tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,847
- 18,254
Sitaki salamu nimevurugwa, naingia kwenye mada moja kwa moja. Nchi hii ina maamuzi ya ovyo na ya kipumbavu sana. Kila kitu kinafanyika ovyo ovyo! Ni juzi tu serikali imeuza nchi kwa warabu wa DP World. Na ni jana tu Rais Samia ameenda India kuwaomba wahindi waje kununua kipande cha nchi kilichobaki baada kuwauzia warabu.
Bado vumbi la uuzaji wa nchi halijatua, serikali ya CCM imegeukia kuua elimu ya watoto wa walalahoi. Wanataka kuua elimu kwa makusudi kwa sababu watoto wao wanasoma Ulaya na Marekani. Vizazi vyao havitahusika na uharibifu huu. Lengo kubwa ni kutengeneza kizazi cha mbumbumbu wanaotawalika kirahisi ili watoto wao wakirudi kutoka masomoni ughaibuni waendelee kuwatawala watoto wa makabwela bila kutumia nguvu kubwa. Inauma sana.
Hivi ni lini serikali ya CCM itajifunza kutokana na makosa? Kipindi cha nyuma serikali ilifanya mabadiliko katika mitaala bila kuwafundisha walimu. Kuna somo ambalo hadi sasa linafundishwa shuleni linaitwa Stadi za Kazi lenye mada za kitaalamu kama vile ufundi seremala, uashi, utengenezaji wa redio, ufugaji, ushonaji, nk lakini hakuna mwalimu hata mmoja aliyepata mafunzo ya useremala, uashi, ufundi, ufugaji au ushonaji na kuandaliwa mahsusi kwa ajili ya kufundisha masomo kama hayo.
Tazama sasa serikali hii hii ya CCM inataka kubadili mitaala bila kuwapa mafunzo walimu. Nimetembelea tovuti ya taassi ya elimu ili kuona jinsi mitaala itakavyobadilika nimeshikwa na butwaa! Mitaala imebadilika kwa 99% kama unavyoona lakini serikali haijafanya jitihada zozote za kusomesha walimu licha ya kusisitiza kuwa miezi michache ijayo mitaala hii mipya itaanza kutumika hapa nchini. Hivi hawa viumbe ni nani aliyewaroga? Hebu ingia wewe mwenyewe kwenye tovuli ya taasisi ya elimu ujisomee usije ukadhani labda nawaonea kwa sababu ya chuki zangu binafsi. Kwa kweli serikali hii ina mipango ya ovyo sijapata kuona.
Niilitegemea serikali kwanza iwekeze kwenye mafunzo ya walimu kwa miaka takribani nitano hadi walimu waive ndipo ianze utekelezaji mitaala mipya. Cha ajabu serikali imetoa miaka 3 ya kuelimisha wananchi kuhusu katiba mpya licha ya kwamba maoni yalishakusanywa na Tume ya Warioba na kuandika rasimu lakini inashindwa kutoa miaka 5 ya kuwaandaa walimu watakaofundisha mitaala mipya kwa watoto wa wakulima! Kumbe huwa wanaangalia yale mambo tu ambayo yana manufaa kwao kisiasa. Hawana uchungu na maendeleo ya wananchi wa kawaida. Hawa jamaa ni wabinfasi kuliko fisi wa mwituni. Serikali ya kihuni siku zote hufanya mambo kihuni ilmradi matumbo yao yanashiba na kusaza. Nchi ya ajabu sana hii.