Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,503
- 113,614
Wanabodi,
Tanzania tuko hapa tulipo kwenye lindi la umasikini uliotopea kutokana na kukosekana viongozi wa kutosha wenye boldness ya kuchukua maamuzi magumu!. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, John Pombe Magufuli, na huyu dogo Paul Makonda, ni miongoni wa watu wenye boldness ninayoizungumzia hapa!
Ikitokea umelalamikia kuhusu kukosekana kwa boldness kwa viongozi wetu, kwenye issues za uwajibikaji Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma halafu wakajitokeza viongozi vijana ma bold wa viwango hivyo, huwezi kukaa kimya, lazima ujitokeze, upongeze!
Kitendo cha Kujiuzulu kwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed Said ambaye pia ni mwakilishi wa jimbo la Tunguu, Zanzibar, ni kitendo cha ushujaa mkubwa uitwao boldness ya cheo ni dhamana kama alivyofanya Baba wa taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alivyojiuzulu Uwaziri Mkuu wa Tanganyika. Mhe. Simai anastahili pongezi na kupigiwa mfano badala ya kusakamwa, kusimangwa na kukaliwa vikao!
1. Kitendo kilichofanywa na Mhe. Simai, cha kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri, bila kuwepo kwa kashfa yoyote, wala shinikizo lolote, ni kitendo cha ushujaa wa hali ya juu ambacho kinapaswa kupigiwa mfano na wanasiasa wote wa Tanzania. Badala ya Mhe. Simai kushutumiwa, kusakamwa, na kukaliwa vikao!. Mhe Simai, anapaswa kutolewa mfano wa kuwa miongoni mwa mashujaa wa taifa hili.
2. Jina la Mhe. Simai, linaingia moja kwa moja katika historia ya mashujaa wa taifa hili, kway eye kuwa ni mwanasiasa wa pili kujiuzulu wadhifa wake wa kisiasa, bila kutokea kashfa yoyote au shinikizo la nje au la ndani. Shujaa wa kwanza kujiuzulu kwa mtindo huu ni Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ile 1962
3. Kwa vile sii wengi walikuwepo enzi hizo tulipopata uhuru ile Desembe 9, 1961, japo sote tunajua shujaa wa uhuru wa Tanzania (enzi hizo Tanganyika) ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, lakini sii wengi wanafahamu kuwa Tanzania tulipopata uhuru, hatukuwa Jamuhuri, hivyo Nyerere aliyeuleta uhuru wa Tanganyika aliupokea akiwa ni Waziri Mkuu, hivyo Tanzania ilipopata uhuru wake nchi ilikuwa ikiongozwa na Waziri Mkuu, na Mwalimu Nyerere ndie alikuwa Waziri mkuu wa kwanza wa Tanyanyika.
4. Mwalimu Nyerere alidumu kwenye wadhifa huo wa Waziri Mkuu wa Tanganyika kwa kipindi cha siku 40 tuu, mnamo tarehe 20 January mwaka 1962, Mwalimu Nyerere, bila shinikizo kutoka popote kwa yeyote, aliamua kujiuzulu wadhifa wake wa Waziri Mkuu, na Rashidi Mfaume Kawawa kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu.
5. Kitendo hiki cha Mwalimu Nyerere kuiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu, bila shinikizo lolote kutoka popote, ni kitendo cha kishujaa sana, ukisikia kitu kinachoitwa boldness kwa wanasiasa, hii boldness, ni moja ya sifa muhimu sana kwa mwanasiasa kuwa nayo, Mwalimu Nyerere was bold, Mhe. Simai is bold.
6. Boldness ya aina hii, ilipaswa ionyeshwe na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa baada ya tukio la Machi 17, 2021, kwasababu yeye alikula kiapo mbele ya JPM, kwa vile rais aliyemteua hayupo, nchi imepata rais mwingine, alipaswa awe bold ajiuzulu ili bazara la mawaziri lijiuzulu, kumpa Rais Samia Fursa ya kuteua baraza lake jipya ambalo lingekula kiapo chini yake, na kama Samia alikuwa bado anamuhitaji, angemteua tena, kitu muhimu hapo ni kumpa Samia fursa ya kuteua team yake na kula kiapo chini yake, na sio kocha mpya anaingia na kuendelea na team ya zamani, hivyo viongozi wetu wamekosa boldness ya Nyerere na Simai.
7. Serikali zinaendeshwa kwa kanuni ya uwajibikaji wa pamoja , a collective responsibility, ukijiona unatofautiana na wenzako, unapaswa ama unanyamaza kimya ama unapisha kwa kujiuzulu na kukaa pembeni. Enzi za awamu ya pili ya Mzee Mwinyi, Agustino Lyatonga Mrema, akiwa Waziri wa Kazi na Naibu Waziri Mkuu, alitofautiana na kanuni ya uwajibikaji wa pamoja kwa kulipukia Bungeni kuwa hakubaliani na jambo fulani lililopitishwa ndani ya kikao cha baraza la mawaziri, Lyatonga alipaswa kujiulu pale pale baada ya kutofautia na uwajibikaji wa Pamoja na sio kuja kutapikia bungeni, hivyo alibidi kujiuzulu kwa shinikizo, lakini Simai hakujiuzulu kwa shinikizo lolote, watu wenye boldness ya aina hii ndio watu wanaohitajika kwa nchi hii kuitoa hapa ilipo kuifikisha kule inapaswa kuwa.
8. Wako viongozi wengi waliwahi kujiuzulu, kwa kuandika barua za kujiuzulu, ama kwa shinikizo baada ya kutokea kashfa kwenye wizara zao, kama ile kashfa ya mauji ya vikongwe iliyopelekea kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa Usamama Peter Siyovelwa, Kuliwahi kutokea kashfa ya Sukari, Waziri wa Biashara Iddi Simba akajiuzulu, Kulitokea kashfa ya Richmond, Waziri Mkuu, Edward Lowassa akajiuzulu. Kulitokea kashfa ya mgomo wa madaktari, Waziri wa Afya akajiuzulu.
Nikiwa Dodoma, Waziri mmoja aliitisha press conference akatapika nyongo!, nikamuuliza kwanini usijiuzulu kwanza ndipo uwashe moto?, alinigomea!. Omari Nundu: Sioni sababu ya kujiuzulu haikupita siku 2 baada ya press conference ile, Waziri na Naibu wake wote wakapigwa chini!. Angekuwa bold angekuwa shujaa!.
Wakati wa Bunge maalum la Katiba, Kiongozi mmoja wa Zanzibar akaleta za kuleta!, nikamshauri Dr. Shein Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii, hazikupita siku mbili!, mtu chali!. Ila huyu baada ya kujiunga upinzani na kula lile shavu, sasa amekuwa mtoto mzuri, na kwa vile Rais Samia ni mtu rahim wa haki bin haki, huyu jamaa ndiye anakwenda kuwa rais wa Zanzibar 2025 , na kumkabidhisha Mama Samia tuzo ya Mo Ibrahim!.
9. Wako pia viongozi waliojiuzulu kwa sababu ya matatizo ya kiafya, hapo hakuna boldness, ni circumstances kufuatia hali ya afya yako unajiona huwezi kumsaidia mteuzi hivyo unaamua kujiuzulu.
10. Spika Mhe. Job Yustino Ndugai alipotofautiana na serikali kuhusu mikopo, alipaswa awe bold apishe kuliko kuja kujiuzulu kwa aibu!, tulimshauri awe bold, aachie ngazi, kishujaa aonekane shujaa, Ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu. Je, wajua pia kuna msamaha halali wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu? Msamaha ule ni batilifu! lakini yeye alikomaa, tena nakumbuka vizuri nilimuuliza Baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama ni timamu, je, tumshauri to do "The needful?" au akomae nao, till they do him away?
akaja kuandika barua ya kujiuzulu kwa shinikizo hivyo kupanic na kuikosea, hatimaye akajiuzulu kikondoo shingo chini Msameheni bure Job Ndugai, amechanganyikiwa baada ya kuomba msamaha batilifu uliokataliwa! Barua yake ya Kujiuzulu nayo pia ni batilifu!
11. Niliwahi kuandika Makala kuhusu kokosekana wabunge wenye boldness ya aina hii ndani ya bunge letuhivyo Bunge kushindwa kuisimamia serikali kikamilifu, hata sasa ndani ya bunge letu, wabunge bold ni wa kuhesabika mmoja wao ni Mhe. Luhaga Mpina. Bunge butu linaloingiliwa na kunyamaza, linapojikomba na kujipendekeza kwa Rais, linaweza kweli kuisimamia Serikali?! na Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi? na Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali? hata Bunge hili la sasa bado linajipendekeza kwa serikali not expressly but impliedly kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kikamilifu wa kuisimamia serikali!. Serikali inapeleka madudu Bungeni, Bunge linayapitisha madudu hayo hivyo hivyo yalivyo!. Ushahidi ni IGA ya DPW ni mkataba batili na juzi wamepitisha sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba!.
12. Pia kuna kitu kinaitwa kujiuzulu na kutishia kujiuzulu, kujiuzulu ni kuamua with boldness, kujiuzulu kwa kuandika barua ya kujiuzulu na kutangaza mwenyewe kujiuzulu kisha kupeleka barua ya kujiuzulu kwa mamlaka ya uteuzi, hiki ndicho alichokifanya Mhe Simai na hii ndio boldness ninayoizungumzia,
13. Kutishia kujiuzulu ni kuandika barua ya kujiuzulu kwa mamlaka yako ya uteuzi, as if ni kuomba ruhusa ya kujiuzulu, ukikubaliwa ndipo unatangaza, wako viongozi wengi wameandika barua hizi, lakini wengine hazikukubaliwa hivyo hawakujiuzulu, ndio maana nasisitiza hii boldness iliyoonyeshwa na Mhe Simai, inapaswa ipongezwe na iwe ni ya kupigiwa mfano, hivyo badala ya kusakamwa, kusimangwa na kukaliwa vikao, Mhe. Simai apewe maua yake.
Paskali