Serikali iboreshe mazingira ya shule zake iache kubadili gia hewani, fikra za Ushindani ni muhimu

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Dec 13, 2019
1,099
1,286
Wakuu mimi ni miongoni mwa watu wengi ambao tunatamani kuona mabadiliko makubwa kwenye elimu yetu, ninayo mengi ya kuyaandika juu ya mabadiliko ya elimu yetu.
Sera ya Elimu yetu
Mfumo wa Elimu yetu
Mitaala
Ubora

Ila Kwa Leo nimeshangazwa na Serikali kupitia Necta chini wizara ya Elimu kutoa sababu juu ya kutofautiana mazingira ya utoaji elimu.
 
Tusiunge mkono serikali kuficha data pale inaposhindwa kutekelez wajibu wake,

Kama mazingira yanatofautiana basi ni jukukumu lake kuboresha mazingira Ili Kila mwanafunzi apate elimu kwenye mazingira yaliyo Bora. Na sio kuficha uhalisia kisa tu shule zake zimeanguka

Kuna haja Gani kutoa mtihani unaofanana Kwa shule zote kama mazingira hayasapoti

Kama sio kuwaonea wanafunzi wengine
Kulikuwa na haja Gani kuwapotezea wanafunzi muda wao wa miaka minne kama wanajua mazingira ya shule zao hayawapi nafasi ya kufanya vizuri

Kuna haja gani serikali kuzikasirikia shule zilizofanya vizuri kuzipongeza Ili kuongeza motisha Kwa utoaji Bora wa elimu

Tusiunge mkono mawazo ya kijinga na kijamaa ya kuondoa fikra za ushindani Kwa wanafunzi ili tufanane wote chini ya viwango

Mabadiliko tunayoyataka kwenye Elimu ni makubwa sio hayo ya kuficha takwimu za waliofanya vizuri haitusaidii sana kama nchi yenye kuhitaji kuongeza Kasi ya maendeleo
 
Serikali inaharibu watoto wa walalahoi kwa kuwaweka watoto kwenye makambi ya bangi na ngono (usiite sekondari za kata) kwa miaka 4.

Ndiyo maana hakuna hata kiongozi mmoja anayesomesha mtoto wake kwenye makambi hayo
 
Back
Top Bottom