Mbunge Martha Mariki, Najma Murtaza na Rose Tweve Waibana Serikali Bungeni Kutoa Elimu kwa Watanzania Wasiojua Kusoma na Kuandika

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MBUNGE MARTHA, NAJMA NA TWEVE WAIBANA SERIKALI BUNGENI KUTOA ELIMU KWA WATANZANIA WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA

"Tuna zaidi ya Watanzania asilimia 16 hawajui kusoma na kuandika. Ni upi mkakati wa Serikali wa kuhakikisha tunatenga bajeti kwenda kuhudumia watanzania ambao wanapata elimu kwenye mfumo usio rasmi kama vile taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ambao kwa sasa hawapati ruzuku" - Mhe. Rose Cyprian Tweve, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa

"Tutakwenda kufanya tathimini ya kina namna gani tunaweza kutenga bajeti kwenye taasisi ya elimu ya watu wazima ili kuweza kuwafikia kundi la watu wasiojua kusoma na kuandika" - Mhe. Omary Juma Kipanga, Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia

"Je, Serikali haioni umuhimu sasa wa kuwa na takwimu halisi za viwango vya Elimu na Makada yake kuanzia kiwango cha juu cha elimu hadi kufikia chini kwa mustakabali muhimu wa Maendeleo ya Taifa letu? - Mhe. Najma Murtaza Giga, Mbunge wa Viti Maalum, Wazazi Tanzania.

"Tuna mfumo wa Takwimu wa Elimu (BEST - Basic Education Statistics of Tanzania) kwa muda mrefu ulikuwa unaangalia shule zinazomilikiwa na TAMISEMI na Shule zinazotumia mtaala wa Taifa" - Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia

"Sasa hivi tuna dawati la kuhakikisha Takwimu za kuanzia elimu ya awali mpaka Vyuo Vikuu zinakusanywa nakala itakayokuwa inatolewa kila mwaka na kujumuisha watoto wanaotumia mitaala ya kigeni (Cambridge)" - Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia

"Upi mkakati wa haraka zaidi kuhakikisha mnawanusuru hususani watoto wadogo ambao wanapatikana jamii za wafugaji na wavuvi ambao hawajui kabisa kusoma na kuandika ili waweze kujua kusoma na kuandika? - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Maboresho ya mtaala wa Elimu yaliyofanyika mwaka 2023 Bungeni unakwenda kuchukua ngazi zote za watoto wote kuhakikisha wanakuwa shule. Sera na mitaala hii ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha mtoto aliyefikisha umri wa kwenda shule aweze kwenda shule" - Mhe. Omary Juma Kipanga, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia

"Nitoe maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya iwe ni eneo la Wachungaji au wavuvi kuhakikisha vijana wenye umri wa kwenda shule waandikishwe na kukaa shuleni" - Mhe. Omary Juma Kipanga, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
 
Back
Top Bottom