Dkt Elizabeth Sanga: Serikali Isifanye Afya za Wananchi Bidhaa

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Tamko la ACT Wazalendo kusitishwa kwa Bima ya NHIF kutumika katika hospitali binafsi nchini.

ACT Wazalendo tumeshtushwa na mivutano kati ya Serikali kupitia Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na chama cha watoa huduma binafsi za afya nchini (APHFTA) na baadhi ya hopsitali binafsi. Mvutano uliopelekea baadhi ya vituo binafsi kusitisha kupokea wagonjwa wanaotumia Bima ya Mfuko wa Taifa (NHIF) na wagojwa walioanza matibabu wamepewa muda wa saa 48 kuondolewa katika hospitali hizo kakuanzia juzi tarehe 1 Machi, 2024.

Mvutano huu unadhihirisha kwa mara nyingine tatizo la kimsingi la kisera namna Serikali ilivyofanya afya ya wananchi wake kuwa bidhaa na huduma ya afya imegeuzwa kuwa bidhaa ambayo upatikanaji wake unabishaniwa katika msingi wa bei na vitita. Afya sio tena haki ya msingi ya kila mwananchi. Si jambo la utu ni biashara. Jambo hili ni hatari na hasa hasa kwa sasa wagonjwa wenye bima ya NHIF wanaoendelea kupata huduma kwenye hospitali hizo. Ni wazi mgogoro huu utawaathiri zaidi wananchi.

Tunafahamu 85% ya wananchi wanalipia huduma za afya kutoka mfukoni, hii inatokana na gharama kubwa za kujiunga na NHIF pamoja na ukosefu wa huduma bora za afya hasa kwenye ngazi za zahanati na vituo vya afya. Kuongeza huduma kwa njia inayoathiri utoaji huduma kwa watoaji huduma wa binafsi sio suluhisho.

Uamuzi ambao hauondoi mzizi wa tatizo la mwananchi kushindwa kupata huduma za afya, ama kwa kushindwa kugharamia au kwa ukosefu wa huduma bora.
ACT Wazalendo tunaona kuwa mgogoro huu ni matokeo ya huduma ya afya kugeuzwa kama bidhaa iliyopelekea kutungwa kwa sheria mbovu ya bima ya afya, sheria ambayo imeweka matabaka makubwa kupitia vifurushi na haitoi uhakika kwa mwananchi kuendelea kupata huduma kila atapohitaji. Hivyo, tunataka hatua zifuatazo zichukuliwe.

i. Serikali isitishe vitita vyake ilivyopitisha kutumika na tunatoa rai kwa hospitali zote za binafsi ziendelee kuhudumia na kupokea wanachama wote wa NHIF na kuondosha mgomo huo ambao utaathiri sana wananchi (wanachama wa NHIF).

ii. Serikali ifute sheria ya bima ya afya ambayo ni dhahiri haiondoi tatizo la ugharamiaji, uhimilivu, haiokoi NHIF wala haitasaidia kutoa nafuu kwa wananchi. Badala yake ichukue pendekezo letu la kufungamanisha Bima ya afya na Hifadhi ya Jamii ambapo kila mwananchi atakuwa na bima ya afya na atachangia kulingana na uwezo wake na atapewa huduma kulingana na mahitaji yake.

iii. Tunaendelea kuisistiza Serikali kuboresha na kuongeza huduma za afya ya msingi ya zahanati na vituo vya afya, ili kuimarisha huduma za kuzuia magonjwa na kupunguza idadi ya watu kwenye hospitali za rufaa.
Mwisho, katika mgogoro huu ambao sekta binafsi inataka faida zaidi na Serikali inataka kuokoa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya anayeumia ni mwanachama wa NHIF.

Hakuna muujiza wa kuondoa ombwe hili, Serikali isihangaike na matokeo badala yake ihangaike na mzizi wa tatizo kwani hata wakikubaliana bado vifurushi/vitita hivyo bado vitapokea upinzani mkubwa kwa wananchi ambao hawatamudu gharama hizo, suluhisho pekee la kisayansi kwa sasa ni kufungamanisha huduma ya Afya na hifadhi ya jamii.

Ahsanteni sana.
Imetolewa na;
Dr. Elizabeth Sanga
Waziri Kivuli wa Afya
03 Machi 2024.
 
Back
Top Bottom