangaza mengi ni ya kujitafutia umaarufu tu.</b></font></font></p>
<p>&nbsp;</p>
<p><font size="3"><font color="navy"><b>Kwa hiyo hawa wote wenye maamuzi ya kisifa-sifa kama Magufuli hawafai kabisa kukaribishwa kugombea uraisi na ndio watu ambao Nyerere alikuwa hawataki.</b></font></font>
</p> NDIO. MAANA NYERERE ALITAKA WATU WASIO NA SIFA KAMA MKWERE. VERY GOOD. NDIO MAANA SIKU ILE YA KIKAO NYERERE ALIMKATAA MKAPA AKAMKUBARI KIKWETE.
<p>&nbsp;</p>
 
Hivi vya ukabila, udini na ukanda naona ndio vitu vya kuangalia sana maana kuna wajinga wengi ambao huko ndiko walikoegemea. Ukingalia maamuzi ya Kikwete anayoyatangaza mengi ni ya kujitafutia umaarufu tu.

Kwa hiyo hawa wote wenye maamuzi ya kisifa-sifa kama Magufuli hawafai kabisa kukaribishwa kugombea uraisi na ndio watu ambao Nyerere alikuwa hawataki.

Nyerere alikuwa makini, hakuwa mtu wa kuendeshwa na wapenda sifa, watanzania walimshangaa katika kuibua viongozi mara zote walipo fikiri kusiki jina la mpenda sifa fulani Mwl aliibuka na jina ambalo hata halijunikani vichwani mwa wengi. Hii ilikuwa hata kwa kada ya Watendaji wakuu kama Mkatibu wakuu, Wakurugenzi, Wakuu wa vyombo vya Dola nk.

Siku hizi watu wanamjua IGP ajae kabla hata Mamlaka ya uteuzi haijaingia madarakani, hivyo hivyo kwa CDF, Mkuu wa UWT, Wakurugenzi nk. unaweza kukutana na mtu akakwambia nasubiria kuwa Mkurugenzi au Katibu mkuu kiongozi soon.

Watu wanasubiri nafasi zao za RC ndio maana utasikia kila siku wanauliza mbona Rais anachelewa kutangaza majina ya RC's wanajulikana, Wanasiasa wametusoma sawasawa wanatujua Watanzania uwezo wetu wa kuchambua na tamaa zetu za kupewa hongo wakati wa Uchaguzi. Kuna mtu anaweza kujua kwanini Mkono kila mara hana mgombea hata wa upinzani? Kwanini wakina MO wanashinda bila shaka huko Singida?, Kama RA hafai na mchafu kwa Umma wa Tanzania kwanini anashinda kwa kishindo huko Igunga pamoja na kelele zote zinazopigwa? Zaidi ya wa 90% ya wapiga debe wa Pombe hawawezi kujibu hayo maswali bila kupindisha.

Katika wimbo wa Taifa tunatakiwa kubadilisha kile kipengere cha "Mungu Ibariki Tanzania" iwe "Mungu Isaidie Tanzania" wananchni wengi wanahitaji kusaidiwa hawajijui hata kidogo.
 
Hana lolote huyu alikua ana beep tuu ,aone kombora lake lina nguvu gani, alijua hata akiandika hiyo barua kwa kipindi hiki haiwezekani kukubalika .
Kimaadili ya uongozi sijui imekaaje, ila Pinda alipo ongea sikuona kibaya zaidi alichokisema,zaidi niliona kama ali msifu Maghufuli kama Mchapa kazi na hana mchezo, ila yeye alijaribu kupunguza nguvu ka kuwapa wananchi elimu zaidi ya kile kinacho taka fanywa na serikali.

We ulimsikiliza Pinda nashukuru sana, lakini ujue wasiosikiliza na kuropoka bila kujua maana ni wengi kuliko wanasikiliza kwa makini na kuelewa "Context" ya jambo husika na kujua maana yake; hivyo wanasiasa Watanzani hawakuhitaji mtu kama wewe hata kidogo.

Hawa kuhitaji siyo kwasababu tu kuwa utachambua na kuainisha pumba zao, la! hapana; hawakuhitaji kwasabasabu Siasa ni wingi wa kura (Watu), hivyo upande wa pili (yaani wale wasio sikiliza kwa makini na kuelewa) katika kupiga kura lazima watashinda tu!
 
Back
Top Bottom