DOKEZO Waziri wa Elimu: Prof. Mkenda, kituo cha Walimu (TRC) Mawenzi Moshi Manispaa wanakusanya michango kutoka kila shule bila kibali chako

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,828
21,457
TANGAZO KWA WAKUU WOTE WA SHULE MOSHI MANISPAA:

Wakuu wa Shule za msingi Moshi Manispaa, Mkoa wa Kilimanjaro ,tafadhali wasilisheni michango kwa ajili ya chakula cha walimu watakaohudhuria semina kesho, tarehe 25.01.2024.

Kila shule au kituo kinatakiwa kuchangia bila kukosa ni TSh. 100, 000/=. Pia wapeni taarifa walimu watakaohudhuria ili kesho tarehe 25.01.2024 kabla ya saa 1:30 asubuhi wafike TRC (Teachers Resources Center).

Wako
Ester Michael Rwambau(+255 682 848 443‬).

Kny: Mkurugenzi wa Moshi
Manispaa.

Maswali ya msingi ya kujiuliza:

1. Wakuu wa shule wanapata wapi hizo fedha au kupitia vyanzo Gani?

2. Kwenye kituo cha walimu Kuna mhasibu wa kupokea hizo fedha?

3. Ni nani anaratibu mapato na matumizi ya hizo fedha?

4. Kwanini malipo hayo hayalipwa kupitia Control number?

5. Kwanini fedha hizo hazilipiwi kupitia mtunza hazina wa Moshi Manispaa?

6. Ester Michael Rwambau amepewa mamlaka Kwa barua ipi ya kutoka maelekezo ya Kila shule kulipia fedha kitu ambacho hakipo kwenye mwongozi wa elimu?

7. Kituo hiki kinatumika kama uchochoro wa kukusanya fedha za wizi au kugawana na Afisa elimu.

8. Kituo hiki hata fedha za kuchapa mitihani zinapelekwa Kila WAKATI kwenye TRC bila mamlaka za serikali kujulishwa, na hakuna wa kuuliza mapato na matumizi ya fedha zinazokusanya kutoka Kila shule.

9. Idadi ya walimu waliopo ndani ya TRChiyo ni kubwa na wanapelekwa hapo bila barua au kujulikana na REO ili kujipumzishia hapo na hawana kazi muhimu kupitia miongozo iliyoanzisha TRC, tunaomba waondolewe wakaongeze nguvu kufundisha madasani Kuna upungufu mkubwa wa walimu.

10. Wengine wamewekwa kituoni hapo Kwa sababu ya kutoa Rushwa ili wakapumzike hapo bila kufundisha.

11. Afisaelimu msingi na secondary wote ni wapokeaji wa malalamiko ila sio watatuzi wa malalamiko ya walimu. Wanasema wanajulikana na Wana mtu mkubwa huko juu.

12. Idara ya elimu msingi Ina shule za serikali 36 ila Ina wataaluma (mabosi 3) watatu kutoka Halmashauri, unakuta utendaji wa wataaluma watatu, Kwa shule 36 ni matumizi mabaya ya raslimali watu, na unakuta ni WA awake wa watu au watoto wa mtu Fulani.

13. Kituohicho cha walimu kina watumishi zaidi ya idadi inayohitajika na hawana sifa za kukaa kituo cha walimu kulingana na mwongozi ulioanzisha vituo vya ualimu.

14. Kazi ya kituo cha walimu ni kuwasaidia walimu kutoa mafunzo, senina na washa za kielimu, kituo hicho hakitimizi wajibu HUO kwanini hakuna watumishi wenye sifa.

Msema kweli mpenzi wa Mungu!
 
Iko Hivi:
Mkenda/ Wizara ya Elimu haihusiki hapo, hilo ni suala la OR TAMISEMI
 
The contribution of Teachers’ Resource Centres (TRCs) in enhancing teachers’ professional
developments.
Techers trained at the TRCs were not competent in the subject matter as expected.

There is a need for the TRCs to evaluate and review teachers’
programme for effective teacher training.
Waliopo kituoni hapo hili hawalijui, wapi kusubiria mishahara TU.
 
The contribution of Teachers’ Resource Centres (TRCs) in enhancing teachers’ professional
developments.
Techers trained at the TRCs were not competent in the subject matter as expected.

There is a need for the TRCs to evaluate and review teachers’
programme for effective teacher training.
Waliopo kituoni hapo hili hawalijui, wapi kusubiria mishahara TU.
Hivi vituo viko nchi nzima au?
Lengo hasa ni nini?
Sifa za kufanya kazi kwenye vituo hivi ni zipi?

Kiongozi wa kituo hiki anateuliwa na mamlaka ipi, je anakuwa na sifa zipi za kimuundo na kitaluuma?
 
Hivi vituo viko nchi nzima au?
Lengo hasa ni nini?
Sifa za kufanya kazi kwenye vituo hivi ni zipi?

Kiongozi wa kituo hiki anateuliwa na mamlaka ipi, je anakuwa na sifa gapi za kimuundo na kitaluuma?
CC: Maafisaelimu msingi nchi nzima.
 
Yap vipo nchi nzima
Pamoja na uwepo wake nchi nzima vimejazwa walimu wasio na sifa, vimepunguza idadi ya walimu madarasani, ni eneo la upokeaji wa rushwa Kwa vile vituo vilivyopo mjini.
2. Haijulikani vituo hivyo vinafanya kazi Gani na walimu hawajui majukumu ya vituo hivyo
 
Hivi vituo viko nchi nzima au?
Lengo hasa ni nini?
Sifa za kufanya kazi kwenye vituo hivi ni zipi?

Kiongozi wa kituo hiki anateuliwa na mamlaka ipi, je anakuwa na sifa zipi za kimuundo na kitaluuma?
Kiongozi wa kituo ni Afisa Elimu kata wa kata hiyo. Anateuliwa na Afisa Elimu msingi wa halmashauri Kwa muongozo wa Sasa,ila zamani Afisa Elimu msingi alikuwa anateua mwalimu yoyote wenye diploma ama shahada kuwa msimamizi wa kituo.
Lengo la kituo ni walimu kujiendeleza kwa mafunzo mbalimbali(mafunzo kazini)
 
Kiongozi wa kituo ni Afisa Elimu kata wa kata hiyo. Anateuliwa na Afisa Elimu msingi wa halmashauri Kwa muongozo wa Sasa,ila zamani Afisa Elimu msingi alikuwa anateua mwalimu yoyote wenye diploma ama shahada kuwa msimamizi wa kituo.
Lengo la kituo ni walimu kujiendeleza kwa mafunzo mbalimbali(mafunzo kazini)
Sasa kituo kimejaa walimu wasio na sifa,wamepangwa hapo na nani?

Je malengo ya kituo yamefikiwa au ni kupoteza raslimali watu za taifa?
 

Serikali isipochukua hatua juu ya kituo cha ualimu ( Teacher resources centers) na idadi ya mabosi wa kuwepo ofisi za Halmashauri, kuna siku yatatokea ya walimu kuandamana. Na kufanya migomo ya kufundisha.​

 
Licha ya Takwimu za Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha 4 zilizotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania kuonesha Watahiniwa 484,823 (87.65%) wamefaulu Mtihani huo, Watahiniwa 56,149 (10.64%) wamefeli kwa kupata Daraja 0.

Pia, Jumla ya Watahiniwa 274,001 (51.94%) wamepata Daraja la 4 ikiwa ni ongezeko la 1.1% kutoka Watahiniwa 264,627 (50.84%) waliofanya Mtihani mwaka 2022.

Aidha, Ufaulu wa Somo la Hisabati umeendelea kuwa chini ambapo takriban 74.58% ya Watahiniwa waliofanya Mtihani wamefeli Somo hilo na waliofaulu ni 12.75% pekee katia 527,608.
 
Walimu wenyewe mashuleni hakuna, afu wanaweka wengine vituoni wakae buree,
Halali matokeo mabaya yaendelee kutamalaki. Kazi ipoo
 
Kama Walimu wanatekeleza vema Ilani ya CCM kwanini 61% ya Watahiniwa Kidato cha 4 Wamefeli( IV na 0)?
 
Kwa wanaojua tuelewesheni. Mkenda ni Profesa wa taaluma gani? Niliwahi kusoma kuwa ni Profesa wa ARU lakini sijaelewa taaluma yake pale ARU ni ipi; Land Surveying, Quantity Surveying, Valuation, Real Estate Management, Architecture, ......... nk. ARU ina taaluma nyingi sana adimu ila ya Mkenda ndiyo sijaelewa sawasawa ni ipi.
 
Professor Mkenda, anaonyesha ana dharau sana.

Na anamlinda sana Afisaelimu msingi na secondary Moshi Manispaa, Kuna dalili Xmas wanampelekea ndafu huko Rombo, ili asiwatoe kwenye nafasi hizo.
 
Back
Top Bottom