Riba za Mabenki kwa Watumishi wa Umma na Sekta Rasmi ni Kubwa Sana, Serikali Iangalie Namna ya Kupunguza Riba kwa Watumishi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE ZAYTUN SWAI: Riba za Mabenki kwa Watumishi wa Umma na Sekta Rasmi ni Kubwa Sana, Serikali Iangalie Namna ya Kupunguza Riba kwa Watumishi

"Naomba kutoa pole kwa watanzania wakiwemo wananchi wenzangu wa Mkoa wa Arusha hususani Jimbo la Monduli kwa kuondokewa na mpendwa wetu Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi. Kazi kubwa sisi tunaobaki ni kumuenzi kwa yale mazuri aliyofanya na kuendeleza mbele kwa maslahi mapana ya Taifa letu" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Serikali imekuwa ikifanya jitihada mara kwa mara kuendeleza mikopo kwa sekta binafsi. Sekta hii imekuwa zaidi ya wastani, imekuwa kwa asilimia 19.5 ambayo ni juu ya wastani wa asilimia 16.4" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Changamoto kubwa iliyopo katika sekta binafsi ni riba kubwa ya Benki za Biashara. Riba zimeweza kushuka kutoka asilimia 16.10 hadi kufikia asilimia 15.54. Asilimia 0.56 bado iliyoshuka bado ni ndogo sana ukilinganisha na Serikali inavyofanywa kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Tumeona mazingira mazuri ya kikodi yameboreshwa (Wizara ya Fedha imezindua Ofisi ya Msuluhishi wa Kodi), Kupitia Benki Kuu ya Tanzania, usimamizi na udhibiti wa Mabenki umeendelea kirafiki zaidi, pia, mikopo chechefu imeendelea kupungua kwa asilimia kubwa katika kipindi kilichopita" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Wizara ya Fedha iweze kuangalia jinsi ya kupunguza riba za mabenki ya biashara ili wananchi wengi waweze kufaidika na mikopo ya mabenki na kujikwamua kiuchumi. Viwango vya riba kwa watumishi wa umma ni kubwa mno" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Gharama za kukusanya mikopo kwa watumishi wa umma na watumishi walioajiriwa katika sekta zilizo rasmi, mabenki yanaingia gharama ndogo sana ya ukusanyaji. Mwajiri anakusanya madeni kutoka kwenye mishahara ya waajiriwa " - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Naomba Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania iweze kuangalia jinsi ya kushusha riba za mikopo hususani kwa watumishi wa umma na watumishi wote walioajiriwa katika ajira zilizo rasmi" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Sekta ndogo ya fedha inajumuisha Mabenki ya Microfinance, watoa mikopo binafsi, SACCOS na vikundi mbalimbali vya kijamii vinavyoweka akiba na kukopa. Malengo makubwa ni kuwezesha upatikanaji wa Mikopo kwa watanzania walio wengi wenye kipato cha chini kama vijana, Wanawake, wajasiriamali na Makundi Maalum" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Asilimia 21 ya watanzania wanatumia sekta ndogo ya fedha. Bado kuna watanzania wengi sana hawajaweza kujiunga na sekta ndogo ya fedha kwasababu ya ukosefu wa Elimu ya fedha. Watanzania wengi wanadanganywa na watoa mikopo binafsi hivyo kuwapelekea kwenye mikopo ya kausha damu" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Mwananchi anaenda kukopa anadanganywa, riba ya mkopo ni asilimia 20 kwa mwezi, kwa mwaka anajikuta amelipa riba zaidi ya asilimia 200. Serikali iweze kuongeza kasi ya utoaji wa Elimu ya fedha kwa wananchi" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Kuna waratibu na wahamasishaji zaidi ya 700 wameajiriwa kwenye ngazi za Mikoa na Halmashauri ili watoe Elimu kwenye ngazi za chini. Sijaona kasi ya utoaji Elimu ikiendelea. Mara nyingi Elimu ya fedha inatolewa kwenye makongamano au maadhimisho ya wiki ya fedha kwenye center za Mjini" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha

"Tunahitaji kuona Elimu ya fedha ikienda ngazi za chini, Halmashauri na Kata, wananchi wa Ngorongoro, Longido waweze kufahamu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye sekta ndogo ya fedha na kujua sehemu za kupata mikopo yenye riba zenye uhalisia, kipindi gani wajiwekee akiba wao wenyewe na Elimu iwawezeshe kulipa madeni yao" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-02-14 at 19.10.00(1).mp4
    23 MB
  • WhatsApp Image 2024-02-14 at 19.10.00(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-14 at 19.10.00(1).jpeg
    123.2 KB · Views: 6
Duh huyu mtu ana hoja,asikilizwe,lakinI wenye hisa kubwa kwenye hayo mabenki wako huko huko bungeni,sijui kawa watafurahishwa!
 
Having your Cake and try to eat it....

Kama mmeamua mambo yaende kibiashara na kutumia market forces hayo mambo ya kushusha riba wakati Taasisi ina risk zake katika kukopesha ni kudanganyana....

Kama vipi serikali itoe ujira ambao unatosha kulingana na maisha na sio kuleta hizi hadithi za miaka nenda rudi.....
 
Back
Top Bottom