tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,991
- 18,511
- Thread starter
- #21
Sasa ukienda kutibiwa ukaandikiwa cetrizen utaitupa ukanunue hiyo inayokutibu au utafanyaje? Mimi sijawahi kwenda hospitali yoyote naumwa mafua nikaandikiwa dawa tofauti na cetrizen. Ukiwauliza watoa huduma kwanini wanataka kutuua kwa usugu wa vimelea wanasema wameelekezwa na NHIF watoe dawa hiyo tu.Mimi binafsi nikiugua mafua hakuna dawa inayoweza niponesha kama promethazine, sasa nitalazimishwaje kutumia cetrizen ambayo by nature hainisaidii kitu?
Nikishaona hivyo inabidi niingie gharama nikanunue dawa ya coldril au dr cold syrup nijitibu. Kwa maana hii sasa bima inakuwa haina maana yoyote zaidi ya michosho isiyokuwa na mwisho na kutiana hasara zisokuwa na msingi wowote. Inasikitisha mno.