Serikali yakanusha 'kujiuzulu' kwa Magufuli

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
SERIKALI imekanusha uvumi ulioenezwa na baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli amejiuzulu kuwa si za kweli .

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu tamko la serikali kufuatia uvumi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango alisema habari hizo si za kweli na Waziri Magufuli anaendelea na jukumu alilopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Kauli hiyo ya serikali ilitolewa na Katibu Mkuu huyo, kufuatia baadhi ya magazeti ya leo(jana) ambayo ni Tanzania Daima kuandika kwamba "Magufuli ajiuzulu " na Nipashe limeandika "Magufuli azushiwa kujiuzulu"

"Tunataka kuchukua nafasi hii kuwaarifu na kuwahakikishia kwamba taarifa hizi si za kweli. Mheshimiwa Waziri anaendelea na kazi zake vizuri, amekuwepo ofisini jana na leo, na anaendelea na programu zake kama kawaida ." alisema Katibu Mkuu Mrango.

Aidha Katibu Mkuu huyo, aliongeza kwamba Waziri Magufuli hajajiuzulu , hajawahi kuwa na wazo la kujiuzulu na hana sababu ya kujiuzulu.

Sory kwa kichwa ni 'Serikali yakanusha kujiuzulu kwa Magufuli'
 
nilijua haitawezekana KURUHUSU MAGUFURI AJIUZURI NI KUGAWA CHAMA!
 
hivi junior wa magufuli anaweza kuongea kuhusu tuhuma hiyo na siyo katibu mkuu kiongozi au waziri mkuu ..... hii ni sinema tena pono
 
Kuna walakini katika hili kwanini katibu mkuu akanushe na sio magufuri mwenyewe hapa nina mashaka wamemumba msamaha nakumsihi asijiuzuru ili kulinda heshima ya chama na kuokoa mpasuko lakini hii nifundisho kwa pinda anajidai mwema kumbe mkurupukaji mkubwa wangemuacha ajiuzuru uone kama pinda wao angewaokoa
 
Heshima kwako Mathias Byabato.

Ingawa jina lako la mwisho linatumiwa na watu wa Kagera lakini nina wasiwasi wewe utakuwa mpare.Unashindwa kuandika kujiuzulu je kuongea itakuwaje ?.
 
magufuli mwenyewe njaa tu, hana lolote.ataanzia wapi kujiuzulu?
;

Unamulaumu Pombe kwa lipi?, kwani yeye ndiye aliyetangaza kujihuzuru. Ni muhimu serikali itueleze ukweli habari hizi zilitoka wapi kwani zinahatarisha usalama wa raia
 
Heshima kwako Mathias Byabato.

Ingawa jina lako la mwisho linatumiwa na watu wa Kagera lakini nina wasiwasi wewe utakuwa mpare.Unashindwa kuandika kujiuzulu je kuongea itakuwaje ?.

Heshima kwako.
Ukitazama vizuri POST yangu,niliomba radhi chini yake kuhusu makosa hayo.Unajua natumia simu na ukweli ni kuwa Hapa JF hakuna option ya ku-edit title,bali post, kama ipo nijuze kwani me nimejaribu nikashindwa.mimi halisi from KG.
 
;

Unamulaumu Pombe kwa lipi?, kwani yeye ndiye aliyetangaza kujihuzuru. Ni muhimu serikali itueleze ukweli habari hizi zilitoka wapi kwani zinahatarisha usalama wa raia
Mhhh jamani tujitahidi kuandika kiswahili fasaha, hatusemi "Unamulaumu" bali unamlaumu. Pia hatusemi "Kujihuzuru" bali Kujiudhuru.
 
SERIKALI imekanusha uvumi potofu ulioenezwa na baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli amejiuzulu kuwa si za kweli .

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu tamko la serikali kufuatia uvumi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango alisema habari hizo si za kweli na Waziri Magufuli anaendelea na jukumu alilopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete .

Kauli hiyo ya serikali ilitolewa na Katibu Mkuu huyo, kufuatia baadhi ya magazeti ya leo(jana) ambayo ni Tanzania Daima kuandika kwamba "Magufuli ajiuzulu " na Nipashe limeandika " Magufuli azushiwa kujiuzulu"

"Tunataka kuchukua nafasi hii kuwaarifu na kuwahakikishia kwamba taarifa hizi si za kweli .Mheshimiwa Waziri anaendelea na kazi zake vizuri, amekuwepo ofisini jana na leo, na anaendelea na programu zake kama kawaida ." alisema Katibu Mkuu Mrango.

Aidha Katibu Mkuu huyo, aliongeza kwamba Waziri Magufuli hajajiuzulu , hajawahi kuwa na wazo la kujiuzulu na hana sababu ya kujiuzulu.

Sory kwa kichwa ni 'Serikali yakanusha kujiuzulu kwa Magufuli'

Kuna haja gani ya Kumsemea mtu mwenye mdomo au mkono wa kuandika? Kwa nini Mh Magufuli asikanushe mwenyewe hizi tetesi ili kusafisha hali ya hewa? Kwa muda sasa Serikali imekuwa ikijibu hoja za maandamano ya CDM kupitia mawaziri kama Mh. Membe na Wasira; ni vizuri Mh Magufuli naye akapewa coverage ili ajibu hoja za CDM pamoja na kukanusha huu uvumi wa yeyey kujiuzulu.
 
I support you my bro,
kulikuwa hakuna sababu ya mtu mwingine yeyote kujibu kuhusu uvumi huu,Magufuli mwenyewe alipaswa aongee..sawa aliyeongea ni part ya serikali lakini kwa nini mwenyewe mhusika asiongee?vitu vingine vidogo lakini vinazua maswali mengi ambayo kimantiki watu wanashindwa kupata majibu.
 
Back
Top Bottom