Serikali yakanusha 'kujiuzulu' kwa Magufuli

Msimlaumu Magufuli, HUENDA AKAWA AMEZIBWA MDOMO NA BOSSI WAKE, ASIONGEE CHOCHOTE.
 
Kwanza katibu mkuu yuko chini ya waziri nilishangaa sana kuona anamjibia waziri wake na kusema magufuli hajawahi kuwa na wazo la kujiudhuru kana kwamba yeye yuko kwenye ubongo wake. Kauli za katibu mkuu zimekaa kisiasa zaidi ukweli ni kwamba bado wanambembeleza magufuli asitishe uamuzi wake ndio maana hata magufuli hajajitokeza kukanusha na akipigiwa simu na waandishi hapokei simu.
 
Wabongo wanashangaza sana, eti Magufuli anatafuta umaarufu kupitia suala la kujiuzulu, kwani yeye ndo alovujisha taarifa kwamba anajiuzuru!
 
haka kajamaa kanakuwaga strict sana kwenye bomoa bomoa mbona hakachukui hatua ya kujizungumzia Chenyewe, kako strict sana kanatakiwa kawe strict hivyo hivyo badala ya kumwachia katibu mkuu wake kumzungumzia Its Rediculous, au analinda Ugali yeye ni Interllectual anatakiwa asimame mwenyewe, kuna kamsemo cha kizungu kanasema "A STRONG MAN IS HE WHO STAND ALONE AND FACE THE REAL SITUATION" sasa nimeamini Mr. John ni Nguvu Ya SODA.
 
Jana sikupata nafasi ya kuingia ndani ya janvi maana tulikuwa na semina ya wabunifu wa majengo na wakadiliaji majenzi iliyofanyika jana Arusha. Tulikwa ukumbini mtu mmoja alinijuza kwamba ndani ya JF kulikuwa na thread ya kujiuzulu kwa Magufuli, Nilipoingia janvini asubuhi ya leo sikuiona hiyo thread, je moderator ameogopa akaiondoa? au?

Nijuze wakuu
 
SASA ni dhahiri kuwa Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, ana siri nzito kuhusiana na madai kwamba ameandika barua kwa Rais Jakaya Kikwete, akikusudia kujiuzulu.
Katika hali iliyotafsiriwa kuwa waziri huyo anaepuka kutoa mwenyewe msimamo wa kujifunga moja kwa moja kuhusu kuwa na nia ya kujiuzulu au kutojiuzulu, jana Katibu wa Wizara yake, Herbert Mrango, ndiye aliyejitokeza kukanusha taarifa zilizoandikwa na baadhi ya magazeti zilizohusu kujiuzulu kwake.
Mrango akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, alisema habari zilizoandikwa na baadhi ya magazeti: “Magufuli Ajiuzulu” au “Magufuli Azushiwa Kujiuzulu” si za kweli, huku akikataa katakata kuulizwa swali lolote kuhusu undani wa taarifa hizo zinazomhusu mkuu wake.
“Mheshimiwa waziri anaendelea na kazi zake vizuri, alikuwepo ofisini jana na leo yupo; na anaendelea na programu zake za kazi kama kawaida.
“Tunawaomba muwahakikishie wananchi kwamba Waziri Magufuli hajajiuzulu, hajawahi kuwa na wazo la kujiuzulu na hana sababu ya kujiuzulu,” alisema Mrango.
Hata waandishi walipong’ang’ania kumuuliza maswali, Mrango aliwataka wamtafute siku nyingine za kukutana kwa ajili ya maswali bali siku hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya kutoa taarifa fupi.
“Hiyo ndiyo taarifa fupi nimemaliza sihitaji maswali kwa kuwa sina majibu na kama mnataka kuuliza maswali naomba mnitafute siku nyingine tukutane kwa ajili ya hiyo, asanteni,” alisema Mrango na kunyanyuka huku akitoka nje ya ukumbi huo.
Taarifa zinadai kuwa katika majumuisho ya ziara ya Waziri Mkuu Pinda baada ya kauli hiyo mkoani Kagera , Magufuli alilazimika kueleza kuwa amefikia hatua ya kuamua kuchukua maamuzi magumu baada ya kubaini kuwa hataweza kutekeleza vema utawala wa sheria ambao umeonekana kupindishwa.
Chanzo kimoja kilicho karibu na waziri huyo kililidokeza gazeti hili kuwa alifikia uamuzi wa kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kusikitishwa na kauli iliyotolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ya kusitisha zoezi la bomoa bomoa lililokwishaanza katika baadhi ya maeneo nchini.
“Ni kweli baada ya kutolewa kauli ile kule mkoani Kagera katika kikao chetu cha majumuisho ya ziara hiyo Magufuli alisikitishwa na kauli ile ambapo aliweka bayana kuchukua maamuzi magumu hatua ambayo haikukubaliwa na viongozi waliokuwa katika ziara hiyo,” kilisema chanzo hicho.
Taarifa za kujiuzulu kwa Waziri Magufuli zimeonekana kuwashtua baadhi ya viongozi kutokana na baadhi ya watendaji kujaribu kupeleleza wananchi wamepokeaje juu ya kuzagaa kwa taarifa hizo. Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa ni kweli Magufuli alifikia uamuzi huo hata baada ya kushauriwa na viongozi mkoani humo na kuamua kuandika notisi ikiwa ni njia ya kutaka kumtikisa Waziri Pinda ambayo hajaikabidhi kwa wahusika.
 
Pinda alikosea sana. Sasa Magufuli atabaki tu kumsikiliza Pinda anasema nini kwanza? Huo kama si utumwa ni nini sasa?
 
Nilipata kusema huko nyuma,kama magufuli anataka kuendelea kuaminika kwa umma,na kama kweli anaamini kwenye uamuzi wake wa bomoabomoa,basi lazima ajiuzulu,vinginevyo hana jipya
 
Tuna safari ndefu sana ya kufiikia mabadiliko, huenda kukawa na ukweli au kusiwe na ukweli katika hili la kujiuzulu kwa Magufuli, lakini kauli rasmi ni hiyo aliyoitoa katibu mkuu ya kwamba Dr.Magufuli hakuwahi hata kuwaza kujiuzulu, na la kukataa kuulizwa maswali ni haki yake kwa sababu asingeweza kutoa majibu ya maswali yanayomhusu Magufuli zaid ya kufikisha taarifa ambayo alitumwa na bosi wake kufanya hivyo
 
kweli kaka tunasafari ndefu sana,hii nchi sijui ina viongozi wa namna gani,kwaninim pinda asinge kaa kimya na kuyajadili ndani ya vikao vyao,ama kwa kuwa mkulu wa Dr kwa hiyo anataka kumkata ngebe jamaaa

Dr jiuzuru tu waaaaaaaaaaaaaache baraza lao la ubebana,ipo siku tu mwisho utafika tumechoka
images
 
kama kweli tanzania kuna mgawanyo wa madaraka basi ni lazima Magufuli a.k.a Buldozer ajiweke pembeni kuepusha kuendelea kuingiliwa katika utendaji wake.
 
Kwanini aongee katibu mkuu wake yeye mbona yu kimya?Kuna kitu kinaendelea hapa...
 
Kwanza kwa Hili naona Kama Limechelewa ,iwe ni huzushi wa vyombo vya Habri au Tetesi lakini Kwangu mie Nilitegemea Hili Jambo Kutokea has kwa mtu kama Magufuli ambaye ni Mwanachama na wa sheria ,na mtu nayetekeleza Majukumu yake kwa misingi ya sheri ana katiba.

Kwa Kauli za Waziri Mkuu ,ni kumdhalilisha Magufuri tena kwa wapiga Kura wake .Na ata kama Magufuri atashindwa kuitendea Haki nafsi yake lakini kwa Watanzania atonekana ni mtu asiye na msimamo na mahamuzi yake.

Rai yangu kwa Magufuri ,naomba Aueleze Umma nini Maoni yake kuhusu tetesi hizi.....
 
babu chomoka tuuuuu wasikutishe, jichukulie uamuzi peke yako kama ambavyo pinda alitoa tamko tena jimboni kwako. NAMSHAURI MAGUFULI AENDE MPANDA KWENYE JIMBO LA Mh . PINDA ATANGAZIE KUJIUZULU HUKOHUKO AWAELEZE KUWA ALIMDHALILISHA. ITAKUWA SAFI HIYO.
 
Kanyanyasika sana! Ukweli ni kwamba hakuna Mabasi yaendayo kasi ni danganya toto za ccm. Karibu CHADEMA dr huku tuaongea kwa thumuni mwanzo mwisho! Unakaa kwenye Chama cha viwete hao wao wakingenga hata robo km inatangazwa nch nzima
 
Kwanza kwa Hili naona Kama Limechelewa ,iwe ni huzushi wa vyombo vya Habri au Tetesi lakini Kwangu mie Nilitegemea Hili Jambo Kutokea has kwa mtu kama Magufuli ambaye ni Mwanachama na wa sheria ,na mtu nayetekeleza Majukumu yake kwa misingi ya sheri ana katiba.

Kwa Kauli za Waziri Mkuu ,ni kumdhalilisha Magufuri tena kwa wapiga Kura wake .Na ata kama Magufuri atashindwa kuitendea Haki nafsi yake lakini kwa Watanzania atonekana ni mtu asiye na msimamo na mahamuzi yake.

Rai yangu kwa Magufuri ,naomba Aueleze Umma nini Maoni yake kuhusu tetesi hizi.....

sure.....,
 
Back
Top Bottom