Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

muosha huoshwa... (sishabikii kilichompata) but huenda ni revenge ya mambo aliyofanya au anayoendelea kufanya...

na kama watu wameshaona yuko juu ya sheria wameamua wamwazibu mwenyewe. Pole yake
 
Leo nimegundua watanzania wengi wameingiwa na roho ya kikatili sana,tuna hatari ya kuwa na society ambayo ni fragile.

Huu ufedhuli wa Conc. H2SO4 umekua so popular.

Watu wanashangilia na kuhalalisha kwa kumjengea victim taswira hasi
Mkuu usishangae ukisikia watu wanatembea na vidumu vya tindikali kama silaha nafuu badala ya bastola
 
Nilijua tu, issue Kariakoo haiishi kirahisi.

Media zimenunuliwa, 'redio flani' ikatumika kuonyesha kuwa tatizo ni TRA wakati ukweli unajulikana.

Magazeti mengine yakamezea. Tunashangaa haya?

Njia iliyobakia ilikuwa ni wazi watu hawa ambao biashara zao zimevurugika ghafla wataanza kutafuta mbadala. Tatizo ni kujua mbadala wake ni upi.

#NawazaTu

Sema tu moja kwa moja...Radio iliyonunuliwa kupotosha hilo swala la Makontena Bandarini ya Wafanyabiashara wa K'koo ni Mawingu fm,tena kile kipindi chao cha saa kumi jioni chini ya yule bwana mwenye dental formula tengefu aliweka sana ushambenga...wakakwepesha ukweli na kutupa zigo TRA....Watu wakafunga maduka,mitaji ikayumba kisa "tajiri" mmoja!!Hii radio inabidi ijitazame sana
 
Jana jioni mwenyekiti wa taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwa na baadhi ya wabunge mashuhuri wa chama hicho, Godbless Lema na Halima Mdee, na makada wengine, walifanya ziara ya ghafla kuwafariji wagonjwa katika hospitali ya KCMC, Moshi. Ninamfahamu Mbowe. Nimelazwa hapa. Alishangazwa sana kunikuta hapa. Alinisalimia kwa furaha kwani tumepoteana miaka mingi.

Nilibahatika kuongea na mmoja wa makada waliokuja kutupa pole. Aliniambia kwamba hivi sasa vijana wamechoka kunyanyaswa, wako tayari na mapambano, liwalo na liwe.

Nikamwambia: Lakini hii ni hatari!
Akajibu: Ndio, ni hatari lakini hayo ndiyo matokeo ya sera kandamizi za CCM.

Vijana wameapa kupambana na mafisadi wote wenye ushirika na CCM. Sishangai tajiri huyu kumwagiwa tindikali. Wengine wajiandae. Hukumu yao inakuja.
 
Ukicheka sana ipo siku utalia sana

Ukilia sana ipo siku utakuja cheka sana

Ukiwa mgovi sana kuna siku utakuwa mpole sana

Ukiwa malaya sana kuna siku utakipa kilichopo kwenye huo umalaya(ukimwi)

Ukiwa mchimbaji wa madini na ukavumilia ipo siku utatoka na chochote kama sio kuishia humo humo na shimo lako kuwa kaburi lako

Ukiwa muongeaji sana ipo siku utakuwa mc wa harusi ama mlopokaji

Ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga

Maisha hayawi maisha bila kuishi

Ikiwamwagia sana wenzako ipo siku na wewe utamwagiwa, iwe maji, soda, bia, mafuta ya taa, petroli,acid etc...

Pole sana bro, kama ni kweli wakuwaishe tu india kabla hujadhurika sana, wanadamu kuna mda wanakosa damu wanabakia wana tu

Umesahau na hili, Ukiuza sana unga wa kulevya iko siku utakuja kukuumbua na majihela hela yako na kukuweka mahali pabaya hata kama sio kuzimu.
 
wanadamu wa ajabu sana, yaani wanafurahia kuona mwenzao anadhurika?
Kwa kuwa wao halijawakuta, hivyo haliwahusu. Siku likiwakuta, kelele utakazozisikia.. Inabidi tuheshimu misingi ya sheria hata kama tuna tofauti zetu, tunavyoendelea kushabikia ndivyo tunavyoyapa nguvu haya magenge hatari kuendelea kumea.. Tufike mahali tukatae huu unyama.
 
Nitoke kidogo kwenye Mada.....Ramadan Mubarak!!Kama hukuwahi kujua,au vile sikukiri hadharani...Niliipenda sana JF by then sababu ya michango yako,ukichagizwa na Marwa na Malaria Sugu!!..Mke wangu aliikupenda sana,mpaka leo namuita FaizaFoxy as utani,lakini umepotea sana Mama...LOVE youuuuuuuu!!

Thank you very much. Give my salaams to your loving wife, mwambie nimerudi.

cc. Invisible
 
Last edited by a moderator:

katika hali isiyo ya kawaida, polisi wanahaha kutafuta wahusika kwa nguvu kubwa tofauti na usiku tulipokua Muhimbili alipoumizwa Kibanda, na huenda hadi kesho akakamatwa mhusika.

"kwani kibanda ni nani hasa mpaka polisi wawe busy?" >Wassira
 
Mnajaribu kuhalalisha ujinga; hata adui yako ana haki zake. Vinginevyo kila mtu na mbaya wake eh? Sheria ya msituni.

Ujanja unauhalalisha wewe tu humu JF au siyo?

FYI, hakuna ahalalishae wala abatilishae kitu humu, tunaelezea ukweli ulivyo.

Vipi, ya Dowans na Symbion yalikushinda? hivi umeacha ufataani?
 
Back
Top Bottom