Rais Mwinyi achukizwa na tabia ya viongozi kujiuzulu kimya kimya

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Kiongozi akitaka kujiuzulu anapaswa kumpa taarifa Boss wake kwanza badala ya kukurupuka kwenda kutangaza kwenye Vyombo vya Habari huku akitoboa siri kuwa hata yeye akiwa Waziri wa Ulinzi aliwahi kumwandikia barua ya kujiuzulu Rais Mstaafu Kikwete baada ya mabomu ya Gongolamboto lakini alimwambia ile ni ajali na hana sababu ya kijiuzulu.

Akiongea leo February 1, 2024 wakati akiwaapisha Mawaziri wapya wateule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ikulu Zanzibar Rais Mwinyi amesema “Suala la kujiuzulu Waziri ni suala ambalo si geni ni moja katika njia ya kuwajibika, katika Wizara kunaweza kukawa na mazingira mawili ya Waziri kujiuzulu, mazingira ya kwanza yanaweza kuwa katika Sekta yako inayoisimamia kumetokea tatizo au changamoto na wewe kama Waziri unawajibika kwa changamoto ile, si lazima uwe umeifanya wewe lakini unawajibika kwasababu wewe ndio Msimamizi wa Sekta”

“Nimekuwa nasikia kwenye mitandao kuwa Zanzibar hajawahi kujiuzulu Mtu, si kweli, wakati wa ajali ya meli kuna Waziri alijiuzulu na alijiuzulu si kwasababu alisababisha
yeye ile ajali kawajibika kwasababu ni Sekta anayoisimamia na kilichotokea ilikuwa ni uzembe na si ajali”

“Ilipotokea ajali ya mabomu kule gongo la mboto, Mimi nikiwa Waziri wa ulinzi nilipeleka ujumbe kwa Rais wangu wakati huo Mhe.Kikwete nikimtaka aliridhie nijiuzulu lakini sikukurupuka kwenda kwenye Vyombo vya Habari nikatangaza kwamba nimejiuzulu sio utaratibu, utaratibu unataka umwambie aliyekuteua akubali ndio ukatangaze kujiuzulu, Mhe.Kikwete akasema hii ni ajali huna sababu ya kujiuzulu, hakuna Mtu aliyesikia kama nilitaka kujiuzulu leo nasema hili hadharani lakini sikuwahi kulisema”

Kauli ya Rais Mwinyi inakuja siku chache baada ya aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohammed Said, kujitokeza kwenye Vyombo vya Habari na kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya Uwaziri akisema mazingira ya kutekeleza jukumu hilo yamekuwa magumu.

Source - MillardAyo
 
Kumbe yule Waziri aliyejiuzulu kule Zenji alikurupuka bila hata wakubwa zake kujua kwamba anataka Kujiuzulu.

Sasa Dr.Mwinyi amewataka Viongozi kutoa taarifa Kwa mamlaka ya Uteuzi kabla ya kukirupukia kutangaza Kujiuzulu.

My Take
Naunga mkono hoja Kwa sababu next time hakuna mtu atakuamini tena.

====

Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Kiongozi akitaka kujiuzulu anapaswa kumpa taarifa Boss wake kwanza badala ya kukurupuka kwenda kutangaza kwenye Vyombo vya Habari huku akitoboa siri kuwa hata yeye akiwa Waziri wa Ulinzi aliwahi kumwandikia barua ya kujiuzulu Rais Mstaafu Kikwete baada ya mabomu ya Gongolamboto lakini alimwambia ile ni ajali na hana sababu ya kijiuzulu.

Akiongea leo February 1, 2024 wakati akiwaapisha Mawaziri wapya wateule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ikulu Zanzibar Rais Mwinyi amesema “Suala la kujiuzulu Waziri ni suala ambalo si geni ni moja katika njia ya kuwajibika, katika Wizara kunaweza kukawa na mazingira mawili ya Waziri kujiuzulu, mazingira ya kwanza yanaweza kuwa katika Sekta yako inayoisimamia kumetokea tatizo au changamoto na wewe kama Waziri unawajibika kwa changamoto ile, si lazima uwe umeifanya wewe lakini unawajibika kwasababu wewe ndio Msimamizi wa Sekta”

“Nimekuwa nasikia kwenye mitandao kuwa Zanzibar hajawahi kujiuzulu Mtu, si kweli, wakati wa ajali ya meli kuna Waziri alijiuzulu na alijiuzulu si kwasababu alisababisha
yeye ile ajali kawajibika kwasababu ni Sekta anayoisimamia na kilichotokea ilikuwa ni uzembe na si ajali”

“Ilipotokea ajali ya mabomu kule gongo la mboto, Mimi nikiwa Waziri wa ulinzi nilipeleka ujumbe kwa Rais wangu wakati huo Mhe.Kikwete nikimtaka aliridhie nijiuzulu lakini sikukurupuka kwenda kwenye Vyombo vya Habari nikatangaza kwamba nimejiuzulu sio utaratibu, utaratibu unataka umwambie aliyekuteua akubali ndio ukatangaze kujiuzulu, Mhe.Kikwete akasema hii ni ajali huna sababu ya kujiuzulu, hakuna Mtu aliyesikia kama nilitaka kujiuzulu leo nasema hili hadharani lakini sikuwahi kulisema”

Kauli ya Rais Mwinyi inakuja siku chache baada ya aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohammed Said, kujitokeza kwenye Vyombo vya Habari na kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya Uwaziri akisema mazingira ya kutekeleza jukumu hilo yamekuwa magumu. #MillardAyoUPDATES
 
Swala la wamasai kubaguliwa na wamatumbi wenzao kalizungumziaje otherwise hayo mengine awaambie hao wateule wake wakati anawateua sisi hayatuhusu.

Tunataka kujua hatma ya watanganyika wenzetu huko Zanzibar ache unafiki wake.
 
Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Kiongozi akitaka kujiuzulu anapaswa kumpa taarifa Boss wake kwanza badala ya kukurupuka kwenda kutangaza kwenye Vyombo vya Habari huku akitoboa siri kuwa hata yeye akiwa Waziri wa Ulinzi aliwahi kumwandikia barua ya kujiuzulu Rais Mstaafu Kikwete baada ya mabomu ya Gongolamboto lakini alimwambia ile ni ajali na hana sababu ya kijiuzulu.

Akiongea leo February 1, 2024 wakati akiwaapisha Mawaziri wapya wateule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ikulu Zanzibar Rais Mwinyi amesema “Suala la kujiuzulu Waziri ni suala ambalo si geni ni moja katika njia ya kuwajibika, katika Wizara kunaweza kukawa na mazingira mawili ya Waziri kujiuzulu, mazingira ya kwanza yanaweza kuwa katika Sekta yako inayoisimamia kumetokea tatizo au changamoto na wewe kama Waziri unawajibika kwa changamoto ile, si lazima uwe umeifanya wewe lakini unawajibika kwasababu wewe ndio Msimamizi wa Sekta”

“Nimekuwa nasikia kwenye mitandao kuwa Zanzibar hajawahi kujiuzulu Mtu, si kweli, wakati wa ajali ya meli kuna Waziri alijiuzulu na alijiuzulu si kwasababu alisababisha
yeye ile ajali kawajibika kwasababu ni Sekta anayoisimamia na kilichotokea ilikuwa ni uzembe na si ajali”

“Ilipotokea ajali ya mabomu kule gongo la mboto, Mimi nikiwa Waziri wa ulinzi nilipeleka ujumbe kwa Rais wangu wakati huo Mhe.Kikwete nikimtaka aliridhie nijiuzulu lakini sikukurupuka kwenda kwenye Vyombo vya Habari nikatangaza kwamba nimejiuzulu sio utaratibu, utaratibu unataka umwambie aliyekuteua akubali ndio ukatangaze kujiuzulu, Mhe.Kikwete akasema hii ni ajali huna sababu ya kujiuzulu, hakuna Mtu aliyesikia kama nilitaka kujiuzulu leo nasema hili hadharani lakini sikuwahi kulisema”

Kauli ya Rais Mwinyi inakuja siku chache baada ya aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohammed Said, kujitokeza kwenye Vyombo vya Habari na kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya Uwaziri akisema mazingira ya kutekeleza jukumu hilo yamekuwa magumu.

Source - MillardAyo
Ukitaka kujiuzulu kimya kimya ukakataliwa Umma utajuaje dhamira yako?
 
Ukitaka kujiuzulu upeleke barua kwa boss wako kivip? Maana yake unataka kupima kama unapaswa kuendelea ama huwezi kuendelea jibu nikuamua mwenyewe huwezi kutaka kujinyoga harafu ukaomba mtu akushikie kamba.
 
Kwahiyo Mwinyi anataka kusema nini? Kwamba Mh Simai alikuwa na Baa au alikuwa na kampuni ya kuagiza vilevi ?
Ila hii ni mipasho na unprofessional kabisa kwa mtu mkubwa kama Rais kuongea namna hii, kwanza jambo lenyewe lilishapita na watu walishalisahau hiyo kazi ilipaswa kufanywa na watu aina ya kina Makonda vichwa vibovu ambaye hata akitamka jambo watu hawalitilii maanani.
 
Kiukweli haileti maana ya kujiuzulu, mtu akiamua kuacha aache tu, cause hata wakati wa kumteua hukumshirikisha kwamba nataka uwe waziri, so why yeye akutaarifu kwanza?
Ingekuwa mteuaji anamtaarifu mteuliwa kuna wengi wangekataa teuzi kabisa, hasa kipindi cha Magufuli
 
Haikuwa rahisi kujiuzulu, ukitekeleza wajibu wako afu unapokutana na vikwazo vinavyopaswa kutatuliwa na mamlaka iliyokupa dhamana afu isikusapoti lzm uamue kama maskini
 
Back
Top Bottom