Serikali: Huu ndio ushauri wa mwisho kwa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF)

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,847
18,251
Katika siku za karibuni Bima ya Afya ya Taifa imekuwa gumzo kila kona, hasa inapodaiwa kwamba mfuko huu wa bima unaotoa matibabu kwa watumishi wa umma na familia zao, unakaribia kukata roho. Naomba kutangaza masilahi (declare interest) kwamba mimi ni mnufaika wa mfuko huu kupitia wazazi wangu ambao ni watumishi wa umma.

Mbali na NHIF kuna mifuko mingine mingi inayotoa huduma nzuri zaidi hapa nchini ukilinganisha na mfuko huu ambao kila kukicha umekuwa ukiwafanyia vitimbi wananchama wake na kuwakosesha huduma za matibabu kwa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu. Nasema haya kwa ushahidi mubashara. Uongozi wa NHIF umekuwa ukiwabania wanachama wake dawa nzuri na zinazotibu barabara kwa kuhofia wananchama wao kuwa na afya mujarabu. Lengo la kufanya hila zote hizi wanazijua viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia mfuko. Vitimbi vya karibuni kabisa kufanywa na NHIF ni kufuta fao la Toto Afya Card na kuwapangia wanachama kiasi cha kuumwa – kwamba kila mwanachama aumwe mara 4 tu kwa mwezi!

Kuna bima lukuki hapa nchini zinazotoa huduma nzuri bila unyanyapaa wala vitimbi kwa wananchama. Nimewahi kuwa mwanachama wa bima za afya Medex na AAR. Mifuko hii haina ujinga kama huu tunaoshuhudia NHIF. Wanajali zaidi uhai wa mwanachama tofauti na NHIF wanaojali matumbo yao na kuwaacha wanachama wajifie kifo cha mende. Ukiwa ndani ya AAR au Medex ni raha tupu. Hata ukiumwa ugonjwa mkubwa ulioshindikana kutibika hapa nchini, unasafirishwa nje ya nchi kwenda kutibiwa. Kupitia mifuko hii, wagonjwa wengi tu wametibiwa Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Afrika Kusini India na mataifa mengine ya nje yenye huduma nzuri za afya. Lakini kwa NHIF, ugonjwa wako ukishindikana kutibiwa hapa nchini, unaachwa ujifie kama mbwa. Inauma sana.

Baada ya kutoa dokezo hiili, naomba sasa nitoe ushauri wangu wa mwisho jinsi ya kuboresha huduma za NHIF. Kwanza ni kuondoa ukiritimba na figisu kwa wanachama. Nashauri wanachama wapewe uhuru wa kuchagua mfuko wa matibabu tofauti na sasa ambapo watumishi wote wa umma hulazimishwa kukatwa pesa na kutibiwa na NHIF watake wasitake. Wanachama wengi, ambao ni watumishi wa umma, wamechoshwa na vituko vya NHIF. Wanatamani wafunguliwe minyonyororo ya utumwa waliyofungwa kwa muda mrefu ndani ya NHIF wakatafute huduma nzuri kwenye mifuko mingine inayotoa bima za matibabu kama vile AAR, Momentum, Strategies, NMB, NSSF na mingine mingi tu iliyotapakaa hapa nchini.

Kwanini watu wanyimwe uhuru wa kujiunga na mifuko mingine ilhai kila siku NHIF inalalamika kuwa na hali mbaya ya kiuchumi? Ukiona hivyo ujue kuna manufaa ambayo serikali na watumishi wa NHIF wanayapata ambayo wakiruhusu watu waondoke, wanaweza kuyakosa. Kwa maana hiyo kumbe NHIF haipo kwa ajili ya maslahi ya wanachama bali ni kwa ajili ya maslahi ya serikali na wachumiatumbo wachache wasiopenda kuona watanzania wanakuwa na siha njema. Huu ni zaidi ya uhaini na uhujumu uchumi. Naomba TAKUKURU wafanye uchunguzi wa kina.

Ili NHIF iondokane na malalamiko ya gharama kubwa za matibabu kwa wanacham wake na kuhofia kufilisika, basi iwaachie wanachama waondoke mmoja mmoja waende wakatafute matibabu kupitia bima nyingine za afya. Wakibaki wanachama wachache inaweza kuwahudumia vizuri zaidi. Na hata hao wachache wakiamua kuhama, waachiwe waondoke. Wanachama wote wakishaondoka NHIF ifunge ofisi zake zote nchini na serikali iwapangie kazi nyingine waliokuwa waajiriwa wa NHIF. Kufikia hapo tatizo litakuwa limepata ufumbuzi wa kudumu. Huwezi kung’ang’ania jambo linakuuumiza kichwa wakati kuna ufumbuzi wa kudumu usiohitaji gharama yoyote.

Ikiwa serikali itafuata ushauri huu, itajiondoa jumla kwenye lawama za watanzania wanaokufa kila siku kwa sababu ya ubovu wa huduama za NHIF inayolalamika kutokuwa na fedha za kutosha kugharamia matibabu ya wanachama wake hadi kufikia hatua ya kufuta fao la Toto Afya Card na kuanzisha masharti ya kipuuzi kwa wananchma ambayo hayatekelezeki.

Nawasilisha.
 
Hiyo mifuko mingine gharama zao zikoje?

Au serikali ili kuwasaidia watoto ingeweka sheria iwe lazima kwa mtoto kuwa na Bima nadhani ingesaidia sana
Hii mifuko mingine ni kama nilivyoeleza kwenye uzi. Haijali gharama anazotumia mteja na hawana limitation kwa dawa. Dawa yoyote unapata tofauti na NHIF wanaobagua dawa nzuri na kuruhusu dawa hafifu tu ndio zitolewe kwa wanachama wao.
 
NHIF wanataka watoa huduma za afya wafate mlolongo wa matibabu, tuchukulie mfano wa management ya Malaria, STG inasema kwa uncompleted malaria mpe Alu , but unaweza kuta mtu ana malaria lakini hana dalili za severe malaria analazimisha umchome sindano za artesunate etc, kitu ambacho ni hatari kwa afya za wateja pale ambapo dawa ikiuzoe mwili na kutengeneza usugu, kwa hyo kuna mambo NHIF wako sawa , huwez walaumu
 
Ingekuwa wafanyakazi wa Serikali sio lazima kujiunga na mfuko wa bima NHIF, nadhani mjadala ungekuwa na mtizamo wa aina ingine
 
NHIF wanataka watoa huduma za afya wafate mlolongo wa matibabu, tuchukulie mfano wa management ya Malaria, STG inasema kwa uncompleted malaria mpe Alu , but unaweza kuta mtu ana malaria lakini hana dalili za severe malaria analazimisha umchome sindano za artesunate etc, kitu ambacho ni hatari kwa afya za wateja pale ambapo dawa ikiuzoe mwili na kutengeneza usugu, kwa hyo kuna mambo NHIF wako sawa , huwez walaumu
Mkuu unachoongea is just a subset of the main set of problems created and perpetuated by NHIF at the deadly expense of the patients.
 
Mkuu unampigia mbuzi gitaa

OIG (10).jpeg
 
Na hili ndilo linalopelekea watumishi wa umma kuendelea kupata taabu kwa sababu hawana option ya kutoka kwenye minyororo ya utumwa wa NHIF.
Sidhan kma watumishi wa umma wanapata tabu kiasi hicho kwa sababu ni lazima kujiunga na NHIF, laah Hashaaah!

Kuna maboresho mengi yamefanyika ili kuhakikisha mwanachama anapata huduma stahiki katika kituo husika regardless level ya kituo hicho.

Utolewaji wa dawa kwa wateja unatokana na daraja alililonalo muhusika , mfano kuna dawa zinatolewa na MD na CO haruhusiwi kuzitoa, ila kama kituo husika ni Dispensary kwa mfano, na katika dispensary hiyo yupo MD , zen anaweza prescribe dawa hiyo na NHIF wanalipa vizuri tu. Changamoto ni watoa huduma kutaka kuforce mambo na hapo huwa wanaleta taharuki na kupelekea kituo husika kupata hasara.

Pili, katika vituo vingi vya kutolea huduma za afya , Kuna udanganyifu mwingi kitu kimepelekea kuunzishwa kwa uhakiki kwa alama za vidole.

Kitu pekee cha kuconcern ni matumizi ya fedha hizo za wanachama, ila sio huduma, dawa zote zinatoka depending na qualification ya watoa huduma.
 
Mkuu kuna huu ujinga unaofanywa na NHIF kulazimisha matumizi ya dawa aina moja kwa muda mrefu, jambo linalochochea usugu wa vimlea na kupelekea vifo vya wanachama wengi sana. NHIF kataa ukubali ni janga la kitaifa.

Chukulia kwa mfano dawa ya mafua ya citrizen. Kila hospitali, zahanati au kituo cha afya utakachoenda unaumwa mafua, LAZIMA uandikiwe dawa hii. Matokeo yake vimelea vimeizoea kiasi kuwa wagonjwa hawatibiki tena. Hii shida kubwa sana.
 
Hebu niambie jinsi mwanachama anavyoweza kujitoa NHIF. Hakuna namna. Watumishi wote wanalazimishwa waingie NHIF ili wafe haraka serikali ifaidi pensheni zao, hasa baada ya kufanya wizi wa hela za wastaafu kupitia kikokotoo cha kishetani kilichoanzishwa na serikali sikivu ya CCM.
 
Sidhan kma watumishi wa umma wanapata tabu kiasi hicho kwa sababu ni lazima kujiunga na NHIF, laah Hashaaah!

Kuna maboresho mengi yamefanyika ili kuhakikisha mwanachama anapata huduma stahiki katika kituo husika regardless level ya kituo hicho.

Utolewaji wa dawa kwa wateja unatokana na daraja alililonalo muhusika , mfano kuna dawa zinatolewa na MD na CO haruhusiwi kuzitoa, ila kama kituo husika ni Dispensary kwa mfano, na katika dispensary hiyo yupo MD , zen anaweza prescribe dawa hiyo na NHIF wanalipa vizuri tu. Changamoto ni watoa huduma kutaka kuforce mambo na hapo huwa wanaleta taharuki na kupelekea kituo husika kupata hasara.

Pili, katika vituo vingi vya kutolea huduma za afya , Kuna udanganyifu mwingi kitu kimepelekea kuunzishwa kwa uhakiki kwa alama za vidole.

Kitu pekee cha kuconcern ni matumizi ya fedha hizo za wanachama, ila sio huduma, dawa zote zinatoka depending na qualification ya watoa huduma.
NHIF staff wanalipana mishahara minono mno na mikopo lazima mfuko uchemke
 
Mkuu kuna huu ujinga unaofanywa na NHIF kulazimisha matumizi ya dawa aina moja kwa muda mrefu, jambo linalochochea usugu wa vimlea na kupelekea vifo vya wanachama wengi sana. NHIF kataa ukubali ni janga la kitaifa.

Chukulia kwa mfano dawa ya mafua ya citrizen. Kila hospitali, zahanati au kituo cha afya utakachoenda unaumwa mafua, LAZIMA uandikiwe dawa hii. Matokeo yake vimelea vimeizoea kiasi kuwa wagonjwa hawatibiki tena. Hii shida kubwa sana.
Mkuu, hapana , NHIF hawajawahi kulazimisha kutoa dawa aina moja , isipokuwa ni utashi wa priscibers, mfano dawa katika tiba ya mafua, sio tu lazima kuprescribe cetrizen, Kuna dawa kama chlorpheniramine, promethazine loratadine etc hizi zote zinatibu flue na common cold zinazotokana na allergic reactions , sasa hapa ni chaguo la daktar wako na qualification yake kuprescribe dawa hizo.

Mimi binafsi nikiugua mafua hakuna dawa inayoweza niponesha kama promethazine, sasa nitalazimishwaje kutumia cetrizen ambayo by nature hainisaidii kitu?
 
Hebu niambie jinsi mwanachama anavyoweza kujitoa NHIF. Hakuna namna. Watumishi wote wanalazimishwa waingie NHIF ili wafe haraka serikali ifaidi pensheni zao, hasa baada ya kufanya wizi wa hela za wastaafu kupitia kikokotoo cha kishetani kilichoanzishwa na serikali ya CCM.
Mkuu, Hiyo ya kikokotoo ni PSSF, pia kama serikali isingefanya ulazima wa kumuunga mtumishi katika mfuko wa bima ya afya wengi wasingechukulia umuhimu wa kujiunga kama alivyo mwananchi wa kawaida
 
Back
Top Bottom